Msaada nina miaka 40 nataka kujifunza udrever..

Chuck j

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
2,359
2,000
Wapendwa wanagreatthinker,,,ninamiaka 40 sasa,nilikuwa na dill na mambo ya hotel,(barman) ..nataka kufanya kz ingine ambayo nitafanya kama ten years or 15 year kama mungu akipenda.. Nataka kujifunza udereva wa magari makubwa,malori yanayopeleka mzg nje ya nchi,,je itachukuwa muda gani mpaka kujua? 2,baada ya kujua kutahitajika kitu gani,zaidi 3 na unapata leseni daraja lipi?4gharama zake ni vp? 5 malipo yake yakoje(salary). Natanguliza shukranr.
 

PSM

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
542
0
Yani wewe unachekesha 40 Ndio uingie kujifunza gari,ulikuwa wapi ?kwa umri tafuta kazi nyingine Huo ni ushauri tu maana mpaka ukajue iyo gari kubwa kulimudu siyo Leo wala kesho ndugu,endelea tu na Huo u barman au kazi zakujiari zingine
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,194
2,000
mala nyingi udreva wa magari makubwa huanzia kwenye utingo,kama utapata dreva wa magari makubwa na akawa ana moyo wa kukufundisha baada ya muda unaweza kujua,then ukashughulikia leseni.
 

mtumishidc

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
510
250
wengi wao walianzia utandiboi kwenye hayo malori kisha wakawa madereva sikushauri kuingia huko maana udereva wa malori ni zaidi ya kuendesha gari na hasa kwa aina ya miundombinu tuliyonayo tanzania!
 

junior05

Senior Member
May 3, 2011
186
225
Mkuu timiza ndoto zako, age is just a numbers, kasomee udereva kisha tengeneza mazingira mazuri upige kazi
 

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
0
VETA ya Kihonda Morogoro na Chuo cha Usafirishaji DSM wanaendesha kozi ya truck driving. Jaribu kuwasiliana nao utapewa taarifa sahihi ili ufanye maamuzi sahihi pia
Umri usikufanye ukaacha kutimiza ndoto zako. Ulishawahi kumsikia Mzee Kimani wa Kenya? Alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 80!
 

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,213
2,000
........hakuna lisilowezekana chini ya jua, na usiruhusu mtu akatishe ndoto zako......cha kufanya nenda veta soma hapo ukihitimu katafute kazi kwenye magari makubwa, inawezekana usianze kama dreva lakini utapiga hatua kidogo kidogo na utafanikiwa.........
 

MLERAI

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
671
475
Kama wewe ni barman jiunge na saccos kakope ufungue simple pub wakati unajipanga ajira ni utumwa kwa umri wako nahakika hutakuwa tayari kutukanwa na hawa matajiri zetu.Pia ukianza safari za mbali uzeeni ukimwi utakuua kila mkoa una visawishi vyake,
 

Chuck j

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
2,359
2,000
Yani wewe unachekesha 40 Ndio uingie kujifunza gari,ulikuwa wapi ?kwa umri tafuta kazi nyingine Huo ni ushauri tu maana mpaka ukajue iyo gari kubwa kulimudu siyo Leo wala kesho ndugu,endelea tu na Huo u barman au kazi zakujiari zingine
nilikuwa nafanya kz,na hailipi kwa sasa na sio kulipa ni kuhusu kesho,
 

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
17,377
2,000
nenda chuo cha usafirishaji,usikatishwe tamaa umri sio mwisho wa ndoto zako if you are determined.Only death should be a barrier to your dreams
 

Chuck j

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
2,359
2,000
VETA ya Kihonda Morogoro na Chuo cha Usafirishaji DSM wanaendesha kozi ya truck driving. Jaribu kuwasiliana nao utapewa taarifa sahihi ili ufanye maamuzi sahihi pia
Umri usikufanye ukaacha kutimiza ndoto zako. Ulishawahi kumsikia Mzee Kimani wa Kenya? Alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 80!
asante kwa ushauri ndugu yangu,nitajitahidi kufuatilia huko kionda
 

Chuck j

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
2,359
2,000
........hakuna lisilowezekana chini ya jua, na usiruhusu mtu akatishe ndoto zako......cha kufanya nenda veta soma hapo ukihitimu katafute kazi kwenye magari makubwa, inawezekana usianze kama dreva lakini utapiga hatua kidogo kidogo na utafanikiwa.........
Asante asante sana kwa kunipa moyo,nitajitahidi kadri ya uwezo wangu,kuna jamaa yangu ni dereva wa hayo magari,kanishauri nifanye hiyo course,,,,yeye ni dereva wa truck.yeye hajasomea ila alijifunzia mitaani,na kanishauri niende shule ni bora zaidi.
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,349
2,000
Timiza ndoto yako kila kitu kinawezekana umri huo bado kwani ingekuwa ulikuwa huna kazi kabla hapo tungesema lakini kwa kuwa tayari ulikuwa na maisha yako kabla nina imani mambo yatakuwa mazuri kwani wakati unasoma udereva utakuwa unafanya kazi nyingine huku unaangalia namna ya kutimiza ndoto zako ikiwa pamoja na kujenga mazingira ya kupata rafiki ambae anaendesha gari kubwa kwa kupata uzoefu kidogo japo mara moja kwa wiki kuendesha angalau kilometre 100 (mia moja)

Ushauri wangu kwa wengine wanaokusudia kuwa madereva wa magari makubwa, itakuwa vyema kama kabla ya kujifunza kuendesha lori basi angalau hata uwe na ujuzi wa kuendesha gari ndogo ili hata ukienda kwa ajili ya driving ya gari kubwa tayari unakuwa unajua basics za driving.

kuhusu leseni ni Class E
 

Chuck j

JF-Expert Member
Jun 17, 2011
2,359
2,000
Nikweli nafanya kz,na nitakuwa naenda chuo,kuhusu urefu wa course na fees ukoje kaka?
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
9,539
2,000
Nani kasema kujifunza jambo kuna ukomo wa Umri?

Go, achieve your Dreams Bro..... Besides, you are only 40!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom