Msaada: Mpenzi wangu nahisi ni tapeli

Msaada: Mpenzi wangu nahisi ni tapeli

Kaa nae chini uongee nae pengine ana shida ambazo wewe hajakuambia. Kuna wakati unaweza kuwa unahitaji kitu lakini baadae unajikuta una jambo lingine la muhimu zaidi kuliko hilo ulilokuwa umepanga.
 
Bado unamwita MPENZI??? Mimi nadhani mpenzi hawezi kuogopa kukuambia babe nimeipenda perfume naiomba au achukue vitu bila kusema
Kwa maelezo yako huyo ni MDOKOZI au KIBAKA
 
Kaa nae chini uongee nae pengine ana shida ambazo wewe hajakuambia. Kuna wakati unaweza kuwa unahitaji kitu lakini baadae unajikuta una jambo lingine la muhimu zaidi kuliko hilo ulilokuwa umepanga.
Tatizo lake nikutokuwa mkweli, awe mkweli tu Mimi nitamuelewa
 
Hayo mashuka bado unayo?
Ninayo nikamwambia nanunua nakuletea nimefika nampigia simu hataki kupokea mwisho kazima simu, na nikimpigia hapokea na sms hataki kujibu.
 
Huyo ana shida ya pesa! Unampa hela kidogo wewe utakuwa! Mpaka hana sabuni!!
Tatizo lake anaomba pesa yakununua vitu, alafu vitu siyoni hakinunua bora asinitajie vitu, yeye aniombe hela kuliko kuniambia nimpe hela akanunue godoro alafu nisilione godoro lenyewe, kwa wewe ungemfikiliaje
 
Kutafuta nae suruhu hapo ni ngumu sana, labda kama utakubali kua lolote lile na liwe kwa baadae. Vitu kma sabuni, perfume u aweza potezea. Lkn kwenye kumnunulia mashuka halafu hataki kuyapokea ndo matatizo yanalianzia hapo, pia kutotumia majina yake halisi pia ni shida, kuna uwezekano mkubwa kua hata ww umedanganywa jina halisi, siku atakufanyia tukio halafu utashindwa kwa kumpata. Pia inaonekana kwa tabia za uongo hauko peke yako, mtakua mnashare na wanaume wengi. Na hayo mambo anawafanyia watu wengi sio ww tu.

Kitu muhimu, usimuache nyumbani kwamo peke ake, hakikisha unatoka nae, usimwamini sana hata kma unampenda.

Mwisho, uchumba sio ndoa, achana nae tu, huyo kubadilika ni mpaka maisha yamkunje haswaa, au itokee kapata mimba ndo labda anaweza kutulia, lkn tofauti na hapo ndugu yangu jiangalie utakuja kupigwa geto zima.

Nb: usimwamini mwanamke Muongo kupitiliza, na asie tumia majina yake halisi, hawanaga mapenzi ya kweli, ila ni wadangaji mashuhuri ko kila mwanaume anatajiwa jina lingine ili msigunduane hata kwa bahati mbaya.
 
Pole sana mkuu,japo vinachekesha... Well huyo ni mdokozi na mwizi na hapo ukute kakuibia vingi labda tu vingne hujashtukia
 
jingine kaniambia simu yake mbovu
Hili tabia wadada wengi wanayo. Wanachofanya wanaficha simu zao anakuja ghetto na kitochi akipewa hela anazitumia kwa mambo mengine halafu siku nyingine anakuja na simu yake ile ile
 
Kama ana-cheat hadi kwenye jina huyo ni viwango vingine, nadhani mheshimiwa kuwa nae ,unafanya mchezo wa kubet, tena umebeti nyumba pekee ya urithi
 
Back
Top Bottom