Msaada: Naomba kujuzwa taratibu za kupitia kuweza kufanya kipimo cha DNA

THE REPORT

Senior Member
Jan 13, 2021
167
201
Habari za wakati huu wanajamvi!

Kama ambavyo maada inajieleza, nataka kujua taratibu za kupitia ili niweze kufanya kipimo cha DNA. Yeyote anayejua anijulishe tafadhali

giphy.gif
 
Ohooo mtu ashachapiwa tayari wanawake hawa.
Pole mkuu ngoja waje wajuvi utapata tu majibu lakini kabla ya kusubiri jaribu kupitia nyuzi kadhaa kuhusu hayo mambo utapata tu majibu ( search DNA) JF watakuletea majibu tu.
 
Unaandika barua ya maombi,kwa ofisi ya ustawi wa jamii wa eneo lako.
  • Afisa ustawi watakujibi pia kwa barua
  • Hiyo barua utaichukua Hadi kwa hakimu au mwanasheria nae ataisaini
  • Then utaipeleka kwa ofisi ya mkemia mkuu wa serikali,ambapo utalipia laki moja,watachukua sampuli,utasubili majibu baada ya mwezi mmoja.
NB. Barua ya maombi lazima utoe sababu za kutaka kipimo Cha DNA, eg. familia, kijamii.
 
Kwa ajili ya nini mkuu?

Kama sababu ni mke kuchepuka nakushauri achana na hilo jambo, wewe lea mtoto.

Amina nakuambia mkuu, endapo ikawa sio wa kwako, maumivu utakayopata HUTOKUJA KUYAONDOA MAISHANI MWAKO KOTE. Lea mtoto, lea mama.

Achana na hizi, maumivu yake ni mazito mno, usithubutu kabisa.
 
ANZA kwenda kwa mwanasheria ama Ofisi za ustawi wa jamii then utapewa taratibu na,miongozo ili kufika ofisi za mkemia mkuu
 
Utakuta mwanamke anakupelekesha balaa kumbe mwana sio wako mwenye mtoto wake Hana hata stress anakula bata tu....
 
Inategemeana na upendl wake kwake mkuu.

Inashauriwa tu kama huwezi kuachana nae ni bora ukapotezea hizi mambo ila kama uwezo wa kumove on unao pima DNA kama sio wako unapiga chini kiroho safi kabisa
 
Acha hayo maumivu yanifike tu, ila ninaamini kuwa hii itasaidia sana kuwa salama kiakili. Sijisikii Vizuri kumhudumia mtoto ambaye sina uhakika kama ni wangu
 
Hii ni hatua ya mwisho kuelekea kwenye kuachana.....kabla ya kufuata utaratibu huu hakikisha ubongo wako ndio mratibu wa utaratibu mzima wa kufanya hayo maamuzi na sio moyo........

Kila la kheri kwenye safari yako ya ukombozi.......nina hakika utalivuka salama huku umesimam imara.....
 
Hawa ship Tanzania. Labda uwe na mtu US ununue kiwe shipped US akuletee hapa.
 
Huna haja ya kuvutana na mtu kuhusu iwapo wewe ni baba wa mtoto au hapana. Nimesema baba kwasababu wasiwasi wa aina hii mara zote upo kwa wanaume. Kuwa fulani ni mama wa fulani karibia mara zote hapana utata.

Basi wapo wanaopenda au ambao wangependa kufanya vipimo vya vinasaba(DNA) kuthibitisha kama ni wazazi kweli ama hapana. Nitaeleza utaratibu mzima hapa kutokana na Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba vya Binadamu ya 2009,Sura ya 73.

1. NANI ANAWEZA KUPIMWA DNA.
Yeyote ambaye anahitaji kujua kuhusu uhalali wa uzazi wake anaweza kupima DNA. Upimaji huu hauna umri. Hata hivyo DNA si kwa jili ya masuala ya kuthbitisha uzazi tu, bali hutumika hata katika masuala ya ushahidi na upelelezi.

2. NANI ANA MAMLAKA YA KUOMBA DNA KUPIMWA.
Si kila mtu anaweza kuomba kupima DNA. Hata kama mwenye uhitaji ni wewe lakini bado huna mamlaka ya kuomba kupima DNA. Kifungu cha 25(2) cha Sheria niliyotaja hapo juu kinawataja wafuatao kuwa na mamlaka ya kuomba DNA kupimwa. Kinamtaja hakimu ambapo kuna kesi/shauri fulani linaendelea, Wakili, afisa ustawi wa jamii, afisa polisi mwenye cheo zaidi ya inspector,daktari, na mkuu wa wilaya.Hawa ndio wenye mamlaka(Requesting Authority).Kwahiyo wewe ukiwa na shida ya DNA unaweza kumuona mmoja kati ya hawa ili aandae maombi ya kupima DNA na kuyapeleka kunakostahili.

3. MAOMBI YA DNA YANAPELEKWA WAPI
Kifungu cha 24 cha Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba kinaitaja maabara ya Vinasaba vya binadamu ya Mkemia Mkuu wa serikali kuwa na Mamlaka ya kupima DNA. Pia kinazitaja na maabara nyingine ambazo zitakuwa na leseni maalum ya kupima DNA kuwa na mamlaka hayo.

Kwahiyo maombi ya DNA yatapelekwa moja kati ya sehemu hizo mbili.
 
Back
Top Bottom