Msaada, Nina simu yangu aina ya TECNO CX, Mpya Nataka Kuiweka Bondi.

Ilikiaje hadi mpeane zawadi, kashakuharibue
Ushaanza sasa ina maana kuwa na rafiki mzungu mpaka aniharibu?
Unajua kama huna hulka ya kuongea na watu utawaza hayohayo tu kama kama uliyepata fafafafafa
 
Dogo hyo simu kuweka bond naweza kukusaidia tatizo ukiahindwa kulipa mda tutakaokubaliana ndio mtihan utaona mm mkorofi,,,mm ninauza simu nipo dar ukitaka kuiuza uza moja kwa moja,ila bei ya jumla nakuambia ukwel ni 351,000 rejareja ni ujanja wako kuuza,na CX air ni 290000-305000 so hujasema yakwako ni CX au CX air... Kama unauza itakua salama zaid ila kama bond kwa watu wasiofahamiana unaweza dhulumiwa
Hata mm nimehofia kudhurumiwa maana watu wameitamani ile mbaya yan,Hii ni CX basi
 
Kwan kuna ulazima gan ya kusema rafik yako mzungu tka ulaya?si ungesema tu rafik yako inatosha?uswahil matatizo sana.

bfa23cec6d99812d0fb4bdaca723a19c.jpg
dbd6c06ca5cf1f0e7d091ba5bc0868cc.jpg
33f83eb32f0e41750df7880050bafbaf.jpg
Habari zenu wana JF,
Jameni kama Kichwa cha uzi kinavyojieleza,
mimi ni kijana ambae nina ndoto nyingi tu za maisha na Mungu akisaidia nitazitimiza.

Juzi kati nilipewa zawadi na rafiki yangu mzungu kutoka USA. Bwana Lenox,Simu aina ya TECNO CX mpya toleo jipya.

Na mpaka sasa simu ninayo.
Lakini ndugu zangu mimi nina hali mbaya kiuchumi na hata vocha muda mwingine huwa nakoswa.
Sasa ili kukabiliana na ugumu wa maisha ningependa,nyinyi wana JamiiForums,Mnikopeshe kiasi cha Tsh.150,000/=.

Mtanipa hicho kiasi cha pesa kwa kuiweka simu hii Bond kwenu,kwa makubaliano ya kurejesha hiyo pesa badae,kulingana na makubaliano yetu tutakayoyafanya.

Siyo kwamba siipendi hii simu,la hasha.

Lengo ni kukuza kibiashara changu hapa ili angalau niweze kuukabili umasikini ulio tukuka.

Kwasasa natumia hiki kimeo changu cha zamani kuingilia humu JF na simu hii niliyopewa ama kuachiwa kama zawadi na rafiki yangu Bw.Lenox nimeitunza tu simu na wala sijaitoa kwenye karatasi zake wala maboksi lake,Naitamani na mimi kuitumia lakini hakuna namna.

Nawatakieni Jumapili njema.
 
Back
Top Bottom