Msaada, nini maana ya "Mahala ulipozaliwa"?

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
242
450
Habari wanajukwaa, naomba moja kwa moja niende kwenye uzi mfupi wa hiyo swali kama linavyosomeka.

Katika baadhi ya nyaraka mbalimbali ninazokutana nazo kama za kazini, NIDA, fomu za maombi ya kupigia kura, kujiunga na Chuo na nyaraka nyingine zinahozitaji kijua wapi ulipotoka au wapi ulipozaliwa utakuna kuna sehemu imeandika 'Mahala ulipozaliwa'.

Swali langu litachukulia kwenye huu mfano; Kwa mfano wewe ni mkazi wa Mtaa wa Shimo la Udongo, Kata ya Kurasini, tarafa ya Kurasini, Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam na wakati Mama yako anatarakia kujifungua siku hiyo ya wewe kuzaliwa alipelekwa Zahati ya Kata ya Kurasini ( hapo hapo mnapokaa) ila kutokana na changamoto za hapa na pale akalazimika kupewa rufaa kwenda Hospital ya Rufaa ya Amana iliyoko Mtaa wa Bungoni, Kata ya Amana, Tarafa ya Boma, Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Swali langu ni je, ukiulizwa Mahala ulipozaliwa unatakiwa uandike taarifa za wapi, kule Amana ulipozaliwa au Kule Shimo la Udongo utakaporudi na ndiko unakoishi siku zote?

Nawasilisha.
 
Wewe popote unapojiskia andika tu..Hata sio mambo serious san na waohaqwatakuja kukufuatilia..ni utamaduni tu katika ku collect data ila nothing serious
 
wewe akili ipo kweli? ...mahali ulipo chungulia Duniani rasmi kwa mara ya kwanza ni wapi bana? palee nurse wa labour ward alipojaza form zako ni hapohapo ulipokutanana jinai makata........ swali dooog hili mpaka uje kujaza saver humu??? au bado kattoto wewe
 
Back
Top Bottom