Msaada: Namna ya Kumhandle Binti Aliyefeli Form Four

Hata mimi nina dada yangu (mdogo wangu) nilimlipia ada kubwa halafu amezungusha. Nilimnunulia vitabu vyote vinavyotakiwa lakini bado amefeli. Nilijaribu sana kumpa counciling na ushauri na mbinu za kusoma. Ila Tatizo la mabint walio wengi ni wavivu kusoma. Alikua akijua ndio narudi home ndipo huingia mezani na kusoma. Akijifungia chumbani anawasha taa, utadhani anasoma kumbe amelala. Sasa mtu kama huyu ukimbembeleza utakua umemsaidia au umefanya nini? Kikubwa ni kutokua mkali kupita kiasi, kwani unaweza kukatisha mtui tamaa na kufanya maamuzi mazito. Siku hizi watu hawaoni tatizio kupiga wanafamilia shoka, kumeza vidonge, sumu n.k. Ila kila Mtu amejaliwa kipaje chake. Mi nitakachomwambia, umefeli, tuliza akili alafu huko baadae useme fani yako ni nini? Ambayo itakuweka busy na kukuingizia kipato

hap sasa umenena...hii tbia ya kubembeleza ndiyo inawaongezea ujinga zaidi...anajua hata akifeli hakuna wa kumkemea. lakini ukijaribu kuwa mkali kiadogo inasaidia. wazo ulilotoa naliunga mkono mia/mia
 
Mwambie

1. Ulijitahidi kadri ya uweza wako, mitihani ni kipimo cha uelewa wako katika masomo husika na ku fail hamaanishi wewe hukuelewa au kutokujua kabisa la hasha, ni kwamba jitihada kidogo inahitajika ili mambo yawe sawa wakati mwingine.

2. Wewe una bahati kufika form four, embu waza wangapi wameshindwa kulipa ada na kushindwa hata kufanya mitihani yao na kupata div 4/3? wangapi wagonjwa? etc.....

3. Mwambie unampenda sana uko nae bega kwa bega kuhakikisha kuwa ndoto yake inatimia

4. Toa mfano wa ndg au rafiki unayemjua ambaye alirudia shule mara kadhaa na akafanya vizuri darasani/kimaisha

5. Kubwa kuliko salini pamoja kwa imani ya dini yenu na kunukuu maneno matakatifu yatakayomtia moyo

Nguli this is classic
 
Usithubutu kumkaripia hata siku moja au kumsimanga, hilo ni tukio ambalo hatasahau maishani mwake, kuna kijana alikuwa na akili sana baba yake akategemea atapata div I, matokeo kutoka yakawa mengine japo yeye ndo alikuwa kichwa wa mikondo yote, hadi leo hii anamchulia baba yake sana kwa kumtukana na kumtishia kumfukuza nyumbani. Jamaa alisota ila sasa ni mtu kati ya watu ila kwa juhudi zake mwenyewe mnake dingi alimtosa. Huwezi amini hata dingi aumwe hampigii simu wala kwenda kumsalimia baba yake mzazi. Inamuuma hadi leo hii.

AMEAPA HATAKAA AMGOMBEZE ALIEFELI MITIHANI MANAKE MAUMIVU YAKE UNAWEZA HATA KUJIUA:

Mpe moyo na alternatives ambazo anaweza kurudia mtihani manake umri wake nahisi utakuwa mdogo unaruhusu.

Mbona Anne Makinda alirudia mwaka IDM Mzumbe na sasa ni Spika wa jamhuri ya muungano wa TZ?

Mwambie asikate tamaa. Elimu darasa sio elimu maisha.
 
hakuna cha kumbembeleza kuwa mkali ili kama akirudia mitihani ajue kuwa alifanya ujinga. umbembelezeje wtk mda mwingi ndo hao hao wanaoandika nyimbo kwenye booklet, vibarua vya love,simu kwa viboyfriend kila saa na kuchakachuana> nimesahau madisko kila wekend nk bila kujaua anatakiwa kusoma> mdogo wangu alifeli form 6 last year div 4 nkashangaa hata D moja hana wkt form 4 alifaulu vema? eti ohh anapenda kuheshimu mawazo yake mwenyewe wkt wa kusoma na si kuzingatia ya walimu. Ukifika home mzabe cha fasta ajue kafanya upuzi na mweleze maisha bila elimu ni bure,....watu tunshindia chips dume mchana ili kulipa ada kumbe wanafanya upuuzi agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr mlete nimzabe kama huwezi
 
Mwambie

1. Ulijitahidi kadri ya uweza wako, mitihani ni kipimo cha uelewa wako katika masomo husika na ku fail hamaanishi wewe hukuelewa au kutokujua kabisa la hasha, ni kwamba jitihada kidogo inahitajika ili mambo yawe sawa wakati mwingine.

2. Wewe una bahati kufika form four, embu waza wangapi wameshindwa kulipa ada na kushindwa hata kufanya mitihani yao na kupata div 4/3? wangapi wagonjwa? etc.....

3. Mwambie unampenda sana uko nae bega kwa bega kuhakikisha kuwa ndoto yake inatimia

4. Toa mfano wa ndg au rafiki unayemjua ambaye alirudia shule mara kadhaa na akafanya vizuri darasani/kimaisha

5. Kubwa kuliko salini pamoja kwa imani ya dini yenu na kunukuu maneno matakatifu yatakayomtia moyo

Kweli umenena!! Ulisha kutana na haya ambo yakuweka watu sawa nini?!!!!!, cze unaonyesha uwezo Big up sanaaa
 
tayari kijana mmoja ambaye alikuwa amerudia mitihani huko moshi amekunywa sumu na hali yake ni mbaya.
Mdogo wangu wa kike alifeli mwaka 2008, mwaka 2009 alibaki nyumbani na kujisomea kidogo, mwaka jana akarudi shule kufanya pepa tena. Matokeo ni mabove amepata d3 only. Cjui nimwambie nini na atafanya nini?
 
Matokeo yanaonekana kuwa gharika maana amabao hawajaguswa ni wachache sana. Ukiangalia Div O ni nyingi mno ikifuatiwa na Div 4 (division ya vijana kama wenyewe wanavyoiita). Sasa hapo unashindwa kuelewa hawa vijana walidhani wameenda shule ili wakue au vipi maana kweli kwa mtu serious D mbili tu zinakushinda! Naona kama wanasoma wakiwa wadogo mno sielewi. Unajua wakishaona wanakula, kulala bure, kuvaa na kupewa vijisenti baaaaasi. Huwa hawaoni kuna siku nao watatakiwa wajitegemee.Kila saa wao na TV ,TV na wao wakati wewe uliye inunua wala huna muda wa kuiangalia.Wanajua ratiba ya vipindi vyote lakini mambo ya darasani hakuna kitu. Watoto hawasomi wanakaa kusubiri sijui tamdhilia gani ya usiku mpaka iishe saa tano.Atasoma saa ngapi? Ukimfukuza anaingia chumbani anafunga mlango anategesha sikio kwenye mlango angalau asikie tu hiyo tamthilia.Unajitahidi kumpa kila anachohitaji lakini wapi.Kazi kuchati kwenye simu tu.Laiti wangejua tunavyo hangaika ili wapate elimu!
 
kumfariji nini bwana...we kamchalaze bakora ili ajue kuwa umechukia...mtu kila siku ulikuwa unamwambia asome yeye anajifanya nyangema...halafu leo amefeli eti ukamfariji...ndio maana tunazidi kulea ujinga. kule china ukifanya ujinga wa hivyo wanakufunga kwenye kamba juu ya mti ili ujutie dhambi yako na siyo kuelezwa maneno matamu kama vile ulichofanya ni cha maana.....

Mkuu siyo wote wana "nyangema". kuna wengine wanakuwa wamekomaa kusoma ila ngoma siku yenyewe ikapiga chenga. kwa hiyo siyo vizuri kila aliyefeli apigwe bakora. twende case by case.
 
Nashukuru sana Kwa Michango yenu yenye Kujenga na Kutia Moyo

kaka uyo mdogo wako kapata ngapi? Usije ukawa unamsema wakati hajapa FLD?! Kama ana 3 au 4 hajafeli kwa viwango vya Tz. Kama ana 4 yenye kurange 30 pt and below usimkatishe tamaa,kama Vp unipm nimpe ushauri wa bure na nakuhakikishia atawashangaza wengi. Watu wanadhani kusonga mbele ni kwenda f5 hapana,kuna shortcut kibao na wenzie waliopata div.1 wakienda f5 na 6,wakimaliza wanamkuta tayari wanakaribiana kielimu. Ushauri huu nakupa wewe kukuliwaza ili uweze kumliwaza mdogo wetu! Where plan A fail,try plan B. Usiku mwema.
 
Nina mifano miwili ya kuonesha kuwa mtihani hautabiliki: 1. Mdogo wangu alikuwa serious na shule ile mbaya,f6 Azania akala div.3 ya mwisho. Akabahatika kwenda chuo kwa pre entry course. Kaenda Bachelor of Banking and Finance,na anamaliza mwaka huu. Leo hii yuko semista ya 5,ana A zote na B+ya ripoti. Uyu tuna uhakika atapata First class. PILI: kuna mtoto wa ndugu yangu alikuwa anacheza balaa,fom 1-3 full kucheza darasani ,nje ya darasa,nyumban n.k. Alipofika fom 4 mwenzi wa kwanza akatwambia "sasa naanza kusoma rasmi,mwenye material aniletee mezani naanza kazi" dogo alikamua na matokeo aliibuka na pt.7 div.1 na kuwa Top ten taifa. Kaenda PCM karuka na pt3 na sasa yuko mwaka wa 3 COET UDSM. In short,wanaoshauri atayeshindwa acharazwe si busara,mtu anaweza kuonekana wa mzaha lakini mwishowe akaja kuwa tishio. Waliofeli watie moyo wataibuka na mtashangaa!
 
tayari kijana mmoja ambaye alikuwa amerudia mitihani huko moshi amekunywa sumu na hali yake ni mbaya.
Mdogo wangu wa kike alifeli mwaka 2008, mwaka 2009 alibaki nyumbani na kujisomea kidogo, mwaka jana akarudi shule kufanya pepa tena. Matokeo ni mabove amepata d3 only. Cjui nimwambie nini na atafanya nini?

mwambie asikate tamaa,ni bahati mbaya tu!
 
Back
Top Bottom