Wanajamvi,
Kwa wale wenye utaalamu na haya makufuli yetu ya siku hizi kama vile Wohu, Solex, Solit na mengineyo ninaomba tusaidiane ushauri wa uzoefu hapa.
Mimi nimekuwa nikiyatumia sana kwenye biashara yangu, kibandani kwangu, lakini hivi karibuni nimekutana na matukio ya kupoteza vitu mule ndani bila kuvunjiwa. Na si mara moja wala mbili, jambo hilo hujirudia.
Hata nikaamua kuwa nanunua kufuli mpya mara kwa mara, tena naenda kununulia mbali ambapo hakuna anaenifahamu na kisha naficha sana funguo zangu lakini bado hali imekuwa inatokea.
Je, najiuliza, ni mtu ana funguo malaya? Je hizi kufuli si zinasemekana funguo zake zimetengenezwa vile huku na huku ili kuzuia funguo malaya?
Je, ni mtu anatumia ndumba ya kufungua kufuli na kuingia ndani kisha kufunga na kutoka zake. Maana saa nyingine nakosa amani kabisa na huyu mtu anayefanya haya.
Tusaidiane ufumbuzi tafadhali.