bunyebunye
JF-Expert Member
- Apr 12, 2013
- 530
- 676
Salaam wakuu. Poleni na majukumu mbalimbali, mimi ni mhitimu wa chuo kikuu shahada ya biashara (Bachelor of Commerce), kwa mda wa miaka minne sasa sijafanikiwa kupata ajira na hivyo kupelekea akili yangu kukata tamaa kabisa. Matumaini yamerudi baada ya kutembelea jukwaa hili la ujasiriamali na kukuta thread nzuri zinazofundisha maswala mbalimbali ya kijasiriamali ikiwemo kilimo pamoja na ufugaji. Mfano kilimo cha mbogamboga ambacho huwa cha mda mfupi tu na huanza kumpatia mkulima japo kifuta jasho (pesa) Naomba ushauri wenu nifanye nini kwani kusema ukweli sina pesa kabisa ya kuanzisha mradi wowote tofauti na akili, vyeti pamoja na nguvu zangu binafsi ambazo ziko tayari kupambana. Naishi Dsm. Naombeni ushauri wenu ndugu zangu kwani palipo na wengi kuna mengi pia. Naomba samahani kwa nitakayekuwa nimemkwaza hivyo asije na lugha kali zisizo za kiungwana. Nawasilisha.