Pole sana ndugu yangu kwa hofu ya ndoto ulinayo, nijuavyo mimi ndoto zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni :-
1.Ndoto inayotokana na M/mungu ndoto hizi mara nyingi huwa zinawajia watu wema, yani kuna wakati mungu anawapa maono watu wema kwa njia ya ndoto, mf Nabii Ibrahim alipoteshwa juu ya kumchinja mwanaye wa pekee na akatambua kuwa ilikuwa ni agizo la m/mungu.
2.Kundi la pili ndoto zinazotokana na yale tunayoyawaza mchana, ubongo huwa na kawaida ya kuyarejea katika usingizi mf kuna wakati mtu anaweza kuwa anawaza ana pesa sana, au amesafiri nje ya nchi nk , fikra hizo ambazo unakuwa nazo wakati wa mchana zinaweza kujirudia ukiwa usingizini na kuwa ndoto.
3.ndoto zinazotokana na mapepo( ndoto mbaya kabisa) mf unaweza oteshwa unakimbizwa na mnyama,mf simba ama umegongwa n.k .
kwa mujibu wa maelezo yako unaweza tafakari na kuona ndoto yako imeangukia katika kundi lipi kati ya hizo tatu.
KINGA:
Hapa inatofautiana kwa mujibu wa mafundisho ya imani mbalimbali mf Uislam unafundisha ndoto mbaya zote kuwa ni zao la shetani/pepo kwa hiyo mtu anapaswa kuomba ulinzi kutoka kwa m/Mungu kwa kusema Audhbillah mina shetwan rajemi( yani najikinga kwako M/mungu kutokana madhara ya shetain aliyelaniwa),na wala hatodhulika mtu huyo , lakini pia yoyote mwenye kuota ndoto mbaya anakatazwa kuwahadithia wengine kwa sababu watu wanatofautiana imani ili wasizulike wengine.
kwa upande wa wakristo hakika sina ujuzi juu ya namna gani wanavyoweza kudili na hali hiyo.