Msaada nipo kifungoni

Msaada nipo kifungoni

Aisee kumbe saikology yaweza kuwa ugonjwa hatari sana.
Asante ndugu kwa ushauri hata mimi nimejifunza kitu hapo.
fite fite

mengi ya matatizo uliyo nayo ni ya ki-kisaikolojia na yanatukumba waTZ wengi, binafsi nimekuwa na matatizo kama ya kwako kwa miaka kadhaa na kwa sasa ( kwa mwaka wa pili hivi) nimeamua kukabiliana nayo just kwa kuwa 'positive thinker' na kwa sasa nimeanza kuyashinda mengi ya matatizo ya hayo, nimeachana na kunywa mavidonge ya depression. acha kujidharau, acha kujishusha shusha sana, jichanganye na jamii / ndugu waliopo, mara moja moja toka out uone huko nje pakoje, kuwa 'positive thinker' na mwisho mshirikishe Mwenyezi Mungu mambo yako yataanza kwenda,
 
Sawa ndugu asante kwa ushauri.
Fanyia kazi hapa.
Ikiwa ukiwa katika ibada hali inazidi, we uwiache zidisha.
Sijajua dini yako lakin huenda ningejaribu kushauri zaidi, hapa ni Baadhi ya vitu huenda kiiman ndio maana nikasemea dini
 
Sawa sawa mkuu. Shukrani kwa kushare nasi hali iliyokusumbua nawe.
Kelele zilikuwa haziniathiri kwasababu nilikua nakaa ndani nafungua mziki mkubwa
Kuhusu kuogopa watu Ilikua hapana nilikua sipendi tu nikiongea na watu naingiwa na hofu au nakasirika naeza gombana au nikapiga mtu
 
Kweli mkuu hiyo ni changamoto
Simu nzuri anayo lakini ndio hivyo ni mtu wa kujitenga sana hata kwenye social media hayupo kabsa. Labda nianze kumshauri na kumpa somo kadri muda utavyokuwa unaniruhusu.
Ni bora kama ana smartphone ungemfungulia account hapa jf mana watu wengi n wazito kuanza kumtafta mtu kwa smu privately....na ndo mana wameanza kucomment hapa
 
Nafikiri kuna sehemu umenukuu vibaya. Kwenye jamii kuna watu wana matatizo na wanateseka lakini hawana sehemu ya kusemea kutokana na sababu nyingi mimi nimecheza sehemu ndogo tu kulieleza tatizo lake ndani ya hili jamvi.
Nibarikiwe na nini? Kama tabia za makundi ya watu kama hizo siku hizi imegeuka kua magonjwa nahisi wewe ndo mgonjwa mkubwa sana
 
Nasoma nipone.nani napitia kama wewe.Ila mi nimekua hivi baada ya mama kuondoka.sina interest na wanawake mi nikukaa ndani.nje natoka kwenda kuhemea na kuangalia mechi ya Liverpool tu.nilikua mchamgamfu na afya but hii miaka miwili duh....
 
Mkuu kuna baadhi ya sifa tunafanana ingawa baadhi sina , katika maisha sio wote tuna hulka sawa au tabia fanani, mimi ni Introvert person(google kuhusu introvert). Nimejikubali nilivyo , sifa kuu ya sisi maintrovert ni kuwa tunapendelea lone time and we don't trust easily, msingi ni kuwa kama upo kama mimi yaani introvert nakushauri jitahid kuwa open minded walau jichanganye kidogo though ni mtihana sana kwa aina yetu mkuu
 
Pole sana mkuu.....Tafuta mlimbwende ambaye anayejua malavidavi matatizo yako yote yataisha.
 
Wanajamvi poleni na majukumu,

Naomba nisiwachoshe sana kwa makala ndefu sana. Naeleza tu kwa ufupi ili niweze kusaidiwa maana hii hali inanitesa sana.

Nimekuja kwenye hili jukwaa nikiamini pengine ni tatizo la kiafya au la, watalaamu wa afya na wengine mnaoelewa zaidi ushauri wenu ni muhimu sana.

Mimi ni kijana mwenye miaka 26 Nina tabia zifuatazo

1. Nimekuwa naishi kwa kujitenga sana, muda mwingi nipo peke yangu na hata nikiwa kwenye mkusanyiko wa watu huwa najitenga na kukaa peke yangu.

2. Sina hata rafiki ninayemwamini wa kuongea masuala ya maana na ya maendeleo (kiufupi sina rafiki positively wa kunishauri nafikiri ni kutokana na jamii inavyoniona ninavyojitenga).

3. Nimekuwa nawaogopa sana jinsia ya kike. Kuongea nao

4. Napenda sana kukaa sehemu tulivu isiyo na kelele, sipendi kelele za radio, tv, simu, huwa napata maumivu makali ya kichwa ninapopata hizo kelele.

5. Katika mipango mingi ninayoipanga siimalizi, yaani sijawahi kupanga kufanya jambo na likafanikiwa hata kwa 50%.

6. Nikilala siwezagi kuamka ikitokea hakuna mtu wa kuniamsha naweza kushtuka saa kumi na mbili jioni na huwa bado nina usingizi mzito. Kiukweli nateseka jamani sipendi niwe hivi lakini nipo hivi.

7. Kuwa na mawazo sana

8. Mahudhurio yangu kwenye swala/Ibada ni hafifu sana sababu sipendi kelele zinaniumiza kichwa sana.

9. Nina tabia ya kuwa na hasira za karbu

10. Sipendi matembezi napenda kukaa nyumbani tu mpaka jamii iliyonizunguka inanichukulia kwa mtazamo hasi.

11. Sina raha na maisha yangu. Sina amani wala furaha ya maisha.

12. Nina shida ya masikio kutosikia kwa uzuri. mbali na hili sina tatizo lolote linaloonekana physically.

Naombeni msaada wenu, nami nataka niishi kama binadamu wengine niwe na furaha na amani bila kuwa na chuki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba ushauri
Wanajamvi poleni na majukumu,

Naomba nisiwachoshe sana kwa makala ndefu sana. Naeleza tu kwa ufupi ili niweze kusaidiwa maana hii hali inanitesa sana.

Nimekuja kwenye hili jukwaa nikiamini pengine ni tatizo la kiafya au la, watalaamu wa afya na wengine mnaoelewa zaidi ushauri wenu ni muhimu sana.

Mimi ni kijana mwenye miaka 24. Nina tabia zifuatazo

1. Nimekuwa naishi kwa kujitenga sana, muda mwingi nipo peke yangu na hata nikiwa kwenye mkusanyiko wa watu huwa najitenga na kukaa peke yangu.

2. Sina hata rafiki ninayemwamini wa kuongea masuala ya maana na ya maendeleo (kiufupi sina rafiki positively wa kunishauri nafikiri ni kutokana na jamii inavyoniona ninavyojitenga).

3. Nimekuwa naichukia sana jinsia ya kike imetokea automatically, hata kipindi nikiwa nasoma masomo yaliyofundishwa na walimu wa kike nilifeli yote sio kwa makusudi ilitokea hivyo automatically.

4. Napenda sana kukaa sehemu tulivu isiyo na kelele, sipendi kelele za radio, tv, simu, huwa napata maumivu makali ya kichwa ninapopata hizo kelele.

5. Katika mipango mingi ninayoipanga siimalizi, yaani sijawahi kupanga kufanya jambo na likafanikiwa hata kwa 50%.

6. Nikilala siwezagi kuamka ikitokea hakuna mtu wa kuniamsha naweza kushtuka saa kumi na mbili jioni na huwa bado nina usingizi mzito. Kiukweli nateseka jamani sipendi niwe hivi lakini nipo hivi.

7. Nina tabia ya kulamba sana asali mbichi mpaka nisipolamba naumwa (hili tatizo lilinianza 2012 nikiwa nasoma).

8. Mahudhurio yangu kwenye swala/Ibada ni hafifu sana sababu sipendi kelele zinaniumiza kichwa sana.

9. Nina tabia ya kunywa maji sana mpaka mkojo unakuwa mweupe na kufanana na maji kabsa. Ikitokea nimepitiwa na usingizi bila kunywa maji tumbo linaniuma sana.

10. Sipendi matembezi napenda kukaa nyumbani tu mpaka jamii iliyonizunguka inanichukulia kwa mtazamo hasi.

11. Sina raha na maisha yangu. Sina amani wala furaha ya maisha.

12. Nina shida ya masikio kutosikia kwa uzuri. mbali na hili sina tatizo lolote linaloonekana physically.

Kwa ushauri zaidi/rafiki positively
tuma ujumbe +255676 791 188.

NB: Masikio yangu yana hitilafu, nashauri ujumbe wa meseji tu.

Marejeo ya historical background yangu:

2004 niliwahi kupata matatizo ya macho nikiwa kwenye chumba cha mtihani. Ilinichukua miaka 7 kuyahangaikia na kupata nafuu.

2014 Niliwahi kuvamiwa na watu wasiojulikana wakanizimisha walinipora vitu nilivyokuwa nao. Fahamu inarudi nilishtuka nipo hospitalini madaktari wakasema nilichomwa injection ndio iliyopelekea nipoteze fahamu.

Naombeni msaada wenu, nami nataka niishi kama binadamu wengine niwe na furaha na amani bila kuwa na chuki na jinsia yeyote wala mtu yeyote.

Ujumbe huu ni wa kijana mwenye namba tajwa hapo juu. Hana account JF hivyo naomba ushauri utolewe zaidi kupitia namba yake.

Naomba kuwasilisha kwenu
Asanteni sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dalili zako zinafanana na mwenye tatizo la depression. Naomba nikusaidie tafadhali.
 
Back
Top Bottom