Msaada: Naibiwa mali yangu katika mazingira ya kutatanisha

Msaada: Naibiwa mali yangu katika mazingira ya kutatanisha

Rellik

Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
60
Reaction score
59
Wanajamvi,

Kwa wale wenye utaalamu na haya makufuli yetu ya siku hizi kama vile Wohu, Solex, Solit na mengineyo ninaomba tusaidiane ushauri wa uzoefu hapa.

Mimi nimekuwa nikiyatumia sana kwenye biashara yangu, kibandani kwangu, lakini hivi karibuni nimekutana na matukio ya kupoteza vitu mule ndani bila kuvunjiwa. Na si mara moja wala mbili, jambo hilo hujirudia.

Hata nikaamua kuwa nanunua kufuli mpya mara kwa mara, tena naenda kununulia mbali ambapo hakuna anaenifahamu na kisha naficha sana funguo zangu lakini bado hali imekuwa inatokea.

Je, najiuliza, ni mtu ana funguo malaya? Je hizi kufuli si zinasemekana funguo zake zimetengenezwa vile huku na huku ili kuzuia funguo malaya?

Je, ni mtu anatumia ndumba ya kufungua kufuli na kuingia ndani kisha kufunga na kutoka zake. Maana saa nyingine nakosa amani kabisa na huyu mtu anayefanya haya.

Tusaidiane ufumbuzi tafadhali.
 
Tafadhali tafuta zile funguo za Mult lock zile ndo kiboko yao,nafikiri wanaofisi zao maeneo ya mikocheni nadhani
 
Huenda labda kuna mtu ana master key...jaribu siku moja kutega mtego umjue mbaya wako ni nani anayekufanyia hujuma kwenye biashara yako...Pole sana mkuu
 
Cha kufanya funga camera ndani( hidden), atakayeingia utamwona na itakusaidia kujua nani mwizi wako.
 
Lala humo kwenye kibanda siku 10 mfululizo...
 
Huenda labda kuna mtu ana master key...jaribu siku moja kutega mtego umjue mbaya wako ni nani anayekufanyia hujuma kwenye biashara yako...Pole sana mkuu
Sawasawa mkuu, Asante sana mkuu,
 
Sumbawanga kuna radi mkuu kachukuwe kule ni buku tuuu
Kweli mkuu, ndio maana watanzania hata tusome vipi imani za mababu zetu hatutoziacha kwa sababu tuna roho za kwann, sasa watu kama hawa ndio wanatufanya tuwalipue kwa nuclear bomb za asili bure,japo tusingependa kutumia hayo maswala,
 
Naona wachawi wameanza kuchukua vitu madukani kabisa.

Soon watahamia kwenye Mabenki.

Ni mwendo wa kuzihesabu namba tu
 
Mkuu acha huo mlango wazi usiufunge,tafuta damu na manyoya weka hapo mlangoni...wakija wataacha wenyewe kwa huo mkwara
 
Back
Top Bottom