Msaada nipo kifungoni

Msaada nipo kifungoni

fite fite

Senior Member
Joined
Feb 27, 2017
Posts
113
Reaction score
94
Wanajamvi poleni na majukumu,

Naomba nisiwachoshe sana kwa makala ndefu sana. Naeleza tu kwa ufupi ili niweze kusaidiwa maana hii hali inanitesa sana.

Nimekuja kwenye hili jukwaa nikiamini pengine ni tatizo la kiafya au la, watalaamu wa afya na wengine mnaoelewa zaidi ushauri wenu ni muhimu sana.

Mimi ni kijana mwenye miaka 24. Nina tabia zifuatazo

1. Nimekuwa naishi kwa kujitenga sana, muda mwingi nipo peke yangu na hata nikiwa kwenye mkusanyiko wa watu huwa najitenga na kukaa peke yangu.

2. Sina hata rafiki ninayemwamini wa kuongea masuala ya maana na ya maendeleo (kiufupi sina rafiki positively wa kunishauri nafikiri ni kutokana na jamii inavyoniona ninavyojitenga).

3. Nimekuwa naichukia sana jinsia ya kike imetokea automatically, hata kipindi nikiwa nasoma masomo yaliyofundishwa na walimu wa kike nilifeli yote sio kwa makusudi ilitokea hivyo automatically.

4. Napenda sana kukaa sehemu tulivu isiyo na kelele, sipendi kelele za radio, tv, simu, huwa napata maumivu makali ya kichwa ninapopata hizo kelele.

5. Katika mipango mingi ninayoipanga siimalizi, yaani sijawahi kupanga kufanya jambo na likafanikiwa hata kwa 50%.

6. Nikilala siwezagi kuamka ikitokea hakuna mtu wa kuniamsha naweza kushtuka saa kumi na mbili jioni na huwa bado nina usingizi mzito. Kiukweli nateseka jamani sipendi niwe hivi lakini nipo hivi.

7. Nina tabia ya kulamba sana asali mbichi mpaka nisipolamba naumwa (hili tatizo lilinianza 2012 nikiwa nasoma).

8. Mahudhurio yangu kwenye swala/Ibada ni hafifu sana sababu sipendi kelele zinaniumiza kichwa sana.

9. Nina tabia ya kunywa maji sana mpaka mkojo unakuwa mweupe na kufanana na maji kabsa. Ikitokea nimepitiwa na usingizi bila kunywa maji tumbo linaniuma sana.

10. Sipendi matembezi napenda kukaa nyumbani tu mpaka jamii iliyonizunguka inanichukulia kwa mtazamo hasi.

11. Sina raha na maisha yangu. Sina amani wala furaha ya maisha.

12. Nina shida ya masikio kutosikia kwa uzuri. mbali na hili sina tatizo lolote linaloonekana physically.

Kwa ushauri zaidi/rafiki positively
tuma ujumbe +255676 791 188.

NB: Masikio yangu yana hitilafu, nashauri ujumbe wa meseji tu.

Marejeo ya historical background yangu:

2004 niliwahi kupata matatizo ya macho nikiwa kwenye chumba cha mtihani. Ilinichukua miaka 7 kuyahangaikia na kupata nafuu.

2014 Niliwahi kuvamiwa na watu wasiojulikana wakanizimisha walinipora vitu nilivyokuwa nao. Fahamu inarudi nilishtuka nipo hospitalini madaktari wakasema nilichomwa injection ndio iliyopelekea nipoteze fahamu.

Naombeni msaada wenu, nami nataka niishi kama binadamu wengine niwe na furaha na amani bila kuwa na chuki na jinsia yeyote wala mtu yeyote.

Ujumbe huu ni wa kijana mwenye namba tajwa hapo juu. Hana account JF hivyo naomba ushauri utolewe zaidi kupitia namba yake.

Naomba kuwasilisha kwenu
Asanteni sana.
 
Aisee hiyo Hali ya kukaa pekee yangu ilinitesaga Sana siku nikajiuliza nateseka ya Nini Mimi kwani no mnyama nikajichanganya na raia
Sasa ivi naongea mpaka nawaboa najichanganya kila Kona mpaka jumuiya nasoma neno Nina furaha Sana

Ile kipindi nilikua nawaza alafu nachowaza sikijui
 
Ulifanyaje fanyaje?
Maana mwenzetu huyu amezidi mpaka hurumu ilinijia.
Aisee hiyo Hali ya kukaa pekee yangu ilinitesaga Sana siku nikajiuliza nateseka ya Nini Mimi kwani no mnyama nikajichanganya na raia
Sasa ivi naongea mpaka nawaboa najichanganya kila Kona mpaka jumuiya nasoma neno Nina furaha Sana

Ile kipindi nilikua nawaza alafu nachowaza sikijui
 
Ulifanyaje fanyaje...?
maana mwenzetu huyu amezidi mpaka hurumu ilinijia.
Asee mimi nilijikaza tu japo mwanzoni nilikuwa na hofu tunapiga story na washkaji sikai muda naaga kuna mahali nawahi kumbe la! Nilijikaza, nikawa naanza kuona mbona washkaji wananiona poa tu nikiongea wanasema umeongea point.

Nikaanzaa kujiamini washkaji wakawa wananifuata home asubuhi, tunaenda kupiga tizi. Nikaanza kuwa na marafiki sasa na woga ukaanza kupotea. Ila kuna saa ile hali inanirudia ila mpaka ipite muda sana. Naongea sana,napata ramani za pesa najiona nipo duniani.
 
Sifanyingi nilizozisoma ni una "Passive Aggressive Behavior" wewe mimi sio mtaalamu sana wahaya mambo lakini ukawaone watu Wasaikolojia tu wanaweza wakakusaidia lasihivyo kunakitu inaitwa "psychopath" inaweza ikakupata au ukawa nayo.
 
Sawa kiongozi tunashukuru kwa ushauri ingawa jamaa akienda kupima anaambiwa yupo vizuri hana shida.
Sifanyingi nilizozisoma ni una "Passive Aggressive Behavior" ww mm sio mtaalamu sana wahaya mambo lakini ukawaone watu Wasaikolojia tu wanaweza wakakusaidia lasihivyo kunakitu inaitwa "psychopath" inaweza ikakupata au ukawa nayo.
 
Hakuna ugonjwa hapo. Wewe mtoa mada ndo mgonjwa hasa. Nashauri kamuone haraka Mwanasaikolojia ili akutibu ugonjwa wako
 
Wewe ulikuwa unaogopa watu? Je kelele zilikuwa zinakuathiri pia? Hapo kwenye kulala sana mpaka kupitiliza masaa vipi? machiaveli
 
Ni bora kama ana smartphone ungemfungulia account hapa jf mana watu wengi n wazito kuanza kumtafta mtu kwa smu privately....na ndo mana wameanza kucomment hapa
 
Umeshawai kujichua yaani kupiga nyeto
Kama ndio ni mara ngapi kwa siku/Wiki ?
 
fite fite,
Kelele zilikuwa haziniathiri kwasababu nilikuwa nakaa ndani nafungua muiki mkubwa
Kuhusu kuogopa watu Ilikuwa hapana nilikuwa sipendi tu nikiongea na watu naingiwa na hofu au nakasirika naweza gombana au nikapiga mtu
 
Mahudhurio yangu kwenye swala/Ibada ni hafifu sana sababu sipendi kelele zinaniumiza kichwa sana.
Fanyia kazi hapa.
Ikiwa ukiwa katika ibada hali inazidi, we uwiache zidisha.
Sijajua dini yako lakin huenda ningejaribu kushauri zaidi, hapa ni Baadhi ya vitu huenda kiiman ndio maana nikasemea dini
 
Jibu moja kwa moja wewe ni melancholic,jibu la pili Shetani anakukimbiza.
Ha ha! Mkuu umeamua kumpasulia kabisa!!
ni introvert sawa lkn huenda akawa na matatizo ya kisaikolojia,hivyo ni heri akimbie haraka wakamshauli.
 
fite fite

mengi ya matatizo uliyo nayo ni ya ki-kisaikolojia na yanatukumba waTZ wengi, binafsi nimekuwa na matatizo kama ya kwako kwa miaka kadhaa na kwa sasa ( kwa mwaka wa pili hivi) nimeamua kukabiliana nayo just kwa kuwa 'positive thinker' na kwa sasa nimeanza kuyashinda mengi ya matatizo ya hayo, nimeachana na kunywa mavidonge ya depression. acha kujidharau, acha kujishusha shusha sana, jichanganye na jamii / ndugu waliopo, mara moja moja toka out uone huko nje pakoje, kuwa 'positive thinker' na mwisho mshirikishe Mwenyezi Mungu mambo yako yataanza kwenda,
 
Back
Top Bottom