Msaada, nahitaji tiba ya meno

Sukari Yenu

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
1,698
1,253
Wakuu habari za weekend,

Shida yangu kubwa ni meno yangu mawili ya mbele, meno ya tabasamu. Meno haya yameinuka kidogo kiasi ambacho yamezidi ule usawa wa meno ya chini. Yametengeza kitu kinachoitwa overbite. Jino moja la upande wa kulia limeanza kuinuka kabisa linatoka nje ya mstari. Kwa madaktari wa meno wanaita PROTRUDING TOOTH ambalo kimsingi tayari lishatengeneza overjet. Kimsingi tatizo hili linarekebishika. Tazama picha chini kwa ufafanuzi zaidi. (Picha si yangu)

Nimefuatilia mtandaoni aina hii ya tatizo nimegundua moja ya vyanzo vya tatizo hili ni genes unarithi kwa wazazi. Nikiri kuwa baba yangu alikua na meno yamezidi kidogo kwa mbele na baada ya muda mrefu jino moja liliinuka kabisa mpaka likawa kama linatoka nje. Akaenda kuling'oa kabisa.

Kinga ni bora kuliko tiba. Kwa sababu tatizo limeshajulikana nahitaji nirekebishe hii kasoro kabla maji hayazidi unga. Msaada ninaohitaji ni:

1. Hospitali nzuri yenye wataalamu watakodeal na tatizo hili kwa ukamilifu, kwa sasa nipo DSM.

2. Kama kuna njia za tiba naomba mnishauri best option among the available alternatives.
na wa kuugua ugua na huwa sifuatilii sana namna hii bima inavyofanya kazi. Najua tu nalipa katika mshahara wangu.

4. Iwapo bima haiingii hapo basi naomba estimates za gharama za matibabu mambo yakae sawa.
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    8.5 KB · Views: 6
Bima unatumia mbona vizuri sana ila nenda private hospital kubwa kama aghakan, n.k ukienda ndogo watakwambia ulipie kwa sbb bima inatoa malipo ya package kulingana na level ya hospital
 
Bima unatumia mbona vizuri sana ila nenda private hospital kubwa kama aghakan, n.k ukienda ndogo watakwambia ulipie kwa sbb bima inatoa malipo ya package kulingana na level ya hospital
Okay....asante sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom