Msaada: Naomba ushauri kuhusu mgogoro wa kodi ya nyumba ya kupanga

Kibee

New Member
Sep 9, 2021
2
0
Habari za saa hizi Ndg zangu! Polen na majukumu,

Samahani Sana Tena naombeni ushauri tu kwa anayeweza kunishauri.

Nlipanga nyumba mwaka Jana mwezi wa 11 nikalipa kod ya miez 2 Mana niliomba nilipe hivyo ilipofika January mambo yakawa mabaya Maana nategemea utalii Corona imekuwa janga sijpata kazi. Basi nikamuomba anivumilie nitampa ikafika mwezi wa 4 ikawa imefika 320,000 nkalipa 150,000 ikabaki 170,000 ikabidi tukubaliane kuwa niondoke niache baadhi ya vitu tukaandikiana baada ya muda flani nilipe nichukue vitu,lakini Kaka mwenye nyumba hakai hapo anakaa Mwanza akasema nisitoe kitu hata kimoja hadi nilipe hela na ameweka walinzi ili nisije nikaondoka kimya kimya

Nikamwambia kaka yako kasema hivi nawe unasema hivi akasema we nisikilize mimi, akanipa wiki 2. Badae hali ngumu nikakosa hata ya kubebea vitu ikabidi nimuombe japo ya usafiri niache kabati akasema wiki 2 zimeisha itabidi ukae ulipie huu mwezi nikamwambia shida ni kubeba vitu siyo sitaki kutoka

Basi ule mwezi ukaisha wakati hatupo mi nimesafiri nipo Iringa mke na mtoto wa miezi miwili walitoka, kurudi wakakuta kofuli mlango waliponitafuta ikabidi nimtafute awaruhusu walale kesho waondoke akagoma ikabidi mke aondoke na watoto usiku akaombe hifadhi ilikuwa saa 4 usiku.

Basi sikurudi hapo nyumbani tena, amenitafuta anasema nikatoe vitu nilipe kodi anayonidai pamoja na muda ambao vitu vimekaa nilipie.

Naomba ushauri kuhusu kulipia muda ambao vitu vimebaki maana sikufunga mimi mlango alifunga yeye.

Nifanyaje hapo haki itendeke?

Mwenye mawazo ya kunisaidia nitashukuru
 
Nenda kwa mjumbe kwanza umpe habari nzima ila pole sana kwa changamoto , God be with you.🙏
 
Back
Top Bottom