Mitandao ya simu mjitafakari

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
10,518
19,885
Kuna hili suala la mitandao ya simu especially Airtel, Kupokonya wamiliki namba zao za simu na kuwapa watu wengine.,huku wakigoma kurudisha namba kwa mmiliki wa Kwanza hata kama namba haijapewa mtu.

Hili jambo limekuwa ni kero na tatizo kubwa ktk jamii., Na hii kwangu sio mara ya kwanza kunitokea, Utakuta mtu amesajili line kwa vitambulisho vyake halisi vya Taifa (NIDA). Ikatokea muhusika amesafiri nje ya inchi na kukaa huko kwa muda fulani ,,

Wao huchukuwa jukumu la kumpa mtu mwingine namba zile, Tena bila taarifa au kumjulisha muhusika wa Ile namba. Utakuta namba za aliyekuwa bodaboda, anapewa mtu ambaye ahusiani na kazi hyo, Au baharia anapewa namba za dalali wa vyumba,, Matokeo yake mtu anapigiwa simu apeleke boda boda mahali kuna abiria, wakati yeye ni mtu wa shughuli zingine wala ahusiani na boda boda, Au mtu anapigiwa simu anaulizwa chumba cha kupangisha wakati ahusiani na biashara hiyo ya udalali,

Basi shida tupu. Hivi watu wa makampuni ya simu, hamuoni kama mnavuruga networks za watu? Namba ya simu ni sawa na address ya mtu husika, Hamuwezi kumpokonya mtu contact yake muhimu na watu wake na kumpa mwingine,, Mimi nilisafiri nje ya inchi Kwa miezi 8 tu, Nilipokuwa nje sikuwahi kuzitoa line zote mbili Tigo na Airtel kwenye phone. Na zote nikawa natumia kwa whatsap,

Ajabu nimerudi nazipiga zote hazipatikani, Nikaenda Tigo mlimani wakanielekeza niende Tigo makumbusho, Pale tulizozana sn mwishowe wakasema, kwamba namba haiwezi kurudi sababu zimerudishwa TCRA ndy wamiliki wa namba zote za simu hapa Tanzania, So watafatilia kama wanaweza kuirudisha watanipigia simu, Ili niende kusajili upya na kupewa namba yangu, Hiyo inapaswa nisubiri kwa week mbili.,

Dah!! Nilihizunika sn,, niliondoka lakini nilipata moyo kwamba hii inawezekana kuirudisha, Nikaondoka kuelekea Airtel makao makuu Morocco, Hapo pia nilijieleza vizuri, na kuwaonyesha vielelezo vyote kwamba nahitaji kurudishiwa namba yangu ya Airtel ni muhimu sn ,

Airtel costumers care ,,walinijibu kwamba haiwezekani kabisa kurudishiwa namba ambayo imeshafungwa, Nikasisitiza kwamba mbona ikipigwa haiiti? inaonyesha hakuna mtu anayomiliki kwa sasa, ni bora mnirudishie namba yangu ina network za watu wangu na kazi zangu,

Airtel walikataa kuirudisha namba yangu,, Ilibidi nisajili namba ingine ya Tigo kwa muda, ili nijishikize wakati nasubiri week 2 kurudishiwa namba yangu ya Tigo.

Mauzauza

Baada ya kuwa hewani na hyo namba mpya,, nlianza kupokea simu na sms za ajabu ajabu kupitia namba Ile mpya, hadi nikaamua kuiweka pembeni na kutafuta namba ingine kwa muda, Huyu mmiliki wa namba hii mpya sijuwi alikuwa tapeli!!

Nilipokea simu mfululizo za vitisho na sms za ajabu, --Mara siku zako zinahesabika,, --Mara Lete ng'ombe mnadani basi ilikuwa ni vurugu tupu. Huku jamaa zangu nao nikiwapigia nao wanalalamika,, kwamba Ile namba yangu ya zamani ya Airtel ikipigwa anapokea mtu mwingine,, halafu wakimuuliza anatoa lugha chafu Kwa watu wangu.,

Sasa nikajiuliza,,iweje hawa Airtel washindwe kunipa namba yangu ambayo nimesajili kihalali na ina networks za kazi zangu, Ila wao wakaamua kumpa mtu mwingine? Tena ni kama a week after I claimed?

Ilinishangaza Sana, Niliishi kinyonge sn maana Mambo mengi nilisajili Kwa namba zile, Mfano kazini namba za contact ni zile za Airtel, Bank nikasajili na Tigo,

Baada ya week 2,, Tigo walinipiga simu nikasajili upya namba zangu, Lakini hawa watu wa Airtel ndy wamejifanya kichwa ngumu na namba zngu ambazo nimesajili Kwa vitambulisho vyangu vya NIDA wameamuwa kumpa mtu mwingine bila sababu za msingi.

Hivi hamuoni usumbufu mnaotupa Sisi wanainchi? Especially watu wanaosafiri nje ya inchi? Ifike mahali mtuwekee utaratibu wa kuzilinda namba zetu za simu, Ili zisibadilishwe, Kubadili umiliki wa namba, na kumpa mtu mwingine ni kuvuruga network za watu pamoja na kuleta taharuki Kwa ujumla. Airtel mnatatizo kubwa mahali,,mjitafakari.
 
Back
Top Bottom