Msaada: Naomba ushauri wa gari Suzuki Jimny

Dodoma moja

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
307
175
1600371264151.png

Suzuki Jimny

Wakuu naombeni msaada wenu kwa mwenye uelewa kuhusu hii gari maana binafsi ilichonivutia ni kuwa juu na pia utumiaji wa mafuta sifahamu kuhusu gharama za spare pamoja na uimara wake.

Maana mim nahitaji gari ya kuzungukia kwenye shughuli zangu na kwa kuwa ninakofanyia shughuli barabara siyo nzuri ina mawe ndio maana nahitaji gari ndefu kutoka chini.

Asanteni!
 
Hiyo ni gari sahihi kwa mazingira yako, usihofie wala nini. Enginea za suzuki ni ngumu sana na kwa hiyo jimmy inamudu mazingira magumu vizuri. Upatikanaji wa spare sio tatizo, spares ziko na affordavle prices. Kwa hyo ningekushauri uikimbilie ruu
 
Hapa hata mimi nitapata mawili matatu, nakakubali sana haka kapya kalikotoka kuanzia 2018. Japo bei yake imesimama sana ukijumuisha pamoja na kodi ila kananishawishi sana.
 
Hapa hata mimi nitapata mawili matatu, nakakubali sana haka kapya kalikotoka kuanzia 2018. Japo bei yake imesimama sana ukijumuisha pamoja na kodi ila kananishawishi sana.
Hizo new model za suzuki Jimny bei yake ni ndefu sana.
Kama hiyo kwenye picha ya mleta mada hapo, kama huna 40milioni sahau kuimiliki.

Suzuki Jimny ni gari moja safi sana, ni imara, inapiga mazingira yoyote, fuel economy na affordable service cost. Kuna jamaa yangu anafanya kazi kwenye taasisi fulani ambayo kazi zao zipo town na porini na taasisi yao wao wanatumia Suzuki Jimny kwa shughuli zao, anasema hawapati shida yoyote, iwe jua iwe mvua.

Kwa mtanzania wa kawaida, kuweza kumiliki Suzuki Jimny ni vyema akawaza old model, kuanzia model 2002 kurudi nyuma. Naambiwa Kati ya 11-15milioni unaivuta from Japan.
 
muhamar Gadaf,

TRA pekee yake utawaachia si chini ya milioni 17 kwa hiyo ya kuanzia mwaka 2018, hapo sijamuisha na clearing fees zingine kwa wahusika wengine. Hao wengine kama bandari, wakala, n.k usipungue milioni 3 ya ki-Tanzania.

Kwa wastani bei ya hii Suzuki Jimny mpya utaipata kwa dola za kimarekani 16k ~ 17k (sawa na zaidi ya milioni 40 ya ki-Tz) hii ni baada ya ku-negotiate kidogo na watu wa upande wa pili yaani wauzaji. Kabla ya negotiations huwa bei zake ni zaidi ya USD 20k.

Jumla ya gharama mpaka nyumbani kwako yakupasa angalau uwe na kiasi cha milioni 60 (not less than USD 25k) hapa utapata iliyotumika kidogo ya mwaka 2019 au miezi ya mwanzo kabisa 2020.
 
muhamar Gadaf,

TRA pekee yake utawaachia si chini ya milioni 17 kwa hiyo ya kuanzia mwaka 2018, hapo sijamuisha na clearing fees zingine kwa wahusika wengine. Hao wengine kama bandari, wakala, n.k usipungue milioni 3 ya ki-Tanzania...
Duh!!!
 
Back
Top Bottom