Msaada: Naibiwa mali yangu katika mazingira ya kutatanisha

Mkuu acha huo mlango wazi usiufunge,tafuta damu na manyoya weka hapo mlangoni...wakija wataacha wenyewe kwa huo mkwara
Na ajiandae kupoteza wateja pia. Maana kuna wengine tukiona hivyo hatusogei hata kama unauza makinikia kwa bei ya kutupwa
 
Mkuu paa lako umelikagua linakuhakikishia usalama? Isije kuwa wahuni wanapitia juu na kukuachia makufuli yako bila kuyagusa.
Vinginevyo.....kama si master key basi ndumba inahusika.POLE SANA MKUU. Siku hizi huruma watu wamezika
 
Hiyo master key inafanyeje kazi? Unaweza ukatupia kapicha?
 
Wanajamvi,

Kwa wale wenye utaalamu na haya makufuli yetu ya siku hizi kama vile Wohu, Solex, Solit na mengineyo ninaomba tusaidiane ushauri wa uzoefu hapa.

Mimi nimekuwa nikiyatumia sana kwenye biashara yangu, kibandani kwangu, lakini hivi karibuni nimekutana na matukio ya kupoteza vitu mule ndani bila kuvunjiwa. Na si mara moja wala mbili, jambo hilo hujirudia.

Hata nikaamua kuwa nanunua kufuli mpya mara kwa mara, tena naenda kununulia mbali ambapo hakuna anaenifahamu na kisha naficha sana funguo zangu lakini bado hali imekuwa inatokea.

Je, najiuliza, ni mtu ana funguo malaya? Je hizi kufuli si zinasemekana funguo zake zimetengenezwa vile huku na huku ili kuzuia funguo malaya?

Je, ni mtu anatumia ndumba ya kufungua kufuli na kuingia ndani kisha kufunga na kutoka zake. Maana saa nyingine nakosa amani kabisa na huyu mtu anayefanya haya.

Tusaidiane ufumbuzi tafadhali.
Yawezekana tatizo sio kufuli labda unachezewa mchezo mida ya kazi usimwamini kiumbe mwanadamu yeyote binafsi yalishawahi kunikuta mbinu iliyokuwa inatumika sikuamini ni story ndefu Fanya uchunguzi tu utabaini tatizo
 
Mkuu paa lako umelikagua linakuhakikishia usalama? Isije kuwa wahuni wanapitia juu na kukuachia makufuli yako bila kuyagusa.
Vinginevyo.....kama si master key basi ndumba inahusika.POLE SANA MKUU. Siku hizi huruma watu wamezika
Namimi nimewaza hivyo hivyo, huenda kuna sehemu washikaji wanapitia kiulaini wala siyo mlangoni. Jaribu kucheki kwa umakini mkubwa. Angalia pia mizigo unayonunua kama ni kwenye mabox makubwa huenda jamaa wanakuja na mwizi kwenye box unamfungia then anaiba weeee baadae anatoka.
 
Back
Top Bottom