Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,818
11,542
True story: Tea time,

Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.

Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una Waislam tupu. Nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.

Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo. Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.

Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.

Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.

Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.

Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.

Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.

Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.

Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?

Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).

Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu. Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.

Allahu akbar.

PS: Yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.
 
Karibu katika quran na sunnah.
Uislamu maana yake Kusalimika.

Achana na propaganda za dini hii kuhusishwa na Ugaidi

Hivi unajua kuwa kuoa mke zaid ya mmoja kuna hekma kubwa sana kwa Alie tuumba.

Wacha hiyo, hivi unajua uislamu ndio dini iliyokuna kufundisha watu kujilinda vizuri na najisi( kinyesi na mikojo).

Ntaendelea wacha kwanza nimalizie kazi.
 
True story: Tea time,

Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.

Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una waislam tupu. nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.

Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo.
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.
Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.

Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.

Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.

Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.

Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.

Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.

Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?

Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).

Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu.
Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.
Allahu akbar.

PS: yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.
hiyo ilikuwa ni ndoto toka kwa shetani mwenyewe, umepoteza focus na kitu kikubwa sana maishani mwako, kuna siku utakuja kujuta. lakini hata hivyo una nafasi ya kubadilika na umkiri Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako, uokoke kwasababu dhambi ya kwanza utakayohukumiwa nayo na ndiyo ambayo wanadamu watahukumiwa nayo ni kumkana Yesu Kristo kuwa Mwokozi wako. sikulaumu kwa hali uliyokuwa nayo kwasababu hata wakati unaota ulikuwa gizani, haukuwa tofauti na huko ulikokweda, kuwa mkristo wa dini hauna tofauti na waislam, kwahiyo haujabadili chochote umetoka kwa shetani ukaenda kwa shetani yule yule umebadilisha vyumba tu. ila kuwa Mkristo aliyeokoka (sio wa dini) ni kitu valuable na special, na ndicho kitakachofanya mtu auridhi uzima wa milele. hapo upo safarini kwenda jehanum ya moto wa milele. uamuzi ni wako.
 
Bado hujanishawishi aisee!! Mimi
na Kanisa langu la Roman Catholic Church, ni mpaka ukamilisho wa Dahari.
Nna Ndugu yangu mmoja yeye alianza tu ghafla akawa Mlutheri akakaa huko kidogo akahama akaanza kuvaa 'ushungi, baibui & nikabu' na jina akabadirishwa aikupita mda akaanza kupandwa na mapepo kuuliza nini maruhani hatuelewi nini kinaendelea duuh ghafla akahamia kwa Mwamposa akaenda huko baadae akachoka akarudisha mpira kwa kipa RC alipotoka, Maisha haya watu wanatangatanga sana aisee
 
hakuna mtu yeyote aliyewahi kubadili dini kuwa muislam halafu asijute baadaye, hasa wanawake. hayupo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom