Msaada mwenye connection ya ajira nchi za Kiarabu

pole sana. lakini kuwa makini, kuna mijitu inawapeleka watu kwa njia zisizo rasmi na matokeo yake unageuka mtumwa kule uarabuni. utateseka mpaka ujute kuwaza kwenda uarabuni. ninasisitiza, nenda kwa njia halali. usikubali ule mtindo wa kushikiwa passport. usiingie ule mkataba eti ulipiwe nauli na boss kule arabuni, kisha passport unashikiwa,ukitaka kuacha kazi ulipe nauli. usikubali haya ndugu. bora ufe kwa shida hapa bongo. tazama hizi clips kupata uzoefu. Mungu akujaalie

asante kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
hapo itakuwa ngumu kidogo kwa upande wangu wallah ningekuwa ninauwezo wa kuimiliki hiyo laki 6 nisingehangaika kutaka kwenda nje...ningeitumia hiyo hiyo kama mtaji
Una akili sana mdogo wangu. Wakupe kazi kwanza utawalipa ukianza kupata mshahara tena kidogo kidogo. Nje ya hapo ni utapeli tu. Laki sita ni hela ndefu sana kwa sisi watu wa hali ya chini.
 
Ma victim wa kutafuta kazi tupo wengi hapa Tz.me mwenyewe nasubiri wana walete mrejesho na mimi nianze mchakato wa kutafuta kibarua huko ugaibuni.
Maana kwa hapa tz life limekuwa hard conection hatuna kazi kupata ni mtihani yaani ni tabu tup.
kama kuna mtu anaweza nikopesha mtaji nifanye walau biashara maana hali ni ngumu jaman wandugu.
 
pole sana. lakini kuwa makini, kuna mijitu inawapeleka watu kwa njia zisizo rasmi na matokeo yake unageuka mtumwa kule uarabuni. utateseka mpaka ujute kuwaza kwenda uarabuni. ninasisitiza, nenda kwa njia halali. usikubali ule mtindo wa kushikiwa passport. usiingie ule mkataba eti ulipiwe nauli na boss kule arabuni, kisha passport unashikiwa,ukitaka kuacha kazi ulipe nauli. usikubali haya ndugu. bora ufe kwa shida hapa bongo. tazama hizi clips kupata uzoefu. Mungu akujaalie

Hii comment ni ya kuzingatia sana wakuu.
Maagent wengi ni matapeli na hawana utu.
Akishakupandisha ndege yeye anavuta mkwanja wake,lolote litakalokutokea hana huruma na wewe,anakuchekea tu wakati bado ukiwa bongo ili avute pesa.
Hakikisha hata kama utamtumia agent ila uwe na salio la kutosha kwenye akaunti yako ili ikitokea dharula yoyote uwe na uwezo wa kujinasua.
mfumo wa kazi za Asia ni tofauti sana na mfumo wa Africa na Ulaya,mfumo wao upo kibiashara zaidi hakuna mahaba.
Mimi mwenyewe nilikuwa mhanga katika hili,nikiwa na muda mzuri nitakuja kuwasimulia baadae.
 
Shukrani. Tupe uzoefu, vijana wanateseka sana na biashara hii. Uelewa na changamoto za maisha zinawafanya vijana kutaabika na pengine kupoteza maisha. Halafu serikali haifanyi juhudi za kutosha kuwaokoa. Tunawacheka Waethopia vile tunawakamata kila kukicha hapa kwetu, hatujui wala hatuoni vijana wetu wakikumbana na makuu huko ughaibuni,pengine zaidi ya hawa wenzetu hapa
 
Wakuu kwa kifupi ni hivi Dubai kwa sasa hakuna pesa ya kuipata kwa haraka kutokana na janga la Corona ambalo limeathiri dunia nzima.
Kwa hiyo kwanza upatikanaji wa kazi umekuwa mgumu kuna umati wa watu kutoka ghana,kenya,nigeria,ufilipino,bangladesh,india,pakistan wanaranda mitaani kutafuta kazi na hawachagui kazi yoyote ile wanafanya vyeti vinakaa pembeni.
Pili baada ya janga la Corona kampuni nyingi zimeyumba kiuchumi kwa hiyo hata kama utafosi kuipata hiyo kazi malipo yatakuwa ya chini pesa ambayo hata bongo utaweza kuipata,mbali na hivyo malipo hayaji kwa wakati unaweza kufanya kazi miezi miwili au mitatu ndio mshahara unaingia ambayo itakufanya ushindwe kupangilia mambo yako na kuishia kuwa mchumia tumbo,na wakati huo ukishtuka na kuanza kutafuta msaada humpati wa kukusaidia yule agent aliyekuleta hana muda na wewe tena.
Na ukishafikia stage hii ni akiba ya pesa yako ndio itakayokuokoa kwa maana utakuwa na uwezo wa kuachana na kampuni iliyokuleta ukaanze maisha mapya mtaani uanze kusaka kampuni nyingine.
Kwa hiyo hapa nimewawekea wazi kila kitu ili kabla hujakurupuka uchanganue maisha unayoishi bongo ulinganishe na utakayokutana nayo dubai.
Na tena kama una familia mke na watoto ndio usithubutu kabisa utakuja kudharirika hadi ukweni kwenu.
Chaguo ni lako kusuka au kunyoa,nimeweka wazi kila kitu.
 
Ili kupata ajira uarabuni kwenye nchi kama U.A.E na Qatar kupitia kwa agent lazima wakutoze hela baada ya kupata viza na ticket ya ndege.

Na hiyo 600k ni kwa agent karibu 80% ya ma agent wote.
Nimeshaona Kule Malawi pia registered agent wanatoza 200k mwk, ya kule kama fees zao ambayo ni sawa na 600k tz.

Kenya pia fees zao zipo hivyo hivyo sema wako juu kidogo.

Hiyo 600k ni pesa ndogo kama ukilinganisha na utachopata kule. Kwa mfano kama kampuni inakupa free accommodation na Transport plus medical Insurance halafu mshahara wakakulipa 2000 au 3000 riyal ni pesa ndefu sana hiyo.
 
Ok unatakiwa uwe na passport ya kusafiria
Passport size mbili zenye back ground nyeupe
Na yellow fever card ukikamilisha hapo kazi imeisha hyo mwezi mmoja upo Dubai
Kiongozi mimi passport ninayo, na mkwanja unaweza kupatikana. Hizo picha mbili siyo issue. Yellow fever card kama mchongo wa uhakika itapatikana.
Ili kupata ajira uarabuni kwenye nchi kama U.A.E na Qatar kupitia kwa agent lazima wakutoze hela baada ya kupata viza na ticket ya ndege.

Na hiyo 600k ni kwa agent karibu 80% ya ma agent wote.
Nimeshaona Kule Malawi pia registered agent wanatoza 200k mwk, ya kule kama fees zao ambayo ni sawa na 600k tz.

Kenya pia fees zao zipo hivyo hivyo sema wako juu kidogo.

Hiyo 600k ni pesa ndogo kama ukilinganisha na utachopata kule. Kwa mfano kama kampuni inakupa free accommodation na Transport plus medical Insurance halafu mshahara wakakulipa 2000 au 3000 riyal ni pesa ndefu sana hiyo.
Mkuu kila kitu naweza kukipata, nahitaji connection ya hao madalali. Hata kenya naweza kufika maana mara nyingi sana huwa naenda sirari, so kuvuka siyo issue.
 
Njia rahisi ya kupata mishe huko ni kwenda mwenyewe kwa nauli yako na fedha za kujikimu kwa muda utakaokuwa unatafuta kazi,

Agent yyyte anayetaka pesa ili akufanyie mchongo wa kazi huko nje achana naye ni magumashi.. toka lini wewe ukahitaji house girl aje mjini kukufanyia kazi , harafu huyo anayekutafutia house girl, amuombe hela house girl ili apate kazi mjini? Huwa haipo hivyo ... haaa ma agent wanalipwa na kampuni... na wewe ndio bidhaa wanayoiuza!, hupaswi kulipia ..

Bora mtu ukaenda mwenyewe na kutafuta kazi yenye maslahi utakayoona itakufaaa..

Kila la kheri nikisepa nitakutag!!
Gharama za kwenda kwa kutumia nauli na malazi ya siku kadhaa unatakiwa kuwa na kiasi gani cha pesa
 
Nimekaa nikafikilia maisha yamenipiga, kazi niliyokuwa nayo haikidhi kabisa mahitaji yangu ya kila siku, nina mke, nina mtoto, ninao ndugu wanao nitegemea, baba, mama na wadogo zangu mbaya zaidi mimi ndie kaka mkubwa wa familia, najiona kabisa nimeanguka, najiona napoteza uelekeo kila kukicha, nimekuja humu najua kuna watu wa hadhi na kariba tofauti tofauti, maana waswahili husema "mficha maradhi kifo humuumbua"

Nimehangaika kutafuta kazi, ni kweli nipo kwenye kazi ambayo mshahala ni 250k baada ya makato, huo mshahala unanifanya niishi kwa madeni hata kabla sijaupokea unakuwa teyari umeshaisha, sasa ndugu zangu kwa umri wangu huu 25+ najiona kabisa ndoto zangu hazitotimia, nikiwa na akili timamu ninaomba kwa yeyote mwenye connection ya ajira, ata ya ULinzi, na nyinginezo kwenye nchi za kiarabu haswa Doha, Qatar anisaidie pengine huko maslahi yanaweza kuongezeka.

Nimejaribu kufuatilia kwenye mitandao nakutana na maagency ambao wapo nchi za jirani inakuwa ngumu kwangu kuwafikia kwani wengi wao wapo Kenya ama Uganda.

Ndugu zanguni ni matumaini yangu kilio changu kiapatiwa ufumbuzi.

Elimu yangu ni ya kidato cha nne, sijasoma kihivyo ila ujinga wa kuelewa kingereza kidogo nimeuondoa hivyo ninaweza kingereza japo si sana.

VILE VILE mimi ni dereva wa magari...mwenye leseni yenye daraja A, A2, B, C1, C2, C3, D, E

Huku hawajaali elimu kwa kazi ya security ila lazima upite kwa agent na tanzania hakuna agent mimi nilipitia kenya Kuja Qatar
 
Back
Top Bottom