Msaada: Ninasumbuliwa na hali ambayo siielewi

Msaada: Ninasumbuliwa na hali ambayo siielewi

Step by step

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2014
Posts
1,189
Reaction score
1,324
Habari ndugu zangu.

Ndugu yenu ninasumbuliwa na hali ambayo siielewi hivyo kama kuna mtu amewahi kupitia changamoto kama hii anipe muongozo.

Mimi ni jinsia ME Umri 33. Ninapokuwa na ratiba mpya au jukumu lolote mbele yangu au nikipokea taarifa yeyote ya kushtua au ngeni kwangu napata hali ifuatayo:-

1. Tumbo la kuhara linanibana hivyo lazima niende toilet.

2. Kichefuchefu cha hatari mate yanajaa mdomoni hali inayopelekea kutapika.

3. Dry throat, kuna muda najiona koo linakuwa kama limekaukiwa hivyo naanza kumeza mate, mate yakifika tumboni tu basi natibuka natapika.

4. Hamu ya kula inapotea, yaani hata nikisikia harufu ya chakula tu najisikia kutapika.

5. Kama taarifa hiyo nimeipata usiku na jukumu natakiwa kulifanya kesho basi usingizi utakata nikilala basi ni kidogo sana.

6. Mwili kuisha nguvu kabisa yaani mtu akiniona tu anaona niko dhaifu kama nimeumwa mwezi mzima.

HATUA NILIZOCHUKUA
Nilienda hospitali nikapima presha, figo, Hpyrol, sukari, Malaria vyote viko sawa na siumwi chochote.

MBINU NAZOTUMIA
Ikitokea nimepata jukumu jipya basi huwa nalikataa tu, siendi au natoa udhuru na ili niwe sawa basi natafuta dawa inayonipa usingizi na hamu ya kula inaitwa PHAMACTIN ya maji. Nikinywa hii baada ya muda nalala, na relax nikiamka nakuwa na nafuu naendelea na majukumu japo kwa udhaifu.

Itanichukua hadi siku nne kurudi kuwa normal kabisa. Hii hali inaniumiza, inanichosha sana naombeni msaada nianzie wapi?

Nawashukuru sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwili wa binadamu unafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa. Kama kuna kinachopungua mwili hutuma ishara.

pima damu ufahamu madini na virutubisho vinavyopungua mwilini
 
mkuu yafaa kuona wataalamu wa saikolojia, au yakufaa kujua kwanini wapata mshtuko kiasi hicho?

yawezekana mgeni akija kwako unawaza mengi sana kuwa atakula nini atalala wapi, atavaa ini, na kwenye kazi yawezekana unawaza sana kpitiliza labda je utaiwezaa, utamudu kuwa nje ya nyumbani?

So kunavingi ila lazima ujiangalie kwanini unashtuka pindi upatapo hizo taarifa? ukishajuaa unaweza fanyia kazi hilo,

Swali kwako, kipindi ulipokuwa shule ikifika kipindi cha mitihani ulikuwa katika hali gani? ulipopata kazi ulikuwa katika hali gani?
 
mkuu yafaa kuona wataalamu wa saikolojia, au yakufaa kujua kwanini wapata mshtuko kiasi hicho?
yawezekana mgeni akija kwako unawaza mengi sana kuwa atakula nini atalala wapi, atavaa ini, na kwenye kazi yawezekana unawaza sana kpitiliza labda je utaiwezaa, utamudu kuwa nje ya nyumbani? so kunavingi ila lazima ujiangalie kwanini unashtuka pindi upatapo hizo taarifa? ukishajuaa unaweza fanyia kazi hilo,

Swali kwako, kipindi ulipokuwa shule ikifika kipindi cha mitihani ulikuwa katika hali gani? ulipopata kazi ulikuwa katika hali gani?
Kipindi cha shule nilikua okey kabisa, ufaulu wangu ni wa juu sana. Hii hali imenianza baada ya kumaliza chuo kikuu.

Ni kama hali ya wasiwasi hivi au tension.

Nakumbuka kuna siku niko kituo cha mwendo kasi gerezani pale nikapigiwa simu kuwa shemeji angu amefariki basi dakika ile ile nikaanza kutapika na hali ikadhoofu balaa ikabidi nikae kwenye bench lisaa lizima ndo nikajikongoja kurudi home.

Ni hali ambayo iko very powerful ikinivaa mwili unakua dhaifu kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inatibikaje mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Matibabu yanaweza kuwa mabadiliko ya mfumo wa maisha , ushauri na dawa.
Ushauri kawaida huwa na aina ya tiba ya utambuzi kitabia. Dawa kama vile dawa za kutibu huzuni, dawa ya kutibu wasiwasi na hofu (benzodiazepini) au dawa za kudhibiti mapigo ya moyo , zinaweza kuboresha dalili.

pole sana mkuu huo wasiwasi lazima unaandamana na mawazo hasa yakutokuamini kuwa utaweza kuyakabili yaliyo mbeleni?
 
Una uzito kilo ngapi?
And toa mfano wa taharifa mbaya ambayo hupelekea hali hiyo.
 
Una uzito kilo ngapi?
And toa mfano wa taharifa mbaya ambayo hupelekea hali hiyo.
Uzito kg 67 mkuu sio mnene.
Mf nikiambiwa kesho tutaenda Mwanza basi usiku wa kuamkia safari lazma sitalala na asbh ntaamka natapika na kuharisha.
Sijawahi pata ajali wala msuko suko wowote njiani kwenye historia yangu ila tu najikuta nakua kama na wasiwasi au tension ambayo inanipelekea udhaifu wa mwili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi majukumu yenyewe nayopewa yako ndani ya uwezo wangu na nimekua nikiyafanya kwa muda mrefu tu ila nashangaa hii hali inanitokea. Yani kuna muda nikimuangalia mtu akifanya kazi kama yangu namuona kabisa anaifanya vibaya yani mi naweza fanya zaidi yake tena katika ubora wa hali ya juu kabisa ila napopewa mimi hyo kazi naumwa hoi kabisa.
Yani unaweza sema ni ushirikina japo siamini katika hizo mambo
pole sana mkuu huo wasiwasi lazima unaandamana na mawazo hasa yakutokuamini kuwa utaweza kuyakabili yaliyo mbeleni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzito kg 67 mkuu sio mnene.
Mf nikiambiwa kesho tutaenda Mwanza basi usiku wa kuamkia safari lazma sitalala na asbh ntaamka natapika na kuharisha.
Sijawahi pata ajali wala msuko suko wowote njiani kwenye historia yangu ila tu najikuta nakua kama na wasiwasi au tension ambayo inanipelekea udhaifu wa mwili

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda kwa mganga ambae sio wa sayansi.
 
Kimsingi majukumu yenyewe nayopewa yako ndani ya uwezo wangu na nimekua nikiyafanya kwa muda mrefu tu ila nashangaa hii hali inanitokea. Yani kuna muda nikimuangalia mtu akifanya kazi kama yangu namuona kabisa anaifanya vibaya yani mi naweza fanya zaidi yake tena katika ubora wa hali ya juu kabisa ila napopewa mimi hyo kazi naumwa hoi kabisa.
Yani unaweza sema ni ushirikina japo siamini katika hizo mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
1.Punguza kuwa perfect/sahihi saaaaaana kila wakati na kila dakika/sekunde

2. Usiogope kulaumiwa kila mtu huwa anakosea

3.Ingawa una hali ya kujiamini lakini inaonekana kuna past experience umeziweka kichwani either ulipitia jambo ukalikosea sana au ulipitia lawama flani hivi kipindi flani, hivyo inakuletea hofu

4.Kabla hujafanya jambo relax,tulia usifanye jambo lolote kwa pressure jitambuwe wewe ni boss wa akili yako hivyo usipende kupelekeshwa na mtu kwa taarifa yoyote

5.Tafuta daktari au mshauri wa mambo ya saikolojia na au hata wa kidini (in case ni mambo ya upande mwingine)

6Kama ni mtazamaji wa movies jifunze lakini usifanye comparison kwenye maisha

7.Weka kumbukumbu za matukio tangu hali hiyo imekupata

8.Kama kuna jambo unatakiwa uliboreshe au kulipa mkazo kama ni ujuzi au hali au tabia tilia mkazo ili upunguze hali hiyo

9. Usikatishwe tamaa/kutishwa sana na stori za watu wengine

10.Kuamini huleta kujiamini ridhika na kile unachokifanya usibase na ushindani uliopitiliza ni dhahiri utakuwa chini ya matarajio

si lazima yote hapo juu yawe yana relate, lakini machache yanaweza kusaidia
 
Jibu zuri hili hapa

Back
Top Bottom