Msaada: Natafuta pots au vikopo vya kupada maua

mandingo 94

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
270
190
Habair ndugu jamaa na marafiki kijana mwezenu nipo mbele yenu nina shida kubwa sana inanitatiza mimi ninaishi Dar nataka kulima kilimo cha mbogamboga na matunda changamoto ni pots au vikopo vya kupandia maua sijui wapi kwa kuvipata.

Naomba mwenye kujua anasaidie hili

83626951_2733016403446966_3772705190875028703_n.jpeg
 
Hii type unaweza kuipata game pale Mlimani City. Kuna pots za ceramic hizo ni bei kidogo. Zipo kama wewe unaishi maeneo ya Mbezi beach au kawe utaona zipo nyingi.

Unaweza kuomba wenye makopo ya maji ya lita 3-tano wakupe au ununue. Unayamodify unatoboa chini na pembeni na unaotesha. Good luck.
 
Nashukuru sana
Hii type unaweza kuipata game pale Mlimani City. Kuna pots za ceramic hizo ni bei kidogo. Zipo kama wewe unaishi maeneo ya Mbezi beach au kawe utaona zipo nyingi. Unaweza kuomba wenye makopo ya maji ya lita 3-tano wakupe au ununue. Unayamodify unatoboa chini na pembeni na unaotesha. Good luck.
 
Inakuwaje mkuu. Inategemea unahitaji ngapi. Ila kama unataka nyingi tengeneza mwenyewe za zege ni gharama nafuu na rahisi kutengeneza. Chukua ndoo kubwa na ndoo ndogo. Weka udongo nusu kwenye ndoo kubwa.

Kisha weka gazeti au karatasi kati kati.paka oili chafu kwenye mzunguko wa ndoo kubwa kwa ndani. Ile ndoo ndogo paka nayo oili chafu kwa nje. Then koroga zege vipimo cement kipimo kimoja mchanga vipimo vitatu.

Mimi natumia beleshi moja iliyojaa cement na tatu za mchanga. Inatosha kwa kazi hiyo. Koroga vikiwa vikavu vichanganyike vizuri. Then weka maji kidogo then anza kwa kuweka zege ndani ya ndoo kubwa halafu weka ndoo ndogo juu yake then weka zege kwenye mzunguko kati ya ndoo ndogo na kubwa huku unatikisa tikisa mpaka ienee kote. Iache ikauke.

Baada ya masaa kumi, toa ndoo ndogo na toboa shimo la kutolea maji kwa bisibisi . kutokana na hali ya hewa acha ikauke kabisa then geuza ndoo juu chine utoe pot lako
 
Ni njia ya bei nafuu sana maana nimenunua mfuko wa cement sh 14,000/ = ndoo nimechukua mbovu nyumbani na oili chafu nilikuwa nayo. Pia sina ujuzi kabisa wa ujenzi useme ni mtaalamu.
 
IMG_20200505_150653.jpg
IMG_20200502_152232.jpg
IMG_20200502_152257.jpg

Hizi hapa baadhi ya picha. Zenye rangi nyeupe ndizo nilizotengeneza. Rangi tofauti nilinunua
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom