Msaada: Ni ipi Health Insurance nzuri kwa familia?

Architect E.M

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,222
1,426
nawasalimu wakuu wa jukwaa hili. Heshima kwenu.

Nilikua naomba ushauri. mimi na mke wangu tumefunga ndoa siku za karibuni, na wote tumejiajiri, hivyo hatuna health benefits nzuri wanazopata waajiriwa wa makumpuni makubwa na wala hatuna uzoefu wowote wala information yoyote kuhusu bima za afya. Bado hatujaanza familia. lakini tunatarajia kuanza familia siku za usoni. kwa mantiki hiyo, tulitamani kujua ni health insurance gani nzuri, affordable, itakayoweza kucover hata masuala ya uzazi n.k...

Tulitamani kujua malipo average yakoje, na what exactly is covered. Pia hasara na faida zake.

Ninatanguliza shukrani za dhati.

Mbarikiwe sana,
 
NHIF iko poa sana, inapokelewa hospitali nyingi hata ukiwa katika wilayani vijijini huko.
 
Makampuni kwa sasa ni mengi, hapa tingehitaji ushuhuda kwa wale wenye kujua. Maana dhamani ya insurance utaiona pale tu mmoja kati ya wanafamilia atakapopata tatizo kubwa la kiafya, tujuilisheni wakuu. Ni ipi hasa insurance company nzuri?
 
Hivi kama unataka kukata yako binafsi ni shilingi ngapi? kwa anayejua anisaidie
Samahani kwa kudandia Uzi wako mtoa mada
 
Makampuni ya Bima yapo mengi sana mkuu ila makubwa kwa Tanzania ni haya.

1.AAR
2.JUBILEE
3.RESOLUTION
4.STRATEGIS
5.NHIF
6.........
 
Back
Top Bottom