Msaada:Naomba kufahamu tofauti kati ya 'software engineering' na 'computer programming'

IT Guru

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
635
112
Natumai wote mu wazima wakuu. Kwanza ningependa kuwashukuru wote kwa michango yenu yenye burasa, mbarikiwe sana na muendelee na moyo wa kusaidiana.

Mimi ni kijana ambae nasoma form five kwa sasa na ninategemea kuspecialize kwenye mambo ya computer nifikapo chuo.

Ila hivi vitu viwili 'software engineering' na 'computer programming' huwa vinanichanganya na ninashindwa kujua tofauti yake maana huwa naona kama hivi vitu vyote vinahusu computer programs.

Naomba msaada wenu wakuu nipate fahamu vema tofauti kati ya haya mambo mawili.
Natanguliza shukrani zangu kwenu na ninawatakia pasaka njema....
 
Natumai wote u wazima wakuu. Kwanza ningependa kuwashukuru wote kwa michango yenu yenye burasa, mbarikiwe sana na muendelee na moyo wa kusaidiana.
Mimi ni kijana ambae nasoma form five kwa sasa na ninategemea kuspecialize kwenye mambo ya computer nifikapo chuo.
Ila hivi vitu viwili 'software engineering' na 'computer programming' huwa vinanichanganya na ninashindwa kujua tofauti yake maana huwa naona kama hivi vitu vyote vinahusu computer programs. Naomba msaada wenu wakuu nipate fahamu vema tofauti kati ya haya mambo mawili.
Natanguliza shukrani zangu kwenu na ninawatakia pasaka njema....


nikijaribu kukumbuka kwa haraka haraka,

Kwa kiswahili, Computer Programming; unaweza ukai-program computer bila kutengeneza software, nikiimanisha kwamba, unatumia programs zilizopo kuifanya kumpyuter ifanye unavyotaka.

Pia unaweza kuita computer programming, kama njia ya kuifanya computer ifanye unavyotaka kwa kutengeneza programs zako.

Inapokuja kwenye Software Engineering; hapa kuna vitu vingi sana vya kuangalia. kwa kifupi, ni namna ya kutengeneza software katika standards, njia (methodology) zinafahamika;
Yaani hauamki asubuhi na kuanza ku-program, hapana, isipokuwa unaanza kwenye upembuzi yakinifu (feasibility study), unakusanya mahitaji (software/system requirements), then unakuja kwenye design (hapa kunakuchagua tools kwa ajili ya ku-design pamoja na methodology), then unakuja kwenye coding, maintenace, n,k.n.k

kwa kifupi S.E ni pana sana ( hiyo computer programming inamezwa ndani)
 
Hizi term mara nyingi zinatumika interchangibly katika shule tofauti. Yaani Computer Programming Chuo A inaitwa Software Engineering Chuo B, Computer Science Chuo C na Information Systems Chuo D so kama unataka kufananisha bora uangalie syllabus usijali sana jina.

Although technically Engineering inatakiwa iwe focus more kwenye principles na methodology zaidi.
 
Nakushukuru sana mpendwa na pia mkuu kang. Angalau sasa naanza kupata mwanga juu ya haya mambo mawili. Ahsanteni sana
 
Computer programming inahusika zaidi na coding, ni kama art vile, ndiyo maana wanasema coding is poetry wakati software engineering inalenga zaidi kwenye ubora wa kutengeneza programs ambazo ni portable (mf utumiaji wa object oriented programming) na urahisi wa kuzifanyia matengenezo hapo baadae (low maintanance).
 
Computer programming inahusika zaidi na coding, ni kama art vile, ndiyo maana wanasema coding is poetry wakati software engineering inalenga zaidi kwenye ubora wa kutengeneza programs ambazo ni portable (mf utumiaji wa object oriented programming) na urahisi wa kuzifanyia matengenezo hapo baadae (low maintanance).

Shukran sana chamoto, angalau sasa naweza fanya maamuzi yangu vema nikiwa nina angalau idea juu ya haya mambo.

Asante mkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom