Msaada: Nimeibiwa simu aina ya tekno K9 na IMEI zake ninazo

Mar 26, 2018
72
59
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu, jana nilikuwa kwenye harakati zangu za kutafuta tonge japo niishi, nikatoka Kimara nikawa nimeshuka Magomeni ili niende NIDA kufuatilia kitambulisho changu,nilitoka Kimara na usafiri wa mwendo mkasi nikashuka usalama ili nionane na mtu alafu niende NIDA.

Niliposhuka kwenye mwendokasi nikavuka barabara nikawa natembea kule road reserve kuelekea Magomeni hospitali,nikatoa simu mfukoni niwasiliane na mshkaji kwamba nitampata eneo gani pale?

Nikapiga simu, jamaa akapokea akawa ananielekeza ghafla nikashangaa simu imechukuliwa kutahamaki ni boda boda iliyotokea nyuma yangu,nikakimbiza bodaboda, nikaifuatilia kwa kutumia pikipiki nyingine lkn wapi akanipotea sikujua hata alienda njia gani.

Nina IMEI ya simu yangu, je nitafanyaje niipate simu yangu?

UPDATE 18-05-2018.
Cha kwanza nliamua kwenda police,baada ya kutoa ripoti na kila kitu,nikapangiwa mpelelezi baada ya kupangiwa mpelelezi sasa kila nikienda naambiwa ametoka mara njoo kesho asubuhi mara njoo kesho jioni na mimi nimuajiriwa kwa wachina,sasa mchina ashachoka na excuse zangu,sasa nikaamua kutafuta mtu wa TCRA akaniambia niende pale TCRA kuna kitengo kinashughulikia mambo hayo.na nliiwaambia ukweli police wananipotezea muda na kusababisha kibarua changu kuwa mashakani.
Nikishaenda pale TCRA Nitawaletea mrejesho.
 
Polisi huwa wanasaidia ingawa inachukua muda sana na anaweza kumpata mwizi akamalizana naye juu kwa juu na ugumu upo kwenye simu zenyewa akienda kubadili IMEI tu ndo basi tena mkuu na nyingi wazibadili kabla ya kuweka line
 
Nenda TCRA tu mkuu na pia pitia polisi wana kitengo cha cyber ingawa sizan kama kina msaada sna
Hawezi kuipata mkuu mtu akiiba simu huwa anachange imei chap kwa kua yey mwenyewe anajua madhara yake mkuu

me mwenyewe niliibiwa simu ilikua samsung s7 nilihangaika sana ila hamna msaada mkuu

possibilities za kuipata simu yako ikiibiwa labda uwe unatumia iphone tu tena sio kwa asilimia zote!!
 
tatizo la polisi wanazingua sana
 
ingekuwa smartphone kuna Apple inaitwa phone founder tungeipata kwake au kwa aliemuuzia ila kwa hiyo mwachie dada aende nayo
 
Hawezi kuipata mkuu mtu akiiba simu huwa anachange imei chap kwa kua yey mwenyewe anajua madhara yake mkuu

me mwenyewe niliibiwa simu ilikua samsung s7 nilihangaika sana ila hamna msaada mkuu

possibilities za kuipata simu yako ikiibiwa labda uwe unatumia iphone tu tena sio kwa asilimia zote!!
Kuchenji IMEI ni sawa na kula hela za jiwe, mafundi simu waliitwa na TCRA na wakaambiwa kuusu katazo la kubadili IMEI so akienda polisi then TCRA kama hawatataka rushwa basi either ataipata maana watajua imei hyo imetumika tena kwa namba ipi au cm itafungiwa. Na yote haya ni endapo hawatataka chambishi
 
Duuh, Sasa mkuu kila mtu Si anatumia simu kulingana na uwezo wake, ndo maana kukawa na iPhone kukawa na tecno
Sina maana hiyo mkuu namaanisha hivi kutumia simu kulingana na uwezo wako ndiyo sababu inayokufanya ukubaliane na matatizo kama haya kwa sababu tecno ni cheap inamaana hata device security yake haipo strong so inabidi akubaliane na kilichotokea tu

Kuipata inakua ngumu mkuu me mwenyewe nilipoteza s7 nenda sehemu zote police sijui imei ila hamna kilichosaidia
 
Kuchenji IMEI ni sawa na kula hela za jiwe, mafundi simu waliitwa na TCRA na wakaambiwa kuusu katazo la kubadili IMEI so akienda polisi then TCRA kama hawatataka rushwa basi either ataipata maana watajua imei hyo imetumika tena kwa namba ipi au cm itafungiwa. Na yote haya ni endapo hawatataka chambishi
Aaah ok itakua vizuri kama akifanya kwa njia hiyo anaweza ipata
 
Kuchenji IMEI ni sawa na kula hela za jiwe, mafundi simu waliitwa na TCRA na wakaambiwa kuusu katazo la kubadili IMEI so akienda polisi then TCRA kama hawatataka rushwa basi either ataipata maana watajua imei hyo imetumika tena kwa namba ipi au cm itafungiwa. Na yote haya ni endapo hawatataka chambishi
Mkuu sheria zimewekwa ili zivunjwe bado mafundi tuna change imei tena sana tu,wenyewe huwa tunaambiana hii ya moto ifanyie mambo,basi faster tu kitu badala ya kusoma k9 kinasoma tecno l8,sasa hao tcra wataipata wapi???
 
Yeah najua na pia kuwapata inakuaga raisi kama ikiwa ya moto sana iba ya mkubwa aaaaaaf ubadili uone
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom