Msaada: Nahitaji huduma ya internet

Jokia

Member
Feb 18, 2015
93
178
Wakuu salama humu?

Naombeni msaada katika hili. Mahali nilipo huduma ya internet kupitia mitandao ya simu haipatikani na ikitokea inasoma E kiasi kwamba siwezi fanya cha maana kwa kutumia mtandao.

Naomba kuuliza kama kuna uwezekano wa kuunganishiwa wireless internet ili niwe natumia wi-fi badala ya kuwasha data kwenye simu. Je, uwezekano upo na gharama itakuaje kwa mwezi au mwaka?

Asanteni.
 
Uwezekano upo, lakini kama matumizi yako ni binafsi (si ya kibiashara) kama tu kuwasilana na marafiki hutoweza kulipa installation na gharama za mwezi

VSAT solution: gharama ya installation ni sh 1,500,000
Gharama ya matumizi kwa mwezi sh 150,000

Ni rahisi kwako kwenda sehemu mobile network iko sawa, utumie mtandao ukiwa hapo
 
Wakuu salama humu?
Naombeni msaada katika hili. Mahali nilipo huduma ya internet kupitia mitandao ya simu haipatikani na ikitokea inasoma E kiasi kwamba siwezi fanya cha maana kwa kutumia mtandao
Naomba kuuliza kama kuna uwezekano wa kuunganishiwa wireless internet ili niwe natumia
wi-fi badala ya kuwasha data kwenye simu. Je, uwezekano upo na gharama itakuaje kwa mwezi au mwaka?
Asanteni.
Kama sehemu hakuna mobile data kuna uwezekano mkubwa provider wa wifi/fiber pia wasiwepo.

Kwa maeneo ya ndani ndani tumia satellite internet. Ila kama mdau hapo alivyosema ni ghali na speed si nzuri.

Pia jaribu mitandao tofauti tofauti hasa Voda, tigo na hAlotel

Jaribu pia manual network search kama utapata mtandao unautwa Tritel ama Una namba tu bila jina. Search ukiwa umeweka simu 3g only.
 
Niweke kambi maana mimi pia na shida hiyo vipi nikitumia hizi mifi za mitandao?
 
Onana na TTCl wana huduma ya VSAT isipokuwa jiandae kwa installation charges maana zimechangamka
 
Back
Top Bottom