Msaada: Nitapambana vipi na Mchawi?

Action aliyofanyiwa anko wangu kutoka katika afya njema mpaka kuwa katika ugonjwa hewa ndio nikaa mini kuna giza hapo


Action hiyo haiwezekani kivingine vyovyote vile ila kwa uchawi tu?
 
Kabla ya kuzama ndani tafadhali nifahamishe uelewa wako...kuhusu yafuatayo
Dunian kuna viumbe wa aina ngapi???
Unamjua firauni na vitimbi vyake..???
Unaujua moto??
Na jeunajua kuna nguvu za giza ??

Suala la duniani kuna viumbe wa aina ngapi linakuja vipi hapa na umuhimu wake ukoje?

Firauni alikuwa mtawala wa Masr.

Moto ni vitu vinapochanganyika na oxygen na kutoa nguvu inayotokana na mwendokasi wa chembe asili.

Nguvu za giza ni hadithi za tisha toto.

Unaweza kuthibitisha kwamba kuna nguvu za giza?
 
Dawa ya mchawi ni panga zile za shingo ndefu.
 

Hili jibu zur sana mkuu, habar za siku
 
Dawa ya mchawi ni panga zile za shingo ndefu.

Rais Ali Hassan Mwinyi wakati akiwa bado Waziri wa Mambo ya Ndani miaka ya 1970s alishawahi kujiuzulu kwa sababu kuna wazee wa mkoa wa Shinyanga waliuawa kwa tuhuma za uchawi.

Watu wakikuona una macho mekundu tu (hata kama unapulizia sana kuni kwenye kupika) basi mchawi.

Na vile nchi zetu huduma za afya ndogo, akifa mtoto jirani na huyu bibi, kesi anapewa yeye, mchawi, watu wnamuuilia mbali.

Ujinga, umasikini, maradhi.

Mpaka leo.
 
Jina la YESU ni nome, ni njia, ni uzima, "njooni kwangu wote msumbukao na kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha. Nenda mkuu nenda, litakavyoisha uatashangaa mwenyewe.
Amen to that. ONLY JESUS
 
Yaani wewe umeamua kuweka masharti kwenye maombi. Duh.

Hivi unajua Yona aliomba akiwa tumboni mwa samaki katika ukaidi wake na akaponywa? Na kuokoka ni nini? Unless awe analiitia jina la Yesu huku haamini kama ni mwokozi
 
Action hiyo haiwezekani kivingine vyovyote vile ila kwa uchawi tu?

Inawezekana lakini kivingine nilazima kungekuwepo na dalili zake...but sikuziona .....imetokea ghafla
 
Kama binadamu wa kawaida lazima utambue kuna viumbe wanao onekana kama wewe na yule na vingine visivyo onekana kama majini na mapepo
Nguvu za giza zipo tangu enzi hizo hata kabla wewe hujawa mtoto na watu waliiutumia sana sio tisha toto
Kwani wewe ulitambuaje firauni ni mtawala wa misri... na sio kwingine
 
Sikiliza mkali wangu.......kuna vijitu vinajifanya visomi haviamini uchawi ila uchawi upoo na unafanya kazi babu,achana na masharo hao wanaojifanya hawaamini coz wana kiDgrii kimoja sijui kitu gani,bob tafuta mganga mapemaaaaa la sivyo anko utampoteza hayo mambo yapo mwanangu wahiiii ohoo.......
 
Inawezekana lakini kivingine nilazima kungekuwepo na dalili zake...but sikuziona .....imetokea ghafla

Dalili gani?

Utajuaje dalili ambazo hujaziona?

Wewe ni mtaalamu wa forensic science?
 

Unaweza kuthibitisha uchawi upo?
 

asante kunifanya nicheke
 
Wewe na anko wako mwaminini bwana yesu atawapa nguvu ya kupambana na wachawi
 

Viumbe visivyo onekana umejuaje kwamba vipo na si stories tu?

Nimekuuliza unaweza kuthibitisha nguvu za giza zipo? Unaniambia ziko yangu enzi hizo kabla.mimi.sijawa mtoto, hilo si swali nililouliza.

Umejibu swali ambalo hujaulizwa, uliloulizwa hujajibu.

Firauni kuwa mtawala wa Masr is a matter of record. Kwingine wapi?
 
kwanini hujamzaba vibao wakati anamrushia uncle wako zongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…