Msaada: Mtaji kiasi gani unahitajika biashara ya kukaanga nyama ya kuku?

Julius Husseni

JF-Expert Member
Sep 9, 2016
1,364
1,078
Nimepitia katika makundi ya wafugaji wa kuku naona wana kuku wengi sana wanatangaza kuuza.

Sasa najua JF ni jukwaa pana sana, wapo watu wanajua kuanzia mtaji, mahitaji, faida na hasara za biashara hii.

Nisaidiwe kijana mwenzenu, ajira ni ngumu tunakosa kila mwaka, kwahiyo ngoja tupambane upande wa pili.

Asanteni.
 
Anza ...kikubwa ujue kuwakaanga vye ma na kutia spicy sauce za kunukia ..ili hata mtu akiwa hana mpango wa kununua ajikute ananunua kilazima...pia izingatia usafi na bei isiwe kubwa sana...mwanzoni unaweza.ukaanza Kwa kuifanya kama unawagawa Bure (rudisha pesa ya mtaji na gharama za kuandaa tu, faida usiiweke sana kipaumbele) ukishakamata soko lako unaanza kupandisha mdogo mdogo mpaka kuanza kupata real profit
 
Mahitaji boss nini na nini
 
Umenikumbusha kuna siku nlipita njiani mama mmoja anakaanga kuku, wala sikujali nikapita....jinsi navozidi kwenda mbali nilisikia wananukia yani utadhani harufu inanifata, asee nilirudi kununua
 
Biashara nzuri chamsingi tafuta location nzuri yanye watu wengi,pale mbezi magufuli huwa wana kuku choma safi kabisa.
 
Nimepitia katika makundi ya wafugaji wa kuku naona wana kuku wengi sana wanatangaza kuuza.

Sasa najua JF ni jukwaa pana sana, wapo watu wanajua kuanzia mtaji, mahitaji, faida na hasara za biashara hii.

Nisaidiwe kijana mwenzenu, ajira ni ngumu tunakosa kila mwaka, kwahiyo ngoja tupambane upande wa pili.

Asanteni.
Ukipata karibu na maeneo ya stendi itakuwa vizuri zaidi.
Wakati huo unakaanga kuku kwa pembeni tafuta kijana awe anatengeneza maandazi na machapati yale makubwa yanayouzwa 500 kwa pisi moja utakuja kunishukuru baadae,watu wa bodaboda ndio chakula chao wakiwa kijiweni watajazana kununua hapo.
Maeneo ya stendi ya mtaani kwetu kuna wachaga fulani wanatengeneza haya maandazi na machapati aisee wako bize kama kiwandani wanakusanya hela.
 
Nimepitia katika makundi ya wafugaji wa kuku naona wana kuku wengi sana wanatangaza kuuza.

Sasa najua JF ni jukwaa pana sana, wapo watu wanajua kuanzia mtaji, mahitaji, faida na hasara za biashara hii.

Nisaidiwe kijana mwenzenu, ajira ni ngumu tunakosa kila mwaka, kwahiyo ngoja tupambane upande wa pili.

Asanteni.
Nadhani unawajua wachoma mishkaki ile ya 100. Sasa kawachunguze vizuri alafu tafuta vifaa....
Jiko la kuchomea kama yale yale ya mishkaki.
Mkaa.
Mafuta kidogo.
Ndoo kubwa mbili.
Viungo.
Kuku wenyewe.
Location( ambayo naamini mpaka sasa unayo kichwani)
Vikorombwezo kadhaa utakavyoona kwa wafanya biashar awenzako.....

Kata vipande piga hesabu zako vizuri alafu anza kazi.
Kama unajua kupika chapati nzuri basi itakua ni safi zaidi maana tupo tunaopenda chapati na nyama choma sio kukaanga ni kuchoma ila viungo vihusike vizuriiiii...
 
Back
Top Bottom