Msaada: Nimeibiwa simu aina ya tekno K9 na IMEI zake ninazo

Sina maana hiyo mkuu namaanisha hivi kutumia simu kulingana na uwezo wako ndiyo sababu inayokufanya ukubaliane na matatizo kama haya kwa sababu tecno ni cheap inamaana hata device security yake haipo strong so inabidi akubaliane na kilichotokea tu

Kuipata inakua ngumu mkuu me mwenyewe nilipoteza s7 nenda sehemu zote police sijui imei ila hamna kilichosaidia
Nimekuelewa mkuu, Pamoja
 
Polisi hawana msaada labda kwenye wizi wa hiyo cm angakua amekufa mtu au aliyeibiwa ni mtoto wa kigogo, ukifika mtaa wa aggrey kariakoo watu wanacheza hadi na iphone
 
Naomba anayejua kubadilisha iMEI anisaidie na nijue
Lete milion 50 nikufundishe hata km TCRA wakinikamata na kunifunga miaka 20 nikitoka iweze kunisaidia. Ni makosa kubadili imei duniani kote ila kurepair imei siyo kosa sbb imei huwa zinacorrupt kwahiyo unarudishia iliyopo. Ukitoa battery utaiona imei yako halisi.
 
",,aahahah nadhan itakua vizuri kama mleta mada ataleta mrejesho wa mawazo aliyopata humu[/Q
",,aahahah nadhan itakua vizuri kama mleta mada ataleta mrejesho wa mawazo aliyopata humu
Cha kwanza nliamua kwenda police,baada ya kutoa ripoti na kila kitu,nikapangiwa mpelelezi baada ya kupangiwa mpelelezi sasa kila nikienda naambiwa ametoka mara njoo kesho asubuhi mara njoo kesho jioni na mimi nimuajiriwa kwa wachina,sasa mchina ashachoka na excuse zangu,sasa nikaamua kutafuta mtu wa TCRA akaniambia niende pale TCRA kuna kitengo kinashughulikia mambo hayo.na nliiwaambia ukweli police wananipotezea muda na kusababisha kibarua changu kuwa mashakani.
Nikishaenda pale TCRA Nitawaletea mrejesho.
 
Hawa watu wanataka pesa na mwisho wa siku watakulia pesa zako na kukuacha ukiduwaa. Angalia usipoteze kazi. Nunua simu nyingine achana na hiyo
N:B
Simu ambazo huwa zinafanyiwa kazi ni zile zilizoporwa kweny tukio la mauaji (mfano. Majambazi yamevamia, yakaua watu na kupora simu. Hapa ni faster tu inapatikana). Nyingine ni simu ya kigogo au ya mtoto wa kigogo (Simu za wakubwa) na ziliporwa kwenye tukio la uvamizi wa bank au taasisi kubwa.
 
Back
Top Bottom