Msaada: Neno hodi kwa Kingereza

Msaada: Neno hodi kwa Kingereza

Hakuna tafsiri ya moja kwa moja kwenda kwenye Kiingereza, instead unaweza kusema "Hello au Hello, anybody home" au kama unaelezea tukio la mtu kugonga hodi unasema mfano " He knocked the door but there wasn't any response"
Umeeleza vizuri isipokuwa kwenye kugonga, hodi inabishwa (kubisha hodi siyo kugonga hodi)
 
Nisaidie, ilitakiwa kuwaje mkuu.
Nimefafanua hapo juu kwamba badala ya kusema "kugonga hodi" ungesema "kubisha/kupiga hodi";

Unaweza kubisha hodi kwa kugonga mlango, kubonyeza kengele au kwa kutamka neno hodi ambapo kwa ung'eng'e ndo wanatumia hello there, somebody in there. Kwa asili milango yetu inikuwa haina milango kwa maana ya top na fremu, au ilikuwa inazibwa kwa aina Fulani ya miba au milango iliyosukwa kwa fito ambayo ukigonga sauti isingeweza kusikika na wenyeji, ndiyo maana ubishaji wa hodi ukawa ni wa kutumia kauli zaidi
 
Back
Top Bottom