Msaada: Nawezaje kujua taarifa ya figo zangu?

Full charge

JF-Expert Member
Mar 1, 2018
1,550
1,422
Nisipoteze muda, nawezaje kupata taarifa ya figo zangu kabla majanga hayajanikuta ukizingatia mimi naishi maisha ambayo siwezi kumudu hospitali ya zaidi ya laki moja (sina uwezo kifedha)?

Nikiangalia hizi maabara zetu nyingi huongozwa na vijana walioshindwa kuendelea na masomo, yaani wengi wao wamekariri tu mambo baadhi na hata vipimo majibu hutofautiana.

Naombeni msaada maana kuna hali siielewi yapata mwaka sasa, nachomwa sindano tu na kupewa vidonge vya UTI ila sioni mabadiliko yoyote.
 
Laki moja nenda tu hapo mloganzila, yaani wakupime tu, mashine wanazo, ila zaidi ya hapo usije sema nilikushauri.

Najua na huko Mhimbili ya jakaya kikwete wanapima, ujipange vizuri zaidi.
 
Nenda hospitali kafanye Kidney function test. Sasa humu unataka ushauri gani tena mkuu.
 
Laki moja nenda tu hapo mloganzila, yaani wakupime tu, mashine wanazo, ila zaidi ya hapo usije sema nilikushauri.

Najua na huko Mhimbili ya jakaya kikwete wanapima, ujipange vizuri zaidi.
Hivo vipimo bima inaweza kutumika??
 
Kwa hiyo pesa ni vyema usijikite kwenye kupima figo tu. Bali fanya consultation/ mwone daktari kwa kituo kinachoweza kufanya vipimo husika, ili uweze kuangaliwa na risk factors nyingine kwenye maisha yako zinazoambatana na kujeruhi au kuumiza figo na kushauriwa nini ufanye kuepuka hayo.
 
kujua usalama wa figo zako ni vyema ukapima utendaji kazi wa moyo wako pia, maana kuna changamoto za moyo zinaathiri figo pia.
Ushauri wa bure epuka sana kutumia antibiotics kwa muda mrefu
 
Kuna magonjwa hata ukijua awali kuwa unayo,hayazuiliki kutopata labda utaongeza tu siku za ugonjwa kuanA kuwa effective.
 
Mkuu nakudhauri hiyo laki 1 usiitumie kwanza. Bali jichange change kwanza angalau ifike TSh 192,000/= ili ukate bima ya afya ktk kifurushi Cha bei hiyo halafu ndiyo uende hospitali sasa.
Hii itakusaidia pia kupata dawa na vipimo vingine vya kutatua changamoto Yako kwa kipindi Cha mwaka mzima. Ahsante.
 
kujua usalama wa figo zako ni vyema ukapima utendaji kazi wa moyo wako pia, maana kuna changamoto za moyo zinaathiri figo pia.
Ushauri wa bure epuka sana kutumia antibiotics kwa muda mrefu
Hizi antbiotics zinagawiwa kama pipi huko famasi yawezekana ni chanzo kikubwa cha kuunguza viungo vyetu asee. Kibaya zaidi kila hisptal na kila unayekutana nae anakwambia amekutwa na UTI dawa alizoshika mkononi ni hizohizo ant biotics. Hatari sana
 
Mkuu nakudhauri hiyo laki 1 usiitumie kwanza. Bali jichange change kwanza angalau ifike TSh 192,000/= ili ukate bima ya afya ktk kifurushi Cha bei hiyo halafu ndiyo uende hospitali sasa.
Hii itakusaidia pia kupata dawa na vipimo vingine vya kutatua changamoto Yako kwa kipindi Cha mwaka mzima. Ahsante.
Aende hospital kwanza
Akafanye renal function tests (Serum creatinine na Blood urea nitrogen, BUN) ukikuta zipo juu, hyo ni ishara moja wapo kwamba Figo hazifanyi kazi vzuri
Pia aangalie vzur kiasi Cha mkojo anaotoa (normal ni 1500 to 1800mls per day)
Kwa setting niliyopo Mimi, hvi vipimo ni 5000 tu Kwa Kila kimoja
Kwahyo maabara ni sh 10, 000
Kama utakuta hzi renal function tests ziko raised basi further investigations kama abdominopelvic ultrasound (25,000), CT scan (200,000) ndo anaweza kufanya
Lakini primary ni creatinine na BUN na hyo urine output

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yana uhatari gani?,kwa Tanzania vifo vitokanavyo na Malaria na pneumonia kwa Wakubwa ba Watoto ni mara 1000 zaidi ya vifo vya sukari na figo.
Mkuu labda hujakaa kwenye hospital kubwa!
Kisukari na presha ndio wauwaji wakuu
Hawa watakusababishia Figo kufeli, moyo kufeli, strokena mambo lukuki
Malaria ipo lakini mpaka kuwa severe na kufikia kuua ni Kwa asilimia chache sana
Hyo pneumonia nayo sidhan sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi antbiotics zinagawiwa kama pipi huko famasi yawezekana ni chanzo kikubwa cha kuunguza viungo vyetu asee. Kibaya zaidi kila hisptal na kila unayekutana nae anakwambia amekutwa na UTI dawa alizoshika mkononi ni hizohizo ant biotics. Hatari sana
Na hii ndio changamoto nyingine Kwa nchi yetu
Watu wakiugua tu, Cha Kwanza ni kukimbilia pharmacy kununua dawa
Lakini hata mgonjwa akifika hospital na asipewe dawa yoyote, atalalama sana
Kwahyo imekua kama kasumba kunywa dawa
Lakini above all, kunywa dawa Kwa maelekezo ya daktari tena wakati ukiwa unaumwa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom