Msaada: My Jamiiforums e-mail on outlook... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: My Jamiiforums e-mail on outlook...

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by LUSAJO L.M., Mar 24, 2009.

 1. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wakuu nawasalimu...

  Nimekuwa na jaribu kuweka e-mail address yangu ya jamiiforums kwenye outlook yangu ili iwe rahisi kwangu ku access mails akati naendelea na kazi nyengine bila ya mafanikio.

  nimejaribu kuifanyia setup automatically imeshindikana then nikajaribu kuifanyia kwa kutumia default settings za POP3 account za gmail napo bila ya mafanikio...

  Invisible and other mods....naomba mnisaidie kupata settings kama incoming mail server, outgoing server...ports ili niweze configure na kutumia mail hii... natumaini itawa na manufaa si kwangu tu bali kwa member wengi wa Jamii Forums...

  Nawakilisha,

  Lusajo.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Mar 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndugu swali lako unapoamua kuliweka hapa kwanza unakuwa unavunjia heshima structure nzima ya jamii forums haswa hao waliokupa hiyo email cha kwanza kufanya ni kuwasiliana nao kwanza kwa njia zenu ambazo mlipeana -- lakini kwa kuanza hapa naona umekosea heshima kama ingekuwa umekula kiapo basi umetapika -- kuna wahusika wa jambo hilo
   
 3. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Shy,

  Nashukuru kwa jibu lako zuri husiana na ombi langu ambalo kwa bahati mbaya ama kutokujua nililiwasilisha mahali pasipo husika. Pia naomba nichukue nafasi hii kuiomba radhi 'structure' nzima ya jamii forum kwa kuivunjia heshima kutoka na hili ombi langu na pia naomba radhi kwa wahusika wa jamii forum ambao walifanikisha mimi kupata email ya JF. Nna hakika ya kwamba ntakuwa nimewakwaza wengi sana.

  Naomba niseme ya kwamba nia na dhumuni langu la kuomba kupatiwa maelekezo hapa jamvini ni kwamba nilikuwa nikitegemea ya kwamba jibu ambalo ningepatiwa lingeweza kuwa msaada kwa wengine ambao huenda wana email za Jf lakini inawawia vigumu kuzitumia katika Outlook, sikufanya kwa nia mbaya na wala sikuwa nimedhamiria kuwavunjia heshima watu.

  Pili ntashukuru kama Shy utanisaidia structure nzima ya JF ili nweze kujua siku nyengine nikiwa na swali la aina gani natakiwa kulipeleka upande gani wa structure maana naona kwamba nimewakwaza sana kwe kupost hii kitu hapa ili kila mtu aone. Sintotaka kuwakosea heshima tena.

  Nawakilisha.

  PS: Shy nadhani wewe ndo umewavunjia heshima kina 'Structure' maana sidhani kama kwa kuuliza lile swali nilikuwa nimevunjia heshima mtu, naamini kuuliza si ujinga na ukiwa kama mtu mwenye utashi na ustaarabu nilitegemea kwamba ungejibu kwa kunielekeza nini kifanyike badala ya hiyo lugha ambayo uliamua kutumia. Ungeweza kuni PM na jibu lako hilo ningekuelewa tu... Ahsante kwa kunielimisha.
   
 4. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2009
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shy kutokuelewa kwa mtu anapouliza sio kuvunjia heshima,kwani si kila mtu anajua,kwani hii site ni kwa wajuzi wa mambo tu?wengi wetu ni mbumbumbu wa IT na kwa kutumia Jamii Forum tunajifunza mengi toka kwenu wajuzi wa mambo,au mnataka tuwaulize nini?kwa mpango huu wa kukatishana tamaa sidhani tutafika jamani.
  Lusajjo hajakosea na hastahili kuomba radhi!Lusajjo anaweza asijue IT lakini ni mjuzi wa mambo mengine,tusaidiane na sio vizuri kubezana!!
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  SHY angekuwa hakimu ningempangia kusikiliza kesi za Liyumba, Mramba, Yona na Mgonja.
  kaazi kweli kweli
   
 6. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu Kyelaboy, naungana na wewe kabisa kuhusiana na hili. Lusajjo hakustahili kuomba radhi eti kwa kuuliza ili afahamishwe asichokijua ili akijue. Si vyema kukatishana tamaa wenyewe kwa wenyewe!
   
 7. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,583
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Taratibu Shy, kuuliza si ujinga. Ungempa maelekezo tu na sio kusema amevunja heshima. kwenye JF kuna wadau wa proffesionals tofauti tofauti. Lusajjo anaweza kuwa ni Daktari na wewe Shy unaweza kuwa ni mtu wa IT. kwa kifupi tunategemea michango kama ilivyo kwa wana JF wengine.
   
 8. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #8
  Apr 10, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Dah,

  Maswali kama ya mkuu Lusajo kuyajibu hapa inachukua muda. Ni kwa sababu si kila topic tutaisoma.

  Mkuu Lusajo, kama hujapata ufumbuzi wa tatizo lako tafadhali wasiliana nami kwa njia unayoona ni mbadala ili nikusaidie.

  Email zote ni POP3 enabled na accounts zote ni zaidi ya 7GB storage.

  Pole na karibu
   
Loading...