Msaada Namna Ya Kufanya Application South Africa

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,146
Reaction score
7,685
Habarini...!!! Nimeona kwa Nchi za Afrika ,South Afrika ndio nimeona nchi yenye Gharama nafuu kwa sisi watanzania kusoma kule..kama Nitakuwa nakosea naomba mnitajie nchi nyingine tofauti na Tanzania!

Sasa nategemea kuanzia March 2017 kuanza kufanya application za kuomba kusoma Bsc.OF ULTRASOUND katika vyuo vilivyoko SOUTH Afrika! Toka sasa ni kama Nina miezi miwili ya kujiandaa!

Tatizo ni kuwa sijawahi Fanya applications za vyuo nje ya Tanzania hasa South Afrika ndio maana nimekuja hapa kuwauliza walionitangulia na wale wajuzi wa Mambo kuomba msaada wenu, wa kiushauri,kimawazo hata kimatendo ili nifanikishe Lengo langu!

Kati ya vitu vinavyo nitatiza ni pamoja na

1.Sisi kwa huku Tanzania Diploma tunamaliza mwezi wa 8/2017 wakati huo kwa vyuo vya South Afrika application zinaanza Mwezi wa 3 na mwisho mwezi wa 9! Je hapo maombi nitafanyaje ukiwa sina Certificate? Je naweza tumia Matokeo ya kunzia Semister 1 hadi 5? Bila ya ile semester 6?

2.Mimi nikiwa na Diploma in Diagnostic Radiography ya hapa bongo naweza Soma hiyo BSC of ultrasound South Afrika kwa Miaka mingapi?

3.Kuna sehemu wanasema sijui F1-Visa ila sijui ni nini?

Kiujumla Naomba muongozo kabisa wa kufanya Application Nchini South Afrika au nchi nyinge yenye Gharama nafuu!! Kwa kozi hiyo! Ila has a South Afrika....kwa walioko huko au waliopeleka Ndugu zao huko naombeni msaada ili nijiandae mapemaaa kabisaa

Pls msaada Tafadhari!!! Ili nifanikishe
 
Kwa wanao fahamu tafadhari

Application yoyote ya chuo, huwa unaidentify chuo Mfano University of Pretoria, fungua web yao utaona prospective students, bonyesha hapo, utaona sehemu ya application then apply, ila yapasa upitie taarifa za chuo ili upate kuona course unayotaka kuomba kusoma
 
mdogo wangu DANYA! unataka kusoma chuo gani pale RSA?
Umeshaona hiyo kozi unayohitaji?Una uwezo wa kifedha (Ada & matumizi ya kila siku?) maana kule bodi ya mikopo haihusiki. Kama ndio basi ingia kwenye website yao na anza ku-apply.
 
Thanks mkuu shida ni kuwa Mimi Nina apply kma international student sasa matokeo nayafanyaje yawe sawa na ya kule au natuma kama yalivyo
 
Ndio mkuu nimezingatia naona sisi wa kutoka Tz tunalipa Ada sawa na wao lakini kwenye qualifications ndo panapo nipa ugumu
 
Cheki Makerere university.
Imetulia sana!
 
Thanks mkuu shida ni kuwa Mimi Nina apply kma international student sasa matokeo nayafanyaje yawe sawa na ya kule au natuma kama yalivyo

Tuma matokeo kama yalivyo wao ndio watakujudge wewe kutokana na qualities zao. Watafanya equivalent
 
Danya, nitumie matokeo yako kwenye andreakalima@gmail.com. Mimi naweza kukusaidia kwa vyuo vya Kenya, unipe course preferences zako (tatu). Nitatumia gharama zangu kisha nitakuja kukudai nitaenda kenya mwezi huu kabla ya Xmass.
 
Mkuu this is 21st century... Mpaka unapanga kusoma huko that means umefanya research ya chuo gani unataka kwenda! Either ulikiskia then ukagoogle details maana kila chuo kina website yao na full details Zake jinsi ya kujiunga for both local and foreign students!!!!! Tena hadi student visa wanakusaidia jinsi ya kupata. Hayo mambo ya kutuma mtu sijui akusaidie kuapply ya kizamani sana nowadays kila kitu Kiganjani mwako within 5 minutes unaaply kilichobaki kusubiri majibu!
Kaa chini ujipange upya sio kukurupuka hujui hata unataka kwenda chuo gani
 
the best way ya kupata chuo SA nikufunga safari hadi chuo husika ukiwa na vyeti vyako original ukifika application utaifanyia hapo hapo chuoni then rudi bongo kusikilizia selection fanya booking mapema ya fastjet
 
Thanks mkuu nitakutumia kwenye hiyo Email lakini Kenya kusoma si ni gharama sana ukiringanisha Na south? Kama nakosea naomba nirekebishe
 
Mkuu this is 21st century... Mpaka unapanga kusoma huko that means umefanya research ya chuo gani unataka kwenda! Either ulikiskia then ukagoogle details maana kila chuo kina website yao na full details Zake jinsi ya kujiunga for both local and foreign students!!!!! Tena hadi student visa wanakusaidia jinsi ya kupata. Hayo mambo ya kutuma mtu sijui akusaidie kuapply ya kizamani sana nowadays kila kitu Kiganjani mwako within 5 minutes unaaply kilichobaki kusubiri majibu!
Kaa chini ujipange upya sio kukurupuka hujui hata unataka kwenda chuo gani
Unanigombeza bure tuu mkuu! Umeelewa nilicho andika? Sijaomba mtu anifanyie Application pia nimesema mm ni mgeni na hivyo nimeomba kueleweshwa kuhusu Namna ya kutumia Matokeo yetu ya kitanzania kufanyanyia application south ikiwa mihula tunapishana! Sijaomba mtu anifanyie application,nimeomba msaada wa kuelekezwa kwa wanao jua kama unajua nielekeze kama hujui basi! Lakini sio kunigombeza
 
the best way ya kupata chuo SA nikufunga safari hadi chuo husika ukiwa na vyeti vyako original ukifika application utaifanyia hapo hapo chuoni then rudi bongo kusikilizia selection fanya booking mapema ya fastjet
Kupitia mtandao inasumbua au?
 
Back
Top Bottom