Huyu ndio yule mwanafunzi alieandika mistari ya bongofleva kwenye mtihani wa form four 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu ndio yule mwanafunzi alieandika mistari ya bongofleva kwenye mtihani wa form four 2011

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by IrDA, Aug 19, 2012.

 1. IrDA

  IrDA JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  View attachment 62432
  Unakumbuka February 8 2012 wakati baraza la mitihani lilipotangaza matokeo ya kidato cha nne? stori kubwa ilikua mwanafunzi alieamua kuandika mistari ya bongo fleva kwenye sehemu ya kujibia maswali.

  “nashukuru sana wanaosahihisha mitihani hii ya shule yangu, nitakapofeli naendelea na fani yangu ya bongofleva, Majita wangu wako levo za juu na sio East Zuu, kukosa ni kawaida kwa binadamu” hiyo ilikua ni swali namba 6 na 7

  kwenye swali la 11 kwenye moja ya mitihani yake aliandika mistari ya bongofleva kwamba “acha utani my girl, unakuja nyumbani umezizi mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa mbaya”

  Baada ya hayo matokeo watu wengi ana walitamani kumfahamu huyu mwanafunzi, Jina lake la kuzaliwa ni Julius lakini la kisanii ni Elinaja, na ametoa sababu 5 za kwa nini aliamua kuandika hiyo mistari ya bongo fleva kwenye mitihani yake ya kumaliza kidato cha nne.
  Amesema “1 ni kutaka kutuma ujumbe kwa watu wanaosimamia Elimu kwa ujumla, sababu ya pili ni kutaka kusaidia watu wanaoteseka mtaani ambao wanaishi maisha magumu kwa sababu tu ya kushindwa kwendana na system ya elimu iliyopo ambayo ukishindwa kwenda nayo sawa umefeli, tulivyoumbwa kuna mtu anaweza akawa anashindwa kitu flani lakini ni mzuri kwenye kitu kingine sasa mfumo uliopo hautoi nafasi kwa wasioweza hiyo system, sababu ya tatu ni kutokana na utaratibu wa usaishaji wa mitihani kwa sababu sijui kama kuna mwanafunzi yeyote aliewahi kufanya mtihani wake wa mwisho alafu mtihani wake ukarudishwa ili kuona wapi alipokosa na wapi alipopata”
  “Sababu ya nne ni kuhusu wazazi kutambua uwezo wa watoto wao toka wakiwa wadogo kipi wanaweza kipi hawawezi ili kuokoa muda na pesa, sababu ya tano ni kwa serikali ijaribu kuweka shule za vipaji toka mwanafunzi akiwa mdogo kabisa, leo hii kuna mtu amepata degree pale chuo kikuu kasoma miaka mitatu na kupewa degree ya sanaa lakini hawezi kukuonyesha cheti hata kimoja kwamba alikua na elimu ya awali ya hiyo degree, huwezi kuniambia una degree wakati hukupata elimu ya msingi ya ulichosomea”
  “Kwa namna moja au nyingine sidhani kama nimefanikiwa kwa sababu nilichofanya watu walikichukulia tofauti sikufanikiwa ndio maana nimeamua kujitokeza kumalizia kazi ambayo niliianza kuifanya kule kwa sababu nafsi yangu ilikua inanisuta, ila kwa sasa watu watakua wameelewa na ninaweza kuwasaidia watu wengine” – Julius (Elinaja)
  Orginal source HUYU NDIO YULE MWANAFUNZI ALIEANDIKA MISTARI YA BONGOFLEVA KWENYE MTIHANI WA FORM FOUR, HIKI NDICHO ALICHOSEMA. « Millard Ayo
   
 2. Jiang Yang

  Jiang Yang Senior Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 111
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Elinaja anaujasiri, japo kuwa wengi wata comment kwa mtazamo hasi, ila ni mtu anayethubutu, na Tanzania tunahitaji kuona watu kama hawa wenye kuonesha uthubutu wa kufanya mambo.
   
 3. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  ana lolote huyo, mi namuona kilaza sawa na vilaza wengine tu...
  :)
  :)
   
 4. Gele vaheke

  Gele vaheke Senior Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utabaki ukweli kwamba anaye ongea ukweli tanzania hapendwi m4c fanya kazi
   
 5. Me370

  Me370 JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 995
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  m4c ni nini?
   
 6. somba kankara

  somba kankara Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna cha ujanja yaani miaka 4 umeipoteza na pesa pia harafu unakuja kuandika upuuzi eti kwa sababu hiyo we ni kilaza kwelikweli yaani hauna mfano
   
 7. Codon

  Codon JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Acha kujidai Kiziwi wewe!Nakama kiziwi Utaona tu!
   
 8. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamani dogo mwenyewe kasema alikuwa analazimishwa kuendelea kusoma.
   
 9. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Acha kutetea upuuzi!yaani unataka Tanzania ijaze watu wa hivi?vijana wengi kwa sasa wanaamini kwenye umaarufu na huo usanii, hawataki shule unadhani Taifa litakuwaje hili likianza kupromote starehe?TUtakuwa taifa la kuburudisha mataifa mengine!Hivi tu serikali imetait bado vijana hawapendi shule vp serikali ikiwapromote?...............
   
 10. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  wapi nimetetea huo unaouita upuuzi? Kukurupuka muda mwingine ni sawa na kujivua nguo tu.
   
 11. GreatMkubwa

  GreatMkubwa Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  dogo hajisomi anachokifanya, hapa ni bongo shule kwanza usanii badae,. atajulikana kwa ukilaza wake eti mtu ana digrii na hana elim ya awali y digrii yake!!! dogo hajajua watu wanamake kiasi gani na digrii thts y anatake easy tuu
   
 12. M

  MTENDAHAKI JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,992
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Nikutake radhi!Nilkuwa nimemlenga Musa17 kwenye post yake ya "Elinaja anaujasiri, japo kuwa wengi wata comment kwa mtazamo hasi, ila ni mtu anayethubutu, na Tanzania tunahitaji kuona watu kama hawa wenye kuonesha uthubutu wa kufanya mambo"
   
 13. a

  ally zomboko New Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :alien::alien::rant:
   
 14. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Huyo dogo kilaza kweli kweli!
  Si angeacha shule mapema ajiingize kwenye huo usanii?
  NECTA haikuwa sehemu sahihi ya kumwaga ushuz wake!
   
 15. Msimbo Pau

  Msimbo Pau Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dogo umefanya vizuri sana, huitaji kuwa na degree ili maisha yawe mazuri. Lakini pia usijione umetoka kwa kuimba pekeake. Hakikisha unajituma kujifunza kila inavyowezekana, katika kila pato unalopata tenga 10% for personal developments. HAKIKISHA UNAJIFUNZA KWELI NA UNAFANYIA KAZI. Ukweli ni kwamba DEGREE inaweza kukupa uhakika wa chakula lakini kweli ni kwamba hizi degree zetu tangu uhuru ndo zimetufikisha hapa. Wazazi wetu wengine wanadegree za vyuo vya nje lakini kawaida sana hawana jipya hata fungu la kumi wakitoa wanalalamika. Matunda ya degree zetu ndo nchi kuelekea shimoni.
  Dogo we ni JEMBE na madiliko hayaitaji majembe wengi, jembe mbele na wadau wengine nyuma.
  Hii nchi ukiongea jambo la kawaida watu wanashabikia na ukiongea kweli watu wanakuponda. Dogo hakikisha katika kila wiki unakaa na kuongea na wazee 65+ na watoto chini ya miaka 8 itakusaidia katika kuiona Dunia kwa jicho lingine. Elimu yetu sikubaliani nayo kabisa inazalisha wasomi wanaoona upande mmoja tu.
   
 16. data

  data JF-Expert Member

  #16
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,790
  Likes Received: 6,564
  Trophy Points: 280
  puuzi bongo lala hilo..
   
 17. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #17
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Ngoja tu afikishe miaka 25, atajutia alichokifanya.
   
 18. b

  bung'a Senior Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  maisha hayana fomula mimi kuna mtoto wa mjomba wangu nilianza nae chekechea mwaka 95 na wote tulikuwa hatuna akili lakini baba yake alikuwa na hela kwa hiyo akamlazimisha kusoma mimi nkaishia pale la darasa lakini mpaka leo yupo form 4 na atafeli tena lakini mimi nliwezeshwa nje ya shule nikaweza na sasa nina mambo yangu safi tu mpaka naenda sare na mwenye hiyo digrii
   
 19. Shaffin Simbamwene

  Shaffin Simbamwene Verified User

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 16, 2008
  Messages: 1,157
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Duh...!!! kweli wewe ni BUNGA
   
 20. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
Loading...