Msaada: Nini hukumu ya kukimbia mikononi mwa Polisi?

MUSHEKY

JF-Expert Member
May 9, 2014
2,812
2,754
Habarini wakuu,

Nimeleta swala hili hapa jamvini kwa kua hapa ni jungu kuu na wajuzi wa masuala ya kisheria hawatakosekana

Nina rafiki yangu anaishi mkoani Simiyu aliingia matatizoni kwa kuuziwa simu ambayo ilikuja kubainika kuwa iliibwa mahali

Kesi tayari ipo Mahakamani na imeshasomwa kwa mara ya kwanza

Kilichofanya niandike huu uzi ni kwamba jamaa ni muoga sana na pia hawezi kujielezea

Wakati anahojiwa na Polisi alipokea kichapo kikubwa ambacho kilimfanya atimue mbio mita kadhaa kabla ya kudakwa tena na Polisi na kurudishwa sero

Jambo hili limefanya afunguliwe kesi nyingine ya ya kutoroka mikononi mwa Pollisi na kufanya idadi ya mashtaka kuwa mawili

Hivyo naomba msaada wadau kwa anayefahamu hukumu ya kuwakimbia hawa Polisi kifungo cha muda gani kwa mujibu wa sheria lakini pia kama ipo namna ya kumfanya huyu bwana anasuke kwenye kesi hii naombeni ushauri wenu wadau
 
Atua ya kwanza mtaftie dhamana kwanza hili awe huru hili kes yake ikiendelea.

Atua ya pili mtafte police anayepeleleza iyo kesi mumpe kitu flan hili adumaze ushahidi

Atua ya tatu mahakaman nikucheza na maneno mwambie asikubali kosa.

Atua ya nne watften mashahidi wote muwapoze ...kimtindo

Iyo kesi niyakawida sana mwambie uyo jama asiogope.
 
Pesa haijawahi kushindwa kitu.

CASH IS KING.
Na hapa ndo itakuwa pona yake,hiyo ya kukimbia siyo mbaya sana adili na hiyo ya kununua simu ya wizi kwanza.

Kingine mleta mada kama una access ya kuwapa elimu ndugu na jamaa zako waambie waache kununua simu za wizi ni mbaya sana mtu anaweza kukutana na case ya kichwa akaozea jela.
 
Kamuwekee dhamana halafu muwaambie hao polisi na huyo aliyeibiwa hiyo simu ya kwamba mnataka kumalizana nje ya mahakama. MONEY TALK! Labda kama aliyeibiwa alifariki kwenye hilo tukio la uporaji!
 
Atua ya kwanza mtaftie dhamana kwanza hili awe huru hili kes yake ikiendelea.

Atua ya pili mtafte police anayepeleleza iyo kesi mumpe kitu flan hili adumaze ushahidi

Atua ya tatu mahakaman nikucheza na maneno mwambie asikubali kosa.

Atua ya nne watften mashahidi wote muwapoze ...kimtindo

Iyo kesi niyakawida sana mwambie uyo jama asiogope.
Asante mkuu hilo la dhamana tayari
 
Nimejifunza kitu mkuu kuhusu kununua vitu mkononi kuna mtu alipatiwa kesi ya kuua kwa kununua simu
Na hapa ndo itakuwa pona yake,hiyo ya kukimbia siyo mbaya sana adili na hiyo ya kununua simu ya wizi kwanza.

Kingine mleta mada kama una access ya kuwapa elimu ndugu na jamaa zako waambie waache kununua simu za wizi ni mbaya sana mtu anaweza kukutana na case ya kichwa akaozea jela.
 
Kamuwekee dhamana halafu muwaambie hao polisi na huyo aliyeibiwa hiyo simu ya kwamba mnataka kumalizana nje ya mahakama. MONEY TALK! Labda kama aliyeibiwa alifariki kwenye hilo tukio la uporaji!
Kuna jamaa kaenda kumuwekea dhamana mshkaji wake alikua nguvuni na yeye katiwa nguvuni hata hajui jamaa yake kakamatiwa nini wameunganishwa wote kwenye kes moja ya robbery hii imekaaje kisheria?
 
Back
Top Bottom