Msaada, Nina simu yangu aina ya TECNO CX, Mpya Nataka Kuiweka Bondi.

Kazetela

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,612
2,000
bfa23cec6d99812d0fb4bdaca723a19c.jpg
dbd6c06ca5cf1f0e7d091ba5bc0868cc.jpg
33f83eb32f0e41750df7880050bafbaf.jpg
Habari zenu wana JF,
Jameni kama Kichwa cha uzi kinavyojieleza,
mimi ni kijana ambae nina ndoto nyingi tu za maisha na Mungu akisaidia nitazitimiza.

Juzi kati nilipewa zawadi na rafiki yangu mzungu kutoka USA. Bwana Lenox,Simu aina ya TECNO CX mpya toleo jipya.

Na mpaka sasa simu ninayo.
Lakini ndugu zangu mimi nina hali mbaya kiuchumi na hata vocha muda mwingine huwa nakoswa.
Sasa ili kukabiliana na ugumu wa maisha ningependa,nyinyi wana JamiiForums,Mnikopeshe kiasi cha Tsh.150,000/=.

Mtanipa hicho kiasi cha pesa kwa kuiweka simu hii Bond kwenu,kwa makubaliano ya kurejesha hiyo pesa badae,kulingana na makubaliano yetu tutakayoyafanya.

Siyo kwamba siipendi hii simu,la hasha.

Lengo ni kukuza kibiashara changu hapa ili angalau niweze kuukabili umasikini ulio tukuka.

Kwasasa natumia hiki kimeo changu cha zamani kuingilia humu JF na simu hii niliyopewa ama kuachiwa kama zawadi na rafiki yangu Bw.Lenox nimeitunza tu simu na wala sijaitoa kwenye karatasi zake wala maboksi lake,Naitamani na mimi kuitumia lakini hakuna namna.

Nawatakieni Jumapili njema.
 

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,281
2,000
Ina tatizo gani mkuu? Kuuza ama kuweka zawadi rehani siyo busara
 

REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,947
2,000
Asante sana kwa kunitakia juma pili njema, jumapili njema kwako pia ndugu yangu.
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,080
2,000
Unaonaje ukimwambia rafiki yako changamoto za maisha unazokabiliana nazo ili akupige Tafu?
Mimi nafikiri kama anaweza kukutumia zawadi kama hiyo basi hawezi kusita kukusaidia kama utamweleza kinagaubaga!
Jaribu mkuu...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom