Msaada, nahitaji kujua lugha ya mume wangu

Msaada, nahitaji kujua lugha ya mume wangu

prax

Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
27
Reaction score
8
Habari zenu jamani, mimi ni mwanamke mwenye watoto 3 na mume wa ndoa! ndoa yetu namshukuru Mungu anatusaidia tunaishi vizuri kwa maelewano.

Shida yangu ni kuwa mume wangu ni kabila tofauti na mimi, sasa yeye anapenda kweli kuongea kilugha na ndugu zake either kwa simu au hata wakija nyumbani kutusalimia!

Yeye haoni kama ni shida na nalielewa hilo,tatizo ni kwamba wakati mwingine natamani kusikia wanachokiongea ila ndo hivyo nashindwa.Kumuambia nahisi kama namnyima raha.

Ninachoomba ni msaada wa jinsi ya kumuapproach kumweleza natamani na mimi nichangie katika maongezi bila yeye kufikiri vibaya maana ni mtu anapenda kuongea sana kikwao yani.
 
Wekeni house rules, ni primitive languages.

Wageni wakija watumie kiswahili.

Ukishindwa siku akiwa anaongea nao ondoka eneo la tukio
 
Habari zenu jamani,mimi ni mwanamke mwenye watoto 3 na mume wa ndoa!ndoa yetu namshukuru Mungu anatusaidia tunaishi vizuri kwa maelewano!
Shida yangu ni kuwa mume wangu ni kabila tofauti na mimi,sasa yeye anapenda kweli kuongea kilugha na ndugu zake either kwa simu au hata wakija nyumbani kutusalimia!yeye haoni kama ni shida na nalielewa hilo,tatizo ni kwamba wakati mwingine natamani kusikia wanachokiongea ila ndo hivyo nashindwa.Kumuambia nahisi kama namnyima raha.
Ninachoomba ni msaada wa jinsi ya kumuapproach kumweleza natamani na mimi nichangie katika maongezi bila yeye kufikiri vibaya maana ni mtu anapenda kuongea sana kikwao yani.

Jifunze hiyo lugha yao. Moja utajua wanaongea nini na pili kujifunza lugha yoyote ni kupanua upeo wa mtu.
 
Women!!!!! Wonders will never cease!
Muachie na uhuru na ndugu zake jamani! Mume umemkwapua kutoka kwa watu waliom'beba, akaanza kukua wakamtahiri, wakamsomesha. Umemkuta juzi hapa unataka ummiliki hadi lugha ya kwao? Muache aongee ili na wewe ujifunze lugha ya ukweni na wanao pia.

ila wanaume mna kazi! Mweeeh!
 
Umbea tu!
Hapo ushahis wanakusema!
Jamani kuolewa na kuoa hakutufanyi tukawa sio sisi!
Khaaaaaaa!
Tunabaki kuwa tuliolelewa na kuzaliwa na kukua kwenye taasisi fulani!
Pika karanga za mayai na juice ya embe mbichi wapelekee ili kilugha kipande vizur!
We kajikunjie kanga zako kabatini,usisahau kutenganisha za msibani na za kuogea.lol!
 
Women!!!!! Wonders will never cease!
Muachie na uhuru na ndugu zake jamani! Mume umemkwapua kutoka kwa watu waliom'beba, akaanza kukua wakamtahiri, wakamsomesha. Umemkuta juzi hapa unataka ummiliki hadi lugha ya kwao? Muache aongee ili na wewe ujifunze lugha ya ukweni na wanao pia.

ila wanaume mna kazi! Mweeeh!

Af unifundishe kichaga,nahs kabisa mangi akitembelewa na kina miss chagga Nicas Mtei, Mkirua , Asprin na Kaizer wananichakachua!
Haki vile!
 
Last edited by a moderator:
Mmmhhhh unahisi kusemwa.....huyo mume ni kabila gani na wewe kabila gani??ukitaja kabila itakuwa rahis kushaur maana kuna makabila wakiwa hata ofisin ni lugha ya kwao
 
Women!!!!! Wonders will never cease!
Muachie na uhuru na ndugu zake jamani! Mume umemkwapua kutoka kwa watu waliom'beba, akaanza kukua wakamtahiri, wakamsomesha. Umemkuta juzi hapa unataka ummiliki hadi lugha ya kwao? Muache aongee ili na wewe ujifunze lugha ya ukweni na wanao pia.

ila wanaume mna kazi! Mweeeh!
prax chukua maneno haya yatakusaidia!
 
Last edited by a moderator:
Mama yangu anaongea kiufasaha lugha ya kabila la Baba na cha ajabu hajawahi kukaa zaidi ya mwezi home town kwetu.

Ndugu wa kiumeni wakija wanachapa naye kilugha tu na wengine hawajui kama yeye ni kabila tofauti maana anaongea kile kilugha cha ndani kabisa, kwa kijana wa leo mpaka uwe na dictionary ya kilugha ndio utamuelewa sentensi nyingine.
 
Women!!!!! Wonders will never cease!
Muachie na uhuru na ndugu zake jamani! Mume umemkwapua kutoka kwa watu waliom'beba, akaanza kukua wakamtahiri, wakamsomesha. Umemkuta juzi hapa unataka ummiliki hadi lugha ya kwao? Muache aongee ili na wewe ujifunze lugha ya ukweni na wanao pia.

ila wanaume mna kazi! Mweeeh!
Hapo ndipo huwa nakupendea! Yaani unatabasamu kweli nikiwa nagonga kikwetu pindi wageni wanapotutembelea kwenye familia yetu! Ama kweli NIMEPATA MKE, LOL! Wanune, walie, shauri yao!
 
kaz kwel kwel,jifunze lugha yake,kama mama yangu watu hufikiri ni kabila moja na baba yangu kwa jinsi anavyoongea hicho kilugha,hata sisi hatuoni ndani
 
Kwa kweli hyo hali inakera pole mwaya manake wakija wageni wa upande wake inabidi uwapishe mana huna cha kuongea zaidi ya salam, mm hata rafiki anaependa kuongea lugha ya kwao muda wote huwa ananikera
 
Hapo ndipo huwa nakupendea! Yaani unatabasamu kweli nikiwa nagonga kikwetu pindi wageni wanapotutembelea kwenye familia yetu! Ama kweli NIMEPATA MKE, LOL! Wanune, walie, shauri yao!

Wewe umejiunga lini hapa JF? unamjuwa Paw? subiri ban za ajabu zianze kukutembelea ndio utajuwa kwa nini Vicky Kamata aliachwa peke yake kanisani.
 
Last edited by a moderator:
Ooh Sorry sijaweka ushauri, nazani
Mweleze tu kwamba azingatie uwepo wako kwahyo awe anaongea kiswahili atleast wageni wanapokuwepo ili na ww uweze kujumuika kimaongezi, wengine wanakwambia ujifunze hyo lugha jamani sio rahis mwingine lugha ya kwao tu bado ni tatizo kuielewa sembuse lugha ya mwenzio
 
Haaa hivi hujajua tu

Ngoja nianze darsa..."usengwile"...taja maana kabla hujaenda kwen baraza la Idd!

Tatizo huwa mnaongea kichina sijui kikorea kile!
Af mjue sio kibantu kile,sarufi yake na matamshi yako kivyake!
Siambui hata moja!
Najionea sawa tu!
Ongeeeeeeeni weeeeeeeh mkimaliza atakuja kuongea kiyunani parkushonare!baaas.
 
Back
Top Bottom