Msaada: Naogopa kazi mpya

Msaada: Naogopa kazi mpya

Habarini za humu wanajf,mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27.Nilikuwa na kazi katika taasisi moja hivi ya private sector amabapo nilikuwa napewa mshahara wa sh 1,000,000 kwa mwezi,katika harakat zangu za hapa na pale nikawa naomba kazi kwenye taasisi nyingine bahati nzuri nikapata,ambapo mshahara sasa ni mara mbili ya wa awali pamoja na marupurupu,ila naogopa na ninawasiwasi nitazingua kwasababu kazi hii mpya inahitaji umakini sana na kuwa sharp ambapo mimi huwa naona na mapungufu.Msaada wadau on how to go about it,hela ninaitaka ila naogopa maana hapa probation yenyewe miez 9
'Mboga ya majani penye mapendano Ni Bora kuliko ng'ombe mzima alienona penye magomvi'
 
Boss mapungufu kila mtu anayo

Watu tuliajiriwa vitu hatuvielewi tukaenda kujulia mbele ya safari mzee

Cha msingi ni usiwe mzembe tu

Labda uwe mmbovu sana ndo utaachishwa kazi ila vitu vidogo vidogo ni vya kueleweka

Ukibakia hapo kwnye huo mshahara kuna siku kitatokea kitu utajilaumu mara nyingi sana kwanini hukuhama

Bora uende ijulikane ilikuaje kuliko ukae kwa woga na mtu mwenyewe una expiriensi

Asante kwa ushauri wako
 
Kuna kazi nilikuwa nafanya awali nilikuwa naingia Kazini saa 2 asubuhi kutoka saa 10 Jioni. Mshahara kiduchu
Kuna kazi niliipata niliyotakiwa kuingia Kazini saa 1 asubuhi, kutoka saa 11 Jioni plus kuwekewa malengo na boss, Kila baada ya miezi 3 unatoa report na kufanyiwa tathmini, but mshahara ulikuwa almost mara 3 ya ule wa awali.

Nilichofanya ni kuji-twist kuendana nayo. Huwa najisemea, kama Kulala nitalala nikishafika miaka 60 huko nikistaafu.

Wakati huu wa Ujana ndiyo muda wa kujitesa ili kuhakikisha Tukizeeka hatuwasumbui watoto/ndugu kuombaomba hela za matumizi
 
Sawa ila nafasi zinapatikana so naumia kuziacha
Unahitaji ku grow na katika suala la kukua katika career lazima ukutane na changamoto mpya. Hayo mapungufu uliyonayo ilimradi umeshayajua utaweza kuyatatua.

Hilo pepo la kimasikini litoke kwa Jina la Yesu.
Nenda kaongeze CV na ufanye kazi kwa Bidii. Kuwa open minded katika kazi hiyo sehemu ambayo huelewei uliza wenye ujuzi watakusaidia.

Kila la kheri.
 
Kuna kazi nilikuwa nafanya awali nilikuwa naingia Kazini saa 2 asubuhi kutoka saa 10 Jioni. Mshahara kiduchu
Kuna kazi niliipata niliyotakiwa kuingia Kazini saa 1 asubuhi, kutoka saa 11 Jioni plus kuwekewa malengo na boss, Kila baada ya miezi 3 unatoa report na kufanyiwa tathmini, but mshahara ulikuwa almost mara 3 ya ule wa awali.

Nilichofanya ni kuji-twist kuendana nayo. Huwa najisemea, kama Kulala nitalala nikishafika miaka 60 huko nikistaafu.

Wakati huu wa Ujana ndiyo muda wa kujitesa ili kuhakikisha Tukizeeka hatuwasumbui watoto/ndugu kuombaomba hela za matumizi
Usijitese sana ndugu yangu..haya maisha tunapita..si umeona wanaume wanaisha tu na kuwaacha akina mama/wake zao tu.
Stress take your time ku enjoy ili mradi haumkosei muumba wako.

mimi bhana ni mara 100 niwekeze effort kubwa sana kwenye kazi zangu kuliko kumtajirisha mtu..
Mtu unamwingizia millions of money kwa mwezi mtu akipewa 1M per month anaona katoboa.
 
Habarini za humu wanajf,mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27.Nilikuwa na kazi katika taasisi moja hivi ya private sector amabapo nilikuwa napewa mshahara wa sh 1,000,000 kwa mwezi,katika harakat zangu za hapa na pale nikawa naomba kazi kwenye taasisi nyingine bahati nzuri nikapata,ambapo mshahara sasa ni mara mbili ya wa awali pamoja na marupurupu,ila naogopa na ninawasiwasi nitazingua kwasababu kazi hii mpya inahitaji umakini sana na kuwa sharp ambapo mimi huwa naona na mapungufu.Msaada wadau on how to go about it,hela ninaitaka ila naogopa maana hapa probation yenyewe miez 9
Kwanza nikupongeze kwa kufanikiwa kupata ajira mpya, jitahidi sana kujikubali wewe ulivyo usiwe unajilinganisha na mfanyakazi yeyote ktk utendaji wako, mtangulize Mungu mbele siku zote, thubutu jisemeshe wewe unaweza na utaifanya hiyo kazi iliyopo mbele yako maana ukijiogopa hivyo basi mambo yako binafsi hutajiwekea malengo yoyote hata ungalipata kiasi gani cha fedha.
 
Safi
 
Mkuu naomba nisaidie kama kuna nafasi na mimi mkuu. Nipate mishe angalau nipate ugali mkuu. Natanguliza shukrani zangu.
Kaa ulipo tu , kama ulipo ushajikita, pambana hapo .
Kuna dogo nilimtafutia kazi kwa showroom ya magari msahara +bonus alikuwa 1.2M hakosi kwa mwezi . Mazda na Honda wakaja wakitafuta wauzaji waliokomaa so wakamshawishi na 1.8M mshahara. Jamaa akajump ship kuendea hela , mwaka haukuisha akafutwa kazi na kubaki bila kitu . Pale alipokuwa zamani bado panaendelea mpaka leo . Be keen usipoteze vyote

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Usijitese sana ndugu yangu..haya maisha tunapita..si umeona wanaume wanaisha tu na kuwaacha akina mama/wake zao tu.
Stress take your time ku enjoy ili mradi haumkosei muumba wako.

mimi bhana ni mara 100 niwekeze effort kubwa sana kwenye kazi zangu kuliko kumtajirisha mtu..
Mtu unamwingizia millions of money kwa mwezi mtu akipewa 1M per month anaona katoboa.
Umesema sahihi Mkuu

Japo Waswahili wanasema Mtumikie Kafiri upate Mtaji wako.

Wakati unapambana kufanya kazi za watu, hakikisha una serve na kuanzisha biashara zako binafsi.

Ni jambo lisilo na Afya, ukipata shida hata ya milioni 3 inakushinda kuitatua hadi uanze kukopa Kwa watu.

Imagine ukishastaafu na hauna kipato endelevu si utakufa baada ya Mwaka mmoja
 
Habarini za humu wanajf,mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27.Nilikuwa na kazi katika taasisi moja hivi ya private sector amabapo nilikuwa napewa mshahara wa sh 1,000,000 kwa mwezi,katika harakat zangu za hapa na pale nikawa naomba kazi kwenye taasisi nyingine bahati nzuri nikapata,ambapo mshahara sasa ni mara mbili ya wa awali pamoja na marupurupu,ila naogopa na ninawasiwasi nitazingua kwasababu kazi hii mpya inahitaji umakini sana na kuwa sharp ambapo mimi huwa naona na mapungufu.Msaada wadau on how to go about it,hela ninaitaka ila naogopa maana hapa probation yenyewe miez 9
Nakuelewa sana mkuu

Kama unajijua hauna umakini jitahidi kila kazi inayotoka uifanye hapo hapo,hii itakusaidia kuihakiki mara nyingi uwezavyo...usisubiri deadline ndio uanze kukimbizana nayo

Jitahidi pia kusoma mambo yanayohusu hiko unachofanya
 
Huyu atakuw incompetent..

Mie kuna kazi niliwah fanya sikuw na kauli ya kusema kitu fulani sijui au sikifahamu. Napewa Task za senior officers ndio nifanye mimi Junior.

Nikitoka kazini natafuta watu wa taasisi zingine na kuingia ktk mitandao kuona hicho kitu kinafanyikaje exactly, then naunda sasa kile nachoona kinafaa.

Namshukuru Mungu, nilijua vi2 vingi nje ya level niliyokuw nayo, sasa hivi nimekuw mkongwe ingali umri ni mdg san ila kazi za Director nafanya vzr maana ndio yale niliyokuw natwishwa angali naanza kazi.

Kuwa flexible mtoto wa kiume
 
Habarini za humu wanajf,mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27.Nilikuwa na kazi katika taasisi moja hivi ya private sector amabapo nilikuwa napewa mshahara wa sh 1,000,000 kwa mwezi,katika harakat zangu za hapa na pale nikawa naomba kazi kwenye taasisi nyingine bahati nzuri nikapata,ambapo mshahara sasa ni mara mbili ya wa awali pamoja na marupurupu,ila naogopa na ninawasiwasi nitazingua kwasababu kazi hii mpya inahitaji umakini sana na kuwa sharp ambapo mimi huwa naona na mapungufu.Msaada wadau on how to go about it,hela ninaitaka ila naogopa maana hapa probation yenyewe miez 9
Endelea na kazi yako ya awali kama hujiamini na kama kuna probation miezi 9 ni hatari kwamba utakosa kazi zote na itakuwa majuto!
 
Kijana
Jitose kwenye kazi

Fanya kama kutongoza tu😁😁

Hujui kitakachotokea ila unatongoza

Unaweza pigwa kibao ila we unatongoza

Unaweza ukatukanwa tusi zito ila we unatongoza

Unaweza hata ukachaniwa shati ila wewe UNATONGOZA

Ila pia unaweza ukashangaa slope hii hapa mtoto akakubali hadi ukawa unajiuliza ulikua wapi siku zote hizo😂😂😂

Natumai utaenda kwenye hio kazi mpya
Hela hazionewi aibu mkuu
Hii kutongoza....imenikumbusha jamaa kashauriwa kumtongoza boss wake( mkurugenzi).... jamaa kweli baada ya kupambwa na wenzie akajitosa...kampa mama maneno....mama kaona duuh! Kijana pengine ana malaria kichwani...akamshauri rudi nyumbani kapumzike....wenzie wakazidi kumtia kichwa...ati mama keshakuelewa...wee nenda Katie kinywaji halafu mfuate nyumbani kwake........
Kwa kifupi imekuwa kama laana....mpaka leo jamaa anashinda kwenye mabanda ya wanzuki hakupata kazi tena....
 
Back
Top Bottom