Msaada, mwanangu ghafla haongei

mabwiku

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
447
389
Habari wanajanvi,

Samahani kama uzi upo sahihi ama la mnivumilie kwa uandishi naweza kukokesea kutokana na hali niliyonayo kwa sasa sipo sawa.

Nina watoto mapacha wawili wakiume na kike wote wanasoma shule moja boarding ni yakanisa wapo darasa la pili wote.

Juzi tulipigiwa simu shule mtoto kaanguka kapelekwa hospital yupo hoi haongei, hawezi kukaa, hawezi kufanya chochote, wamechukua vipimo hakuna ugonjwa wa aina yoyote ule, nikachukua maamuzi kumpeleka hospital kubwa lakini bado hawaoni ugonjwa, zaidi wamesema ana kifua kikuu.

Kidogo maendeleo yake sio mabaya, kwa sasa anaweza kula chakula, ukimuongelesha anasikia kwa kutikisa kichwa, lakini hawezi kujibu akijaribu kuongea hawezi ulimi unakua mzito.

Kesho nimeomba waturuhusu nimpeleke kwenye maombi maana naona sio hari ya kawaida, dada yake miezi mitatu iliyopita alikutwa na kifua kikuu, leo kaka yake nae kakutwa na kifua kikuu kutoka shule, haya magonjwa naona ni mazito sana kwao.

Naomba kama kuna mtu aliwai kukutana na shida kama hii naomba mawazo uliwezaje kutatua hii changamoto?

Kesho mungu akisaidia nitampeleka kwenye maombi..
 
Shida imeanza ulipompeleka mtoto ambaye anahtaj malez ya wazaz nyie mkawasusia wengne wawalelee

Kwel mtoto wa miaka 7 akakae boarding?

Hapo hata chanzo Cha tatizo huwez pata sababu hakuna kati yenu aliye karibu na watoto sio mama wala baba
 
Samahan mkuu kwanini umewapeleka boarding wakiwa wadogo hivyo?? Na mgonjwa wa kifua kikuu si anatakiwa atibiwe hospital na sio kwenye maombi?
 
Habari wanajanvi,

Samahani kama uzi upo sahihi ama la mnivumilie kwa uandishi naweza kukokesea kutokana na hali niliyonayo kwa sasa sipo sawa.

Nina watoto mapacha wawili wakiume na kike wote wanasoma shule moja boarding ni yakanisa wapo darasa la pili wote.

Juzi tulipigiwa simu shule mtoto kaanguka kapelekwa hospital yupo hoi haongei, hawezi kukaa, hawezi kufanya chochote, wamechukua vipimo hakuna ugonjwa wa aina yoyote ule, nikachukua maamuzi kumpeleka hospital kubwa lakini bado hawaoni ugonjwa, zaidi wamesema ana kifua kikuu.

Kidogo maendeleo yake sio mabaya, kwa sasa anaweza kula chakula, ukimuongelesha anasikia kwa kutikisa kichwa, lakini hawezi kujibu akijaribu kuongea hawezi ulimi unakua mzito.

Kesho nimeomba waturuhusu nimpeleke kwenye maombi maana naona sio hari ya kawaida, dada yake miezi mitatu iliyopita alikutwa na kifua kikuu, leo kaka yake nae kakutwa na kifua kikuu kutoka shule, haya magonjwa naona ni mazito sana kwao.

Naomba kama kuna mtu aliwai kukutana na shida kama hii naomba mawazo uliwezaje kutatua hii changamoto?

Kesho mungu akisaidia nitampeleka kwenye maombi..
Muache atibiwe hospitali, kama kuombewa aombewe tu uko kanisani lkn mgonjwa skiwa hospitali
 
Watoto wadogo Sana kuwapeleka boarding.
Wanahitaji malezi ya nwazazi.na tatizo limeanzia shule.
 
Hivi mtoto unampeleka boarding huko darasa la pili inakuwaje kuwaje aisee?

huwa nashindwa kuelewa haya mambo.
Watu wanakimbia majukumu mume kazini mke kazini watoto wanalelewa madarasani!

Tupo kwenye kizazi kibaya kinachotafuta mafanikio zaidi kimuonekano kuliko kuwa na familia bora,wewe mwenye mtoto vumilia omba Mungu mtoto atapona ila tambua wewe ndiye mwenye jukumu la kumuangalia mwanao kwa 100 percent.
 
Pole sana. Mungu akupe mwongozo sahihi wa kukabiliana na hilo tatizo

Wapendwa huu sio muda sahihi wa kumhukumu, kwanza hatujui mazingira yaliyosababisha kuwapeleka boarding school. Kikubwa anachohitaji kwa sasa ni ushauri na faraja yetu
 
Daah mtoto boarding mdogo Sana. Sheria ya boarding kwangu ni form One.
 
Watu wanakimbia majukumu mume kazini mke kazini watoto wanalelewa madarasani!

Tupo kwenye kizazi kibaya kinachotafuta mafanikio zaidi kimuonekano kuliko kuwa na familia bora,wewe mwenye mtoto vumilia omba Mungu mtoto atapona ila tambua wewe ndiye mwenye jukumu la kumuangalia mwanao kwa 100 percent.
Sidhani kama jibu hili litanisaidia chochote,ungenipa mwongozo ungenisaidia sana kuliko kunihukumu,mimi ni baba,kama wewe unaishi na familia yako mume/mke pamoja mshukuru mungu ndugu yangu,kila mtu kuna maisha anapitia ndugu,ni muda tu utasema
 
Back
Top Bottom