sidhani kama note 4 inachemka ovyo sababu hio ni simu ya mwisho kuwa na soc nzuri ya krait angalia mambo haya
1. simu yako ni version ya kimataifa, kuna matatizo ya watu kuuziwa simu za korea, usa nk simu ambazo zimeshachezewa sana wanakuja kushikishwa huku. nenda setting halafu about angalia aina yake version ya kimataifa inaishiwa na F au C kama sijakosea.
2. hakikisha hujaeka vitu vingi vinavyofanya kazi chini kwa chini, tafuta task manager yoyote angalia cpu, gpu na ram usage kama vinatumika sana angalia app gani inavitumia zaidi jaribu kuifunga kama ukiiifunga inajifungua itoe. task manager zipo nyingi playstore just search
3. simu haina warranty? note 4 ilitoka october 2014 warranty yake haijaisha unaweza wapelekea samsung. una mwezi mzima wa kwenda