Default Matokeo ya form four hatima ya tanzania: Je nini kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Default Matokeo ya form four hatima ya tanzania: Je nini kifanyike?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Albedo, Jan 28, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Matokeo ya Form Four Yametoka, Kwa Mara Nyingine tena Zaidi ya Aslimia 80 Wamefeli. Tuyaangalie haya Matokeo katika Mtindo Mwingine ambao uko Tofauti na Mtindo ambao NECTA wametumia kuyawakilisha haya Matokeo kwa Jamii ya Watanzania, Mtindo ambao NECTA walitaka tuamini kwamba waliofaulu ni 50.4%


  Note: Idadi ya Wanafunzi waliofanya Mtihani ( Ukijumlisha Students and Private Candidates) walikuwa ni 441,271. Naomba niwazungumzie Only Student Candidates
  Jumla ya Wanafunzi waliofanya Mtihani ni 352840


  Divisheni One + Two + Three = 42,014 == 11.9%
  Divisheni Four = 135,826 =========== 38.5%
  Divisheni Zero = 175,000 =========== 49.6%
  Kwa hiyo Divisheni Four + Divisheni Zero Jumla yake ni 310,826 ====== 88.1%


  Tukae Tujiulize hivi hawa Zero&Four 300,000+ Ni nini Hatima yao? Kinachouma Zaidi ni kwamba Zaidi ya Asilimia 90 yao ni Watoto wa Wazazi wanaishi katika Lindi la Umaskini huku Pesa Zao zikienda Kufanya Shopping Dubai, Kosa lao nini hawa hadi Kustahili matokeo haya? Je Hii ni ndiyo Zawadi ya kuimba Nambari one eeeee eee Nambari one ni CCM? Je Tuendelee kulalamika hivi hivi kama Mwaka jana? Watanzania ni watu wa kusahahu hivi tunakumbuka mwaka Jana?


  Ngoja Niwakumbushe Kidogo


  Kuna Mtu ameshawahi kujiuliza Hatima ya hawa 65,708 wa mwaka 2009? Hivi hawa walimkosea nini Mungu?

  Ngoja niyaweke hivi ili Muelewe nini Nazungumzia


  ----------------------------------2009 ---------2010 ------------2011

  Divisheni ( One, Two and Three)....[FONT=&quot]42,672[/FONT]--------- [FONT=&quot]42,014[/FONT] ------------
  Disheni Four...............................[FONT=&quot]130,651.................[/FONT][FONT=&quot]..135,826[/FONT]
  Divisheni Zero............................ [FONT=&quot] 65,708[/FONT] [FONT=&quot] ....................175,000 [/FONT]

  Nauliza Tena Tuendelee kulalamika ili Mwaka huu tena yatukute kama haya?

  Ningependa sana JF kama Jukwaa la Great thinker tulijadili hili Suala ambalo mimi naliita ni Janga la kitaifa, tusilifanye likwa ni la Kidini (maana nimeshaona Baadhi ya watu wa Dini moja wakiwacheka wenzao na wenzao wakilaumu Serikali kuipendelea Dini Nyingine). Unapaswa kuwa Mjadala wa kitaifa wenye Lengo la Kuonesha Suluhisho juu ya Tatizo hili kwa manufaa ya watoto zetu, wadogo zetu na Taifa kwa Ujumla

  Wana JF Nimamua Kuchokonoa Huu Mjadala naomba Tuchangie tukiwa na Tunatambua kwamba Watoto wa Maskini bila Kujali Dini zao wala Makabila yao Maisha yao yako hatarini.

  Karibuni sana

  Angalizo: Tusiingize Mambo ya Dini katika Mijadala yenye Tija kwa Taifa Letu
   
 2. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Shule za kata ni shule za kisiasa majukwani kwamba tumejenga shule kila kata ila hakuna kitu,we shule nzima walimu 2 mpaka 4 unategemea nini yani hapa tusifichane serikali imefuka kuzileta bila kuandaa mikakati madhubuti na hali inavyo endelea ndo watazidi kufeli maana hata ule mchujo wa kidato 2 wamesha utoa, yani serikali ya ccm wanafanya vitu bila kuona mbele wakisha bugi wanashindwa kurudi nyuma na hali inazidi kuwa mbaya wanachemka kila kukicha
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  Albedo umeuliza swali zuri sana mkuu! kula tano!

  Kuna sababu nyingi sana zilizochangia, kwa mfano ninapowaona wanafunzi wa sekondari DSM na adha za usafiri aibu tupu! lakini major problems are

  1. Lack of moral kwa walimu
  2. ukosefu wa walimu
  3. ukosefu wa vitabu/vifaa
  5. system ya elimu yetu (XXXXXXXXXXXX)
  6. Umaskini wa wazazi
  7. Relying on past papers and tuitions
  8. etc

  xxxxxxxxxxx

  system ya elimu yetu ni mbovu, kwa mfano kitendo chako tu cha kusema wamefaulu hwa na wamefeli hawa then is questionable, wamefeli kwenye nini, miaka miine wamesoma nini, je kwa miaka minne mwanafunzi anafeli?? LENGO AU MPANGO wa taifa ni kumuandaa form four ili aweze kufanya nini?? swali hili kama halina jibu basi lolote linalodiskasiwa kuhusu elimu in Tz is a wastage of time!!! four years mt anapata zero?? .... hawezi kufanya lolote lile? hilo lolote lile kalipata hapo shuleni? why do we think evlauating students in one week is enough to grade them??

  kusoma kwa vyeti kumeleta wizi wa mitihani kuwaza fake PhDs, n.k

  Nini cha kufanya!

  1. Kwanza uzalendo wa wananchi uongezwe, uzalendo huu utatupa wajibu wa kila mmoja wetu kuwahusia na kuwapa moyo watoto wa kusoma. Sometime they just need inspiration and good stories!!! bila wao kujua wanasoma ili iwe nini thne we have problems!

  2. Kuongeza facilities

  Hili nalo linarudi juu, kumekuwa na lawama za KIJINGA na kuilamu serikali kwa kuanzisha shule za kata, ni lamwaza za kijinga kwani serikali inaonekana ina lengo zuri, ila imezidiwa....narudi point yangu ya kwanza...WATANZANIA NINAOWAFAHAMU WANA UWEZO WA KUTOA MIACHANGO KWENYE HARUSI NA VIPAIMARA, WANA UWEZO WA KUFANYA SHOPPING PALE MLIMANI CITY! WANA UWEZO WWA KUJIRUSHA CLUBS, NA KUNUNUA SIMU ZA MILION MOJA!!1 SAME WATANZANIA WHEN IT COMES TO THE ISSUES ZA KUSAIDIA TAIFA HASA MAMBO SENSITIVE KAMA HAYA IS A POINT WHERE WE POINT OUR FINGERS TO GOVERNMENT AND HIDE OUR SELFISHNESS IN OUR HEART!!

  KWA STANDARD YA MAISHA YA WALIONAZO NA JINSI FEDHA ZINAVYOTUMIKA VISIVYO , WE WILL BE MAKING AN HISTORICAL SHAME TO ACCUSE GOVERNMENT WHILE OUR PRIVATE LIFE IS CAPABLE TO REMEDY THE SITUATIONS!!!

  Nani msomi humu aliyesema afanya voluntering kuwapa moyo wanafunzi au hata kufundisha katika vijiji tunavyotoka?? HATUNA UZALENDO! na uzalendo ukiisha then that society must point fingers to others...tuliwaambia, tulisema........
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  • Si jambo la kujadili tu na kuliacha...nionavyo serikali itoe motisha kwa wadau wa elimu hususan waalimu tokea ngazi ya awali kwa kua mwanafunzi bora huzalishwa tokea mchakato wa awali wa elimu ya msingi!
  • Shule si majengo na Majina ya wanasiasa tu...kujenga majengo mazuri yaliyobuniwa na msanifu mahiri na kuyaita mathalan Albert Einstein hakumfanyi mwanafunzi anayesoma hapo kua Einstein, baada ya motisha kwa walimu/facilitators vifaa vya kufanikisha na kurahisisha elimu viwepo!
  • Tatu wanafunzi wenyewe watambue umuhimu wa elimu na madhara ya kutojali muda wa masomo vizuri. Hili linawezekana kwa wanazuoni kufanya makongamano 'shawishi' ya kuinspire kizazi kipya kutamani/kuiga mafanikio yaliyofikiwa na watu flani flani angalabu Madaktari wa falsafa,Profesa, wahandisi,Wasanifu(Architects),Oditors,Wanasheria, Neurologist na wengine wengi kwa fani zao!
  • Nne serikali ichunguze(nadhani inajua) kwanini shule binafsi na za mashirika ya dini zinafanya vyema kulinganisha na shule za serikali,baada ya kubaini waboreshe upande wao jahazi lisogee!
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Division four na zero 89% ni huenda ni mpango maalum wa CCM kuhakikisha kuwa nchi inapunguza idadi ya wasomi wa elimu ya juu kwani ni hatari sana kwa uhai wa CCM, ni mawazo na mtazamo wangu. Hasa ukizingatia Kauli ya aliyekuwa waziri wa habari Seif Khatibu aliyotumwa kutamka kama msemaji wa serikali kuwa kuwa na watu wengi waliograduates ni hatari kwa ustawi wa nchi(CCM). Huenda huu ni mpango mahsusi wa utekelezaji. But we have to wait and see form six results as well.
   
 6. D

  DENYO JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi ninaona ccm wameshindwa kuongoza kwa sera makini -huwezi kuwa na sera ya kujenga majengo harafu unachanja mbuga, mimi ningeomba mwandishi wa habari afanye uchunguzi watoto wa mawaziri wanasoma wapi-shule zipi, makatibu wakuu na makamishina mbalimbali-huuu ni unyanyasaji na ukandamizaji. Ccm inafika mwisho na sera zao sasa ili uone hali inavyokuwa mbaya zaidi sasa wanageukia majengo ya zahanati hata kama hawajamaliza hizi kata. Suluhisho ccm iachie ngazi
   
 7. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ikazaniwe sana wajue wanachofundisha wengi walimu ni kusubiri mshahara wao huo mdogo na kwenda makwao
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  I wish this thread was about chadema!!! we are exposing ourself!
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Nashauri thread hii iwe Sticky.......jamani hili sio jambo la mzaha.....kwa mara ya kwanza nimesikitika sana na mustakbari wa nchi yetu.

  ....Wazee dunia kijiji wageni wamejazana nchini wanachukua kila kitu chetu ajira mpaka kila kitu.........sio serikali kwa jambo kama hili wajumbe wa JF ni sisi wote tuliangalie kwa makini jambo hili.....wajumbe tufanyeje?
   
 10. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Sekta ya Elimu ina Wadau Mbali Mbali ambao kila mmoja ana majukumu yake katika Kulisogeza Mbele Gurudumu hili la Elimu. Kwa Mtazamo wangu ili tuweze ku address hili suala ni Lazima tuwaangalie hawa Wadau na kujaribu kuangalia majukumu ya kila mmoja na kama je anayatimiza kweli ama la. Wadau wa Elimu ni

  1: Mwanafunzi: Jukumu kubwa la Mwanafunzi ni Kusoma kwa Bidii

  2: Mwalimu: Kazi ya Mwali ni Kuhakikisha kwamba anahamisha knowledge yake kwa Mwanafunzi, kuhakikisha kwamba anaandaa Masomo kwa Mujibu wa Mtaala ambao Umetungwa na Serikali

  3: Mzazi: Mzazi naye ana wajibu wa kuhakikisha kwamba Mwanae anafuatilia Masomo nan i Jukumu la Mzazi kufuatilia Mwenedo wa Mtoto wake academically, Si Wazazi wengi wenye tabia hata ya kuulizia Ripoti za watoto wao za Masomo

  4: Serikali: Jukumu la Serikali ni Kutengeneza Sera ya Elimu ambayo itatengeza Mfumo wa Elimu katika Jamii Husika, vile vile kuhakikisha Majengo yanayojengwa yanakuwa Shule kwa maana kuhakikisha kwamba Inaajiri Walimu Competent, Inahakikisha Shule zote zinakuwa na Vitendea kazi ikiwa ni pamoja na Vifaa vya kufundishia, Vitabu vya Kutosha, Madawati nk. Vile vile Serikali inapaswa kuhakikisha Kwamba Walimu wanapata Mazingira Ya kufundishia ikiwa ni Pamoja na Kuwalipa vizuri ili waweze kumudu Maisha yao, hii itafanya Walimu wawe na Moyo wa Kufundisha.


  Sasa ni Wakati wa Serikali kujuiza katika haya:

  1: Mfumo wa Elimu: Kutengeneza Mfumo utakaowezesha hata wale wanaoshia kidato cha nne kutokuwa wamepoteza muda wao wa miaka mine, Je katika hili Serikali imefanikiwa kwa Kiasi Gani? Hivi Serikali imeshawahi kujuiliza kila Mwaka inazalisha Vyangudoa/Wapiga debe wasomi (Div four and Zero)) wangapi?

  2: Maslahi ya Walimu: Walimu wamekuwa wakilalamikia Mazingira Magumu ya Kufanyia Kazi, Mishahara Midogo inayowafanya Walimu kuwa ni Watu wanaoota kuondoka katika Sekta hiyo badala ya Kujikita. Je Serikali ni kwa Kiwango Gani imekaa na Walimu na kujaribu kutatua Matatizo yao? Au ndio kuambulia Maneno ya Kejeli kutoka kwa Mawaziri kama Hawa Ghasia? Je Kauli za Serikali kupitia Mawaziri kama Ghasia hazichangia katika Matokeo Mabaya ya Mwaka huu?

  3: Failures Kuwa Walimu: Sekta ya Elimu imekuwa ni Sekta Kimbilio kwa wanafunzi ambao ni Faulures( Sijawahi kusikia Mwanafunzi aliyepata Div One akiwaza kuwa Mwalimu), Je Kweli Tutegemee nini kwa Failures kufundisha watoto wetu? Je Serikali imefanya Juhudi gani kuwavutia Wanafunzi waliofaulu Vizuri kuingia katika Sekta ya Elimu (kwa maana ya kuwa Walimu?)

  4. Usawa katika Mfumo wa Elimu. Pamoja na Kwamba Mwisho wa Siku wanafunzi wote wanafanya Mtihani aina moja ( Yaani Mwanafunzi wa Shule ya Bondeni au Mbuyuni anafanya Mtihani ule ule anaofanya Mwanaffunzi wa Ilboru au Mzumbe au Kibaha, nimetaja shule za Serikali tu kwa Makusudi) Lakini Fersa katika Kuipata hiyo Elimu hazilingani hata kigogo, Walimu wengi wamekuwa wakikimbilia Mjini kwa sababu ya Urahisi wa kupata huduma mbali mbali za Kijamii kama Shule ( Kwa ajili ya watoto wao). Hili linapelekea Shule za Mijini kuwa na Walimu wengi kuliko Masomo wakati zile za Vijijini zikiwa na Mwalimu Mkuu peke yake. Je Serikali inangoja nini kutoa Motisha kwa Walimu wanaokubali kwenda katika Maeneo yenye Mazingira Magumu ya Kuishi?

  Kuna Mambo mengi Serikali inayoweza kuyafanya kwa Kushirikiana na Wadau mbali mbali ili kuinua hii Sekta Muhimi
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Divisheni One + Two + Three = 9.98%

  Divisheni ( Four + Zero) =
  90.1%


  Na Bado tunajisifu kiwango cha kufaulu kimepanda, Kweli prof Watson Alikuwa sahihi juu ya hii Ngozi
   
 12. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280

  maskini tz, naomba kuuliza swali la kizushi, tu, hivi shule za A-level za serikali zina uwezo wa kuchukua wanafunzi wangapi?
   
 13. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mungu wangu nkinki womi!!!i??
   
 14. T

  Tanzanian Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni kweli kabisa kuwa tumekosa uzalendo, ndiyo serikali ina sehemu yake ya kufanya, lakini kwa upande mwingine sisi nasi tuna sehemu ya kufanya ili kufanikisha hili na kuona tanzania yetu inakuwa mahali pazuri katika elimu na masuala mengine. Nimependa sana comments zako.
   
 15. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Nini kifanyike.
  Elimu ya msingi
  1.Kuangalia kwa upya ufundishaji wa shule za msingi. Hii ni kwa sababu wanafunzi wengi wanaofaulu kwenda shule za sekondari uwezo wap wa kusoma na kuadika n mdogo sana sana

  2. Kubadilisha mfumo wa mitihani ya shule za msingi. Hii ni kwa sababu mitihani hiyo, haijengi uelewa wowote kwa mwanafunzim na haimuandai yeye kuweza kukabiliana na mfumo wa elimu ya sekondari anaouendea. Pia mithani hii ina encourage cheating, inasababisha wanafunzi kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na kuwa na dull brain, pia guess working. Maswali yawe ya udadisi, kujieleza, kumfanya mwanafunzi kufikiri sambamba na mitaala

  3. Kuwabana maafisa elimu wilaya, maana wengi ndio hushirikiana na walimu wakuu katika kuwaonyesha watoto mitihani ili kupata sifa za wilaya zao kufaulisha. So hawa, pamoja na walimu wakuu, na wasimamizi wa mitihani watungiwe sheria kali sana, ili pale wanapobainika kufanya hivyo. Na kuwe na ufuatiliaji wa kina.

  4. Kuboresha mazingira ya shule za msingi, kwa maana ya vifaa vya kufundishia, walimu bora, na maslahi mazuri ya walimu hasa mishahara.

  5. Kila mtu kutimiza ajibu wake katika kumwezesha mwanafunzi kusoma vizuri na kupata elimu bora, mwanafunzi mwenyewe kwa nafasi yake, mwalimu, jamii na serikaki.

  Elimu ya sekondari
  1. serikali kuhakikisha inarecruit na kuajiri walimu wa sekondari walio bora, na waliofaulu. Hii ni kumaanisha kuwa ifkie wakati serikali iweke mazingira ya kuweza kwashawishi six leavers waliofulu vizuri kuingia katika profession ya ualimu ili kuproduce walimu bora wa sekondari.

  2. Kuondoa mentality serikali iliyoijenga kuwa elimu ni majengo au kujenga shule nyingi. Strategic plan endelevu inatakiwa kufanywa na serikali, na kuangalia vipaumbele vya elimu vitakavyoleta tija katika elimu yetu. I meam majengo yaende sambamba na furniture, vitabu, maabara na walimu wenyewe. Shule ni nyingi na hazina walimu kabbisaa, au mmoja au waili. Sasa matokeo mazuri yatatoka wapi. Majengo tu hayatoshi kuleta elimu bora na kupandisha kiwango cha ufaulu, so kipaumbele cha selikali kiwe na shule zilizo na full package in quality and quantitiy.

  3. Kuboresha maslah ya walimu kama, mishahara, myumba, posho za mazingira magumu ya kufundishia, teaching allowances. Hapo walimu watalala darasani.

  4. Kuwahusisha kikamilifu wadau wa elimu, hasa walimu pale mabadiliko yoyote ya elimu hasa syllabuses, curriculum n.k

  5. Sekta ya elimu imekuwa na waajiri wengi, au inashughulikiwa na idara nyingi (TSD, CWT, Wizara ya elimu, Tume ya utumishi wa Umma, na Sasa TAMISEMI, na Wakurugenzi wa halmashauri) inayomfanya mwalimu abake kutanga tanga bila kuzijua haki zake na pia akizijua wapi akaanzie kuzidai, hii inavunja sana morale ya walimu. Ifikie wakati kuwe na mwajiri mmoja tu anayeshughulikia ajira na maslah ya walimu, ili kurahisisha mahusiano na mawasiliano kati ya walimu na mwajiri wao.

  6. Kuhakikisha mtihani wa kidato cha pili inafanywa na kusimaniwa kikamilifu, kuweza kupata wanafunzi wenye uwezo wa kuendelea na elimu ya sekondari.

  7. Kupanua wigo wa vocational education, kwa kujenga well equiped shule na vyuo vya ufundi ili kuwawezesha wale walioshidwa kuendele na elimu ya sekondari na kidato cha tatu basi waingie kwenye vocational sector, na kuweza kujiajili.

  8. Walimu kuchukua wajibu wao wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

  Kwa ujumla
  1. Accounability and commitment to educational leanders especially in minisrty.
  2. Good educational policy ambazo zitafuatiliwa kikamilifu
  3. Adhabu kali kwa wote watakaoshindwa kutimiza wajibu wao.

  NAWAKILISHA
   
 16. N

  Ninliy Senior Member

  #16
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cha kufanyika kikubwa hasa kwanza serikali nzimaaa ijiuzulu baadae ndo yatakuja mengine ya kubadili mfumo wa elimu.
   
Loading...