Msaada: Ninasumbuliwa na hali ambayo siielewi

Msaada: Ninasumbuliwa na hali ambayo siielewi

Kimsingi majukumu yenyewe nayopewa yako ndani ya uwezo wangu na nimekua nikiyafanya kwa muda mrefu tu ila nashangaa hii hali inanitokea. Yani kuna muda nikimuangalia mtu akifanya kazi kama yangu namuona kabisa anaifanya vibaya yani mi naweza fanya zaidi yake tena katika ubora wa hali ya juu kabisa ila napopewa mimi hyo kazi naumwa hoi kabisa.
Yani unaweza sema ni ushirikina japo siamini katika hizo mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
pole sana mkuu fanyia kazi yale nlokushauri mwanzo ka utaona yanaweza kukusaidia pia omba kulingana na imani yako.
 
1.Punguza kuwa perfect/sahihi saaaaaana kila wakati na kila dakika/sekunde

2. Usiogope kulaumiwa kila mtu huwa anakosea

3.Ingawa una hali ya kujiamini lakini inaonekana kuna past experience umeziweka kichwani either ulipitia jambo ukalikosea sana au ulipitia lawama flani hivi kipindi flani, hivyo inakuletea hofu

4.Kabla hujafanya jambo relax,tulia usifanye jambo lolote kwa pressure jitambuwe wewe ni boss wa akili yako hivyo usipende kupelekeshwa na mtu kwa taarifa yoyote

5.Tafuta daktari au mshauri wa mambo ya saikolojia na au hata wa kidini (in case ni mambo ya upande mwingine)

6Kama ni mtazamaji wa movies jifunze lakini usifanye comparison kwenye maisha

7.Weka kumbukumbu za matukio tangu hali hiyo imekupata

8.Kama kuna jambo unatakiwa uliboreshe au kulipa mkazo kama ni ujuzi au hali au tabia tilia mkazo ili upunguze hali hiyo

9. Usikatishwe tamaa/kutishwa sana na stori za watu wengine

10.Kuamini huleta kujiamini ridhika na kile unachokifanya usibase na ushindani uliopitiliza ni dhahiri utakuwa chini ya matarajio

si lazima yote hapo juu yawe yana relate, lakini machache yanaweza kusaidia
Shukrani sana mkuu. Nitafanyia kazi kila neno hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na yote...

ila uliposema"unawaambia watu waende wao safari za kikazi"

Nakusubiri uwende taktari wa saikolojia ..pia na kisoma au maombezi upate!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzito kg 67 mkuu sio mnene.
Mf nikiambiwa kesho tutaenda Mwanza basi usiku wa kuamkia safari lazma sitalala na asbh ntaamka natapika na kuharisha.
Sijawahi pata ajali wala msuko suko wowote njiani kwenye historia yangu ila tu najikuta nakua kama na wasiwasi au tension ambayo inanipelekea udhaifu wa mwili

Sent using Jamii Forums mobile app
Una ANXIETY DISORDER,, ni tatizo la Afya ya akili so ushauri nenda uonane na daktari wa Afya ya akili atakusaidia naamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu haya ni maradhi ya wasiwasi (Anxiety Disorder)
Onana na clinical psychologist kwa counseling. Ila pia fanya haya kupunguza hiyo hali...

1.Deep breathing, kaa sehemu tulivu, fumba macho, vuta pumzi kwa nguvu kupitia pua, kisha itoe kwa mdomo kwa dakika kama 10,itakusaidia Kutuliza akili.

2. Ukiona umepata jukumu jipya, tulia, jiambie kuwa unaweza, na hakuna kitakachoharibika, jiambie mara nyingi uwezavyo kuwa kila kitu kitakuwa sawa.

3. Tafuta maneno ambayo utakuwa unayatamka kwa kuyarudia rudia huku unayapa uzingativu, unaweza kuanza kuhesabu kuanzia 100 kushuka chini mpaka moja huku ukizingatia bila kukosea, fanya mara nyingi kadri uwezavyo, husaidia kutuliza akili na ufahamu hivyo kuondoa wasiwasi.
4. Google mind relaxation techniques ujifunze namna Za kukabiliana na hali kama hizo.

Mimi ninapitia hali inayofanana na ya kwako, hizi njia zimenisaidia.

Google pia "How to calm down anxiety disorder" utapata ufahamu zaidi.

Vinginevyo nakuombea kheri ndugu yangu, najua ni namna gani unapata shida. Hauko peke yako, napitia hali hii pia.
 
Back
Top Bottom