Msaada: Mke wangu ameanza ushirikina

Msaada: Mke wangu ameanza ushirikina

Kutwa nzima umeshinda kazini,pengine nguo zina majasho na mavumbi halafu unataka umshike mtoto? Hata mimi.nisingekupa mtoto mpaka uoge.
Wala sio kuwa ni hofu ya kuwa na janaba,bali ni ustaarabu tu wa kawaida. Mwenyewe nikiwa na mtoto mdogo nikitoka nitokako huwa naingia bafuni naoga nabadilisha nguo ndio namshika mtoto na kumhudumia.
 
Unafanya kazi gani? Mtoto kinga yake ya kiafya ni dhaifu, mkeo anahakikisha uchafu wowote wa mitaani unautoa kabla ya kumshika mtoto.
Ni kweli,jamaa huwenda amekulia kwenye familia inayoamini sana ushirikina ndio maana mawazo yake yameenda hukohuko
 
Anaogopa utambemenda mtoto na ukiona hvyo hakuamini
 
Wife ameshapata taarifa jinsi unavyowagalauza mabeki tatu kwenye mapagali anataka amuepushe mtoto usije ukamkira.
 
Wakuu Mke wangu ameniambia nisiwe namgusa hata kumbeba mtoto wetu Mara baada ya kutoka kazini eti mpaka nioge nimeshangazwa sana hili mi naona anataka kujifunza tabia ya Ushirikina hili amerudi nalo kutoka huko kwa mama yake alikokwenda Kujifungulia/kujisikilizia.

Nifanyeje wadau nimemuuliza sababu hajaniambia nikiwa kama Kichwa cha familia nakwazika na hili hadi nioge nibadilishe nguo hapo ndo nakua na ruhusa ya kucheza na mtoto nitakavyo weekend Hali hii inakua haipo kwa sababu nashinda nyumbani.

Msaada wenu wakuu.

Hakuamini anajua unachepuka
 
Kutwa nzima umeshinda kazini,pengine nguo zina majasho na mavumbi halafu unataka umshike mtoto? Hata mimi.nisingekupa mtoto mpaka uoge.
Wala sio kuwa ni hofu ya kuwa na janaba,bali ni ustaarabu tu wa kawaida. Mwenyewe nikiwa na mtoto mdogo nikitoka nitokako huwa naingia bafuni naoga nabadilisha nguo ndio namshika mtoto na kumhudumia.
Sasa mwanangu akija kunipokea getini kwa mbwembwe zote nimkimbie jamani???
 
Wakuu Mke wangu ameniambia nisiwe namgusa hata kumbeba mtoto wetu Mara baada ya kutoka kazini eti mpaka nioge nimeshangazwa sana hili mi naona anataka kujifunza tabia ya Ushirikina hili amerudi nalo kutoka huko kwa mama yake alikokwenda Kujifungulia/kujisikilizia.

Nifanyeje wadau nimemuuliza sababu hajaniambia nikiwa kama Kichwa cha familia nakwazika na hili hadi nioge nibadilishe nguo hapo ndo nakua na ruhusa ya kucheza na mtoto nitakavyo weekend Hali hii inakua haipo kwa sababu nashinda nyumbani.

Msaada wenu wakuu.
Acha akuroge tu mana ameona akili zako kma za bashite
 
Si ushirikina perse ila ni imani za kimila ikiamini kama mwanaume utapiga mechi za nje wife akiwa na mtoto mdogo ukija kumshika mtoto hatokuwa na afya njema ila sijui kama kuna connection hapa ama ni imani za wazee wetu.....Kali zaidi ni ile wife akiwa Labour Ward anajifungua wewe mume wake haitakiwi ujifunge mkanda wa suruali kama upo karibu na kina mama wa makamo watakuja kukutoa huo mkanda chap....
Nakusalim
 
Acha uboya wewe unataka mtoto awe kilema umetoka uko na majanaba yako unataka ummbebe mtoto mke yuko sahihi oga kwanza by pirates Lily
 
Back
Top Bottom