NMB Songwe: Waandishi waishia Mikononi mwa Polisi. Walienda kumhoji Meneja Malalamiko ya Wananchi

Jul 14, 2021
5
5
WAANDISHI WA HABARI MIKONONI WAINGIA MATATANI BAADA YA KUTAKA KUPATA UFAFANUZI WA HABARI YA BANK.

Leo tarehe 21 /11/2023 Waandishi wa habari wawili mkoani Songwe Dicksoni Kapungu wa Global online Tv na Jamal Meena wa Jay Online Tv wamejikuta matatani baada ya kutaka kupata ufafanuzi wa malalamiko ya wananchi kuilalamikia Bank ya NMB ambayo ilitoa mkopo kwa Glant Mwalingo na kuzuia kuwapa hati ya dhamana baada ya kumaliza mkopo.

Wakizungumzia swala hilo waandishi hao wamesema majira ya saa 4 asubuhi walifika Kwa meneja wa Tawi la NMB Tunduma bwana Michae Kipanga kwaajili ya kupata ufafanuzi wa Malalamiko ya mteja aliyelalamikia Bank kushindwa kuwapatia dhamana waliyoombea mkopo baada ya kumaliza deni.

Baada ya kujitambulisha waandishi hao Meneja aliwaita polisi waliokuwa nje ya Bank na kuwaamuru wachukue vifaa na mabegi yaliyokuwa na vifaa kwaajili ya kuvifanyia uchunguzi ikiwa walikuwa wanarekodi kabla ya kupewa ridhaa au la.

"Sisi tulifika Bank mnamo saa nne asubuhi kwa lengo la kupata ufafanuzi wa habari ya malalamiko ya wateja wa Bank hiyo wakiituhumu Bank kutowapa hati walioombea Mkopo baada ya kumaliza deni.

"Tukiwa tunaendelea kumueleza Meneja tulichokifuata ghafla alimwita mlinzi wa Bank awaite polisi waliokuwa nje ili watuchue na kwenda kuchunguza vifaa vyetu ikiwa vinalekodi kabla ya meneja kukubali kuzungumza polisi walichuka Mabegi yetu na Simu na sisi pia mpaka katika jengo la ulinzi baada ya kupekua vifaa ikabainika hakuna rekodi

Mnamo saa nane mchana meneja aliamua kupiga simu kwa Mkuu wa kituo wilaya ya Momba kilichopo tunduma ili atuchukue na kwenda kufanyiwa upekuzi zaidi baada ya kufika kituo cha polisi bado haikuonekana rekodi ambayo meneja alidai amerekodiwa polis wakashauri Meneja na waandishi wazungumze na kumaliza tofauti nje ya kituo cha polisi amesema Dicksoni Kapungu."
 
Habari uchwara kabisa hii. Hapo wananchi wako wapi?

Sasa kama hizi ndo mnaweka kuwa habari basi mtakuwa busy sana na content ambazo hazina maana.

Yaani ukope, umalize kulipa benki ikatae kukupa nyaraka zako za dhamana?

Mkafunga safari kabisa kwenda kumhoji meneja . Mlikuwa mnataka rushwa nyie njaa mbaya sana.

Ningekuwa mie ndo meneja mngelala kabisa serooo kuhatarisha usalama eneo la benki. Muowaombe radhi wananchi wa Songwe /Tunduma waliokosa huduma ya huyo meneja. Kuna watu hawajapata mikopo kwa ujinga wenu.
 
Back
Top Bottom