Msaada: Nikikopesha mtu fedha sina bahati ya kurejeshewa

NDESSA

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Posts
1,945
Reaction score
1,801
Wakuu hii hali sasa imekua mbaya, huwa nikimkopesha mtu fedha iwe kubwa au ndogo hata awe mtu wa karibu kiasi gani au awe na uwezo kiasi gani jambo mojawapo kati ya matatu hutokea:
1. Kudhurumiwa fedha hiyo kabisa.
2. Kunilipa nusu nusu baada ya kusumbuana kwa muda mrefu.
3. Kucheleweshewa kwa muda mrefu sana.
Mpaka sasa nikikopesha na assume nimetoa sadaka kwa sababu hata nidai vipi huwa sirudishiwi kwa muda nilioahidiwa.
Mimi nikikopa fedha kwa mtu narudisha hata nikikwama kidogo nitamuomba mhusika radhi ila kwangu ni kinyume cha hayo.
Hili ni jambo la muda mrefu sana mpaka nimeamua kuandika hapa ni kwamba nimeona linanitesa sana na huwezi kuishi bila kusaidiana na watu.
Naomba kupata msaada kama situation hii ni kwangu tu au manake ni miaka mingi nimevumilia hali hii.
 
Hilo balaa hata mimi ninalo sana mpaka najiuliza why?! Mpka ndugu yako wa karibu kabisa nae anakudhulumu, inanisikitisha sana kwa kweli.
Hivi hii inakuaje make mtu anakudhulumu huku hauna ubaya nae na uwezo wa kukulipa anao,
Nimeshindwa kuelewa kabisa.
Hata iwe elfu kumi na mtu anayo hakupi
 
sielewi kabisa mkuu mpaka nikaanza kuwa na wazo la kumtafuta mshan jr anidadavulie, juzi jumapili kuna ndugu nilimkopesha tena kwa dharura alikuwa kapata biashara anatakiwa leseni ya biashara na hana akaniomba nimsaidie hela tena akiwa na hali mbaya maana biashara alikuwa na uhakika wa kuipata, kapata leseni kapata ile biashara nikmpigia cm ana nipa ahadi tu, jumamosi akaniambia atanipigia tukutane anilipe hakupiga, jumapili ananitumia msg. nilikuwa na kikao mahali nikachelewa sana naomba nikutafute jumapili, sikumjibu akatuma msg, nijibu pls sikujibu akapiga sikupokea maana kama anampango wa kunilipa atume tu kwenye cm yangu, habari za kuchekeana nimefika mwisho.
 
Nikikopesha mtu huwa nahesabia nimetoa Sadaka mpaka pale atakapokumbuka kuwa anadaiwa.

Hiyo tabia ya kukopa na kutolipa ndio imefanya watanzania wengi kuwa maskini.Wahindi na waarabu wameendelea sana sababu hukopeshana na kulipana ndio mfumo wao wa maisha.Ukiwa na duka unaenda kwa muhindi au mwarabu mwenzio anakujazia bidhaa duka zima hata liwe la jumla kwa mkopo unalipa taratibu kadri unavyouza.Mtaji wa mhindi na mwarabu ni uaminifu tu mtaji ambao watanzania wengi tunaudharau wakati ndio mtaji mkuu kuliko mitaji yote.

Waarabu na wahindi hukopeshana hadi mabilioni bila kuandikiana popote na hulipana.Mswahili ukimkompesha ukimpeleka hata mahakamani yeye anajifanya ndio mjanja kuwa siku uliponikopesha uklinipiga picha,onyesha picha.Yaani ni taabu tupu.

Kama tusipowaiga wahindi na waarabu kwa uaminifu wa kukopa na kulipa hatufiki mbali kama nchi,familia au marafiki.

WENZETU akitaka kuanzisha duka au kituo cha mafuta anaenda kwa mhindi mwenzie au mwarabu mwenzie mwenye mali za jumla anamjazia petrol station yake au ghala la duka anaanza biashara kwa kuwa kiwango cha uaminifu kiko juu mno.
 
Kama tusipowaiga wahindi na waarabu kwa uaminifu wa kukopa na kulipa hatufiki mbali kama nchi,familia au marafiki
Acha utumwa wa mawazo wewe kiazi hakuna watu wanaodhulumiana Kama hao! Kama hujui kitu kaaa kimya
 
Hiyo tabia ya kukopa na kutolipa ndio imefanya watanzania wengi kuwa maskini.Wahindi na waarabu wameendelea sana sababu hukopeshana na kulipana ndio mfumo wao wa maisha.Ukiwa na duka unaenda kwa muhindi au mwarabu mwenzio anakujazia bidhaa duka zima hata liwe la jumla kwa mkopo unalipa taratibu kadri unavyouza.Mtaji wa mhindi na mwarabu ni uaminifu tu mtaji ambao watanzania wengi tunaudharau wakati ndio mtaji mkuu kuliko mitaji yote.

Waarabu na wahindi hukopeshana hadi mabilioni bila kuandikiana popote na hulipana.Mswahili ukimkompesha ukimpeleka hata mahakamani yeye anajifanya ndio mjanja kuwa siku uliponikopesha uklinipiga picha,onyesha picha.Yaani ni taabu tupu.

Kama tusipowaiga wahindi na waarabu kwa uaminifu wa kukopa na kulipa hatufiki mbali kama nchi,familia au marafiki.

WENZETU akitaka kuanzisha duka au kituo cha mafuta anaenda kwa mhindi mwenzie au mwarabu mwenzie mwenye mali za jumla anamjazia petrol station yake au ghala la duka anaanza biashara kwa kuwa kiwango cha uaminifu kiko juu mno.
Umechambua vizuri.
 
Wakuu hii hali sasa imekua mbaya, huwa nikimkopesha mtu fedha iwe kubwa au ndogo hata awe mtu wa karibu kiasi gani au awe na uwezo kiasi gani jambo mojawapo kati ya matatu hutokea:
1. Kudhurumiwa fedha hiyo kabisa.
2. Kunilipa nusu nusu baada ya kusumbuana kwa muda mrefu.
3. Kucheleweshewa kwa muda mrefu sana.
Mpaka sasa nikikopesha na assume nimetoa sadaka kwa sababu hata nidai vipi huwa sirudishiwi kwa muda nilioahidiwa.
Mimi nikikopa fedha kwa mtu narudisha hata nikikwama kidogo nitamuomba mhusika radhi ila kwangu ni kinyume cha hayo.
Hili ni jambo la muda mrefu sana mpaka nimeamua kuandika hapa ni kwamba nimeona linanitesa sana na huwezi kuishi bila kusaidiana na watu.
Naomba kupata msaada kama situation hii ni kwangu tu au manake ni miaka mingi nimevumilia hali hii.

Hebu weka picha mkuu. Shukran.
 
Mtu anakuahidi mwenyewe atakulipa lini tena unakuta ana shida kweli kweli anatamani hata kulia lakini ukimpa akimaliza shida na hela kapata harudishi kabisa,
Mimi nimelizwa pesa nyingi mpaka unashangaa mtu umemuokoa kwenye shida flani lakini akipata hela wala hana time na wewe tena na anakuwa mkali mara nyingine.
 
Ushasema nawe kuna wakati unakwama ko ni obvious nawe huwa unawachereweshea watu hera yao. Kaa kimya.
 
Wakuu hii hali sasa imekua mbaya, huwa nikimkopesha mtu fedha iwe kubwa au ndogo hata awe mtu wa karibu kiasi gani au awe na uwezo kiasi gani jambo mojawapo kati ya matatu hutokea:
1. Kudhurumiwa fedha hiyo kabisa.
2. Kunilipa nusu nusu baada ya kusumbuana kwa muda mrefu.
3. Kucheleweshewa kwa muda mrefu sana.
Mpaka sasa nikikopesha na assume nimetoa sadaka kwa sababu hata nidai vipi huwa sirudishiwi kwa muda nilioahidiwa.
Mimi nikikopa fedha kwa mtu narudisha hata nikikwama kidogo nitamuomba mhusika radhi ila kwangu ni kinyume cha hayo.
Hili ni jambo la muda mrefu sana mpaka nimeamua kuandika hapa ni kwamba nimeona linanitesa sana na huwezi kuishi bila kusaidiana na watu.
Naomba kupata msaada kama situation hii ni kwangu tu au manake ni miaka mingi nimevumilia hali hii.
Kiukweli yataka moyo binafsi nikiwa na hela kwenye account mtu akaja kukukopa nimwambie sina? Nafsi inanishtaki nakosa lazima nimpe tu . Tatzo kurudishiwa imenifanya nimkosee Mungu kwa Hakika kutoa msaada ni huduma tusiache kuwasaidia wahitaji Mungu atatulipa kwa wakati wake tusipozimia mioyo cha msingi iombee fedha yako kabla ujaikabidhi.
 
sielewi kabisa mkuu mpaka nikaanza kuwa na wazo la kumtafuta mshan jr anidadavulie, juzi jumapili kuna ndugu nilimkopesha tena kwa dharura alikuwa kapata biashara anatakiwa leseni ya biashara na hana akaniomba nimsaidie hela tena akiwa na hali mbaya maana biashara alikuwa na uhakika wa kuipata, kapata leseni kapata ile biashara nikmpigia cm ana nipa ahadi tu, jumamosi akaniambia atanipigia tukutane anilipe hakupiga, jumapili ananitumia msg. nilikuwa na kikao mahali nikachelewa sana naomba nikutafute jumapili, sikumjibu akatuma msg, nijibu pls sikujibu akapiga sikupokea maana kama anampango wa kunilipa atume tu kwenye cm yangu, habari za kuchekeana nimefika mwisho.
Kweli Mchango wa Mshana Jr ni muhimu.
Mshana Jr pls pitia huku.
 
Wakuu hii hali sasa imekua mbaya, huwa nikimkopesha mtu fedha iwe kubwa au ndogo hata awe mtu wa karibu kiasi gani au awe na uwezo kiasi gani jambo mojawapo kati ya matatu hutokea:
1. Kudhurumiwa fedha hiyo kabisa.
2. Kunilipa nusu nusu baada ya kusumbuana kwa muda mrefu.
3. Kucheleweshewa kwa muda mrefu sana.
Mpaka sasa nikikopesha na assume nimetoa sadaka kwa sababu hata nidai vipi huwa sirudishiwi kwa muda nilioahidiwa.
Mimi nikikopa fedha kwa mtu narudisha hata nikikwama kidogo nitamuomba mhusika radhi ila kwangu ni kinyume cha hayo.
Hili ni jambo la muda mrefu sana mpaka nimeamua kuandika hapa ni kwamba nimeona linanitesa sana na huwezi kuishi bila kusaidiana na watu.
Naomba kupata msaada kama situation hii ni kwangu tu au manake ni miaka mingi nimevumilia hali hii.

= kudhulumiwa
 
Acha kucheza na pesa wewe yaani kulipwa pesa zako unaita BAHATI?
Wewe ni miongomni mwa wanaozifanya taasisi za kibenk na za kifedha nchini kufilisika.
 
Back
Top Bottom