Msaada: Mtoto mchanga kuharisha na kulia usiku kucha

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
3,030
3,324
Habari wakuu,

Naomba msaada wa mawazo, Mungu ametujalia mimi na mke wangu tumepata mtoto. Ila ana siku mbili halali kabisa usiku. Analia tu na ana harisha kamba kamba kama makamasi. Hospital wanasema ni kawaida eti kwa mtoto mchanga.

Sasa nashindwa kuelewa kawaida kivipi mtoto kutokufunga jicho kabisa usiku analia tu hadi sauti inakauka.

Mtoto ana siku saba tangu azaliwe.

Nisaidieni nifanyeje wakuu.
 
Acha upuuzi mpeleke mtoto hospital haraka. Watoto kuharisha wanakata moto fasta, kulia usiku kucha dalili mbaya kuwa anaumwa Halaf unaandika JF kwanza kimbia hospital acha mchezo na ubahili.
 
Wababa wengine wajinga kweli mtoto analia usiku kucha na kuharisha badala umpeleke hospital Kwa daktari unaanzisha Uzi, useless father
 
Mkuu,umeenda hospitali gani?Mtoto kulia ni ama njaa,ugonjwa.Njaa mara nyingi unakuta maziwa ya mama hayatoki vya kutosha.Ugonjwa lazima utakuwa unampa maumivu/discomfort.

Ushauri kwanza siku saba ni veri delicate so ni muhimu umuone daktari wa watoto.Hata hivo nikuulize analia usiku tu au analia usiku halafu mchana katulia?Kama jibu ni hivyo basi inabidi Ukeshe naye umbembeleze maana......
Kuna wakti watoto wanaona vituko vya hii dunia vya usiku kama wanga,wachawi,walozi etc na kujikuta wanalia maana hakuna lingine wanaweza kufanya.

Nafikiri hapa jukwaani kuna wataalamu wa Ndumba kama Mshana Jr wanaweza pia kukushauri maneno ya kumwambia au kufanya ili aache kulialia...

Hongera kwa kuwa baba and I bet ni First born.
 
Acha upuuzi mpeleke mtoto hospital haraka
Watoto kuharisha wanakata moto fasta ,kulia usiku kucha dalili mbaya kuwa anaumwa Halaf unaandika jf kwanza kimbia hospital acha mchezo na ubahili
Hospital wanasema ni kawaida kwa mtoto mchanga boss...
 
Mkuu,umeenda hospitali gani?Mtoto kulia ni ama njaa,ugonjwa.Njaa mara nyingi unakuta maziwa ya mama hayatoki vya kutosha.Ugonjwa lazima utakuwa unampa maumivu/discomfort.

Ushauri kwanza siku saba ni veri delicate so ni muhimu umuone daktari wa watoto.Hata hivo nikuulize analia usiku tu au analia usiku halafu mchana katulia?Kama jibu ni hivyo basi inabidi Ukeshe naye umbembeleze maana......
Kuna wakti watoto wanaona vituko vya hii dunia vya usiku kama wanga,wachawi,walozi etc na kujikuta wanalia maana hakuna lingine wanaweza kufanya.

Nafikiri hapa jukwaani kuna wataalamu wa Ndumba kama Mshana Jr wanaweza pia kukushauri maneno ya kumwambia au kufanya ili aache kulialia...

Hongera kwa kuwa baba and I bet ni First born.
Ni second born. Mchana angalau analala na kutulia tofauti na usiku mkuu.

Nafanya utaratibu niende hospital kubwa zaidi
 
Kawa we ni daktari halafu umetupia neno la wanga na wachawi. Upokonywe leseni
 
Ni second born. Mchana angalau analala na kutulia tofauti na usiku mkuu.

Nafanya utaratibu niende hospital kubwa zaidi
Okay Mpeleke hospitali,Ila Pia kama mchana analala vizuri na ananyonya vizuri na kuharisha sio kwa sana mpeleke hospitali just in case kwenye huko kuharisha.Mwambie meme awe anasafisha ziwa kabla ya kumnyonyesha pamoja na kuoga na aepuke kutumia manukato na azingatiwe usafi wa mazingira ya mtoto.

OVA
 
Nashukuru sana kwa maneno yako mazuri.
Ndio uache uzwazwa utakuja kuua mtoto Kwa uvivu, nenda hata hospital nyingine, hafu ukute mama Hana maziwa. Yani unapata usingizi mtoto akilia na kuharisha usiku kucha,kuwa na huruma aisee
 
Asante Mkuu
 
Watoto wachanga ni kazi sana kuwatunza kama hujawekeza muda na gharama zako hapo, mfano unasema anaharisha ila hujasema anajisaidia mara ngapi maana ndani ya siku Saba mtoto ajisaidie kwa siku hata mara Saba na Kuna rangi za kinyesi zinabadilika kadili uchafu aliokula tumboni unavyoisha.

Kingine kulia mtoto mchanga umechagua usiku tu, wakati mtoto akiwa na tatizo atasumbua muda mwingi na hapo mzazi anatakiwa kuwa na ujuzi wa kuangalia mtoto mchanga, maana inaweza kuwa njaa hashibi, inaweza kuwa joto la mwili lipo juu labda kazaliwa na tatizo kama homa, inaweza kuwa chango la watoto wachanga hapo ni mzazi anatakiwa kuelewa jinsi ya kumwangalia mtoto wake maana hata ukiuliza bila ujuzi siyo kila mtu atakupa ukweli na wengine wataona ni Bora uteseke ukome hata kama anajua kitu anaweza kukujibu uongo hivyo mambo ya mtoto mchanga nenda kapate elimu kwa Dr wa watoto au mtu mzima unayeelewana naye ili ukiwa unaona mabadiliko ya mtoto yasiyo sawa unajua utatueje kama ni kupeleka hospital Moja kwa Moja au anaweza kupata huduma ya kwanza nyumbani na akawa sawa.
 
Back
Top Bottom