1. Kwanini kuna vikundi viiingi vidogovidogo vya majeshi ndani ya DRC? FARDC, FDLR, ADC, Wazalendo...
2. Wale maaskari wana mafunzo ya kijeshi au ni raia wa kawaida tu wanapewa magwanda ya kijeshi wavae?
3. Wanawapataje maaskari viongozi kama majenerali, kanali (wao wanaita Koloneli)?-je wana mafunzo mahususi ya kijeshi yanayowafanya wastahili kupewa hizo nafasi za uongozi?
4. Kwanini maaskari wao wanaongoza kwa kukimbia au kujisalimisha wakati wa mapambano?-Je hawataki kupigana au hawana mafunzo ya kijeshi au kunani hasa?
1. Kwanza hizo ni dalili za uongozi dhaifu.
DRC ina matajiri wengi wenye uwezo mkubwa, wakiwemo viongozi wa kuu hata na wa ngazi za juu jeshini na polisi.
Watu hawa wana machimbo yao ya madini, na hivyo kuhakikisha wana ulinzi mkali kutumia siraha za moto na za kijeshi. Watu hawa, wana uwezo wa kutumia wanajeshi wa serikali, kulinda mali zao na miradi yao binafsi.
Siku zote, hawawezi kuwa waaminifu wote. Kwa ukubwa wa nchi ile, ni kama kuna sehemu uongozi haujali. Hao huwatafuta wasafilishaji wa madini, kwa sababu hata raia wa kawaida wengi kazi zao ni kuchimba madini. Kutokana na tabia hiyo, watu hujikusanya kwa makundi, na wakisha kuwa na uwezo, huanzisha machimbo yao na kuwaasi maboss wao. Wageni wakiletwa maeneo hayo na kuwakuta wenyeji, mwishoe ni kama hivo.
Wengine ni makundi kutoka nchi jirani, ambapo waasi hao hupata hifadhi mapolini na serikali haishughuliki nao, hivyo kujisogeza mpaka kwenye makazi ya watu(raia).
2. Mwanajeshi ana umri wa miaka 70, na ameingia jeshini miaka 50 iliyopita. Unategemea ana nini huyo mpaka hapo? Hao hao, mishahara midogo, na haipatikani kwa muda. Wakijiunga na kuhangaisha raia, wanaishi kiubabe ubabe tu. Mafunzo hupewa mwanzoni, ila wakiona hakuna wa kuwajali, wanajiongeza wenyewe. Magwanda nadhani miezi iliyopita, uliweza kuona viatu vyao na nguo zimewekwa viraka. Kwa kifupi wajitafutie wenyewe, kikubwa silaha wanazo.
3. M23 imewavua nguo hakika umeliona hilo. Siku zote kwenye uongozi kukiwa ni kuvutana kisa mtoto wa mjomba, rafiki yangu , mtoto wa furani, mwisho wa siku ni kama ule.
Lakini pia, hata pamoja na vyeo vyao si kwamba wengine mafunzo hawana, vita vinaendelea, msaada wowote kutoka juu hakuna, bali ni kuhukumiwa kifo, nani atakuwa na nguvu ya kupigana?
4. Anaekuzidi nguvu, huyo huyo ndo unaenda nae. Afie nini? Mshahara asioupata? Maisha mazuri anayoishi?
Juzi kulikuwa na sakata la wake za wanajeshi waliouwawa,waliojisalimisha na waliokimbia. Walikuwa wakikaa kambini. Sasa, M23 ilipofika, si ndo ikakaba kambi, wakatolewa? Je, unadhani mwanajeshi huyo akiona familia yake haina pa kwenda, na anaitumikia nchi, akiwa na pa kwenda si lazima akukimbie!!! M23 inawapokea na kubadilisha mazingira yao ya kazi, ikiwemo na kupata mishahara yao kwa wakadi, na ahadi ya kuongezewa. Huku, familia zao zikiangaliziwa chochote wakati bado hawajapokea mshahara. Hao kwa nini wasikimbie?