Msaada: Nini maana ya jina 'Dativa'

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
4,137
13,824
Kuna mtoto wa familia ya "mboga saba" anaitwa hilo jina na nimemuuliza maana yake nimejibiwa "sijui mama mwenyewe".
Nimejaribu kugoogle lakini nimeshindwa kupata maana yake.
Anayejua tafadhali.
 
Ngoja nimpigie demu wangu wa zamani make naye anaitwa dativa, ila kiukweli jina la dativa huwa ni wazuri balaaa!
 
Kuna mtoto wa familia ya "mboga saba" anaitwa hilo jina na nimemuuliza maana yake nimejibiwa "sijui mama mwenyewe".
Nimejaribu kugoogle lakini nimeshindwa kupata maana yake.
Anayejua tafadhali.
Dativa= ni neno la kilatin kwa kiingereza ni emissive. Ni jina la kikristo direct linahusu sifa za Mungu, mwenye uwezo wa kupita pote. Having power to radiate everything, mwenyezi anauwezo wa kuona yote. Kama mwanga unavyoweza kupenyeza vile vile na Mwenyezi anaweza kupita pote. Neno kuu ni mwenye uwezo wa ku "radiate" nk.
 
Wengi wa arusha wanalitumia sana hilo jina!
Nakumbuka mwalimu wangu Fulani pale udsm Dativa shilla!
Alikuwa chombo hatari......
Hebu watu wa arusha waje
 
Then ukijua itakusaidia nini?
Ya ngoswe muachie Mazoea.

Achakufuatilia vya watu
Heshima tele Wadau!

Kujua istilahi ya jina au tafasiri, asili nk ni kuondokana na ushabiki, ujinga, unazi, umaamuma nk.Akishafahamu huwezi kujua aidha kalipenda jina hilo (Dativa) hivyo anahitaji kujua maana ili kama pengine itakuwa tafsiri nzuri aweze kumpa mwanae au vinginevyo.

Wakati mwingine si lazima tu-comment, tu-reply chochote humu.Kama huwezi kuwa msaada kwa mleta mada basi ni busara, hekima na ustaarabu mwema kukaa kimya kuliko majibu ya kejeli, maudhi nk.

Mkuu Mwanga Lutila , Jina (Dativa) kwa mara ya kwanza nililisikia kanda ya kaskazini.Nadhani asili yake ni la kabisa la Wa-Maasai na utamkwaji wake ni Datipa na siyo Dativa kama linavyozidi kuswahilishwa na wengi wetu.

Tafsiri yake siifahamu ila siku nikiifahamu nitaileta humu.

Mwenye kujua asili, maana zaidi ya nilivyoielezea aongeze au apunguze nyama katika andiko hili.

Asalaam.
 
Wengi wa arusha wanalitumia sana hilo jina!
Nakumbuka mwalimu wangu Fulani pale udsm Dativa shilla!
Alikuwa chombo hatari......
Hebu watu wa arusha waje
Ni kweli Mkuu, Ngushi .

Pia kwa mara ya kwanza nililisikia Kanda ya kaskazini.Ngoja tuwasubiri wana-kaskazini au wajuvi watujuze.
 
Mkuu, sina uhakika kama hii ni maana rasmi, ila kwa msaada wa rafiki yetu google, nimepata hii;

DATIVA.PNG
 
Back
Top Bottom