Msaada: Mke wangu ameanza ushirikina

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Wakuu,

Mke wangu ameniambia nisiwe namgusa hata kumbeba mtoto wetu Mara baada ya kutoka kazini eti mpaka nioge, nimeshangazwa sana hili mi naona anataka kujifunza tabia ya ushirikina hili amerudi nalo kutoka huko kwa mama yake alikokwenda kujifungulia/kujisikilizia.

Nifanyeje wadau nimemuuliza sababu hajaniambia, nikiwa kama kichwa cha familia nakwazika na hili hadi nioge nibadilishe nguo hapo ndo nakua na ruhusa ya kucheza na mtoto nitakavyo, weekend hali hii inakua haipo kwa sababu nashinda nyumbani.

Msaada wenu wakuu.
 
Wakuu Mke wangu ameniambia nisiwe namgusa hata kumbeba mtoto wetu Mara baada ya kutoka kazini eti mpaka nioge nimeshangazwa sana hili mi naona anataka kujifunza tabia ya Ushirikina hili amerudi nalo kutoka huko kwa mama yake alikokwenda Kujifungulia/kujisikilizia.

Nifanyeje wadau nimemuuliza sababu hajaniambia nikiwa kama Kichwa cha familia nakwazika na hili hadi nioge nibadilishe nguo hapo ndo nakua na ruhusa ya kucheza na mtoto nitakavyo weekend Hali hii inakua haipo kwa sababu nashinda nyumbani.

Msaada wenu wakuu.
Kwanza hongera kwa kupata mtoto.

Pili
Huo sio ushirkina ni mambo ya kimila ....

Anahisi kwamba huko unakotoka unaweza kuwa umefanya ngono na wanawake wengine hivyo ukimshika mtoto kabla hujaoga unaweza sababisha maneno mengine mabaya kwa mtoto.
 
Kama wewe ni kicheche hujatulia haina haja ya kuja kulalamika humu.

Ikiwa mtoto wenu ni wa kwanza na tabia zako ni nzuri jua mkeo amelishwa maneno mengi kwao kiasi kwamba atakubana mpka umchukie(yeye akijua anajenga kumbe anabomoa). Tafuta mtu mzima kwenu au mtaan kwenu ongea nae upate ushauri mzuri zaidi.
 
Si ushirikina perse ila ni imani za kimila ikiamini kama mwanaume utapiga mechi za nje wife akiwa na mtoto mdogo ukija kumshika mtoto hatokuwa na afya njema ila sijui kama kuna connection hapa ama ni imani za wazee wetu.....Kali zaidi ni ile wife akiwa Labour Ward anajifungua wewe mume wake haitakiwi ujifunge mkanda wa suruali kama upo karibu na kina mama wa makamo watakuja kukutoa huo mkanda chap....
 
Ndio uoge kwasababu siku unaweza chepuka huko nje ukamshika mtoto na ukambemenda huyo mkeo hana ushirikina wowote ni mtu mzuri na anawapenda watoto wake good woman
 
anaogopa usije ukambemenda mtto na ww utakua mtu wa michepuko ndio mana umeambiwa hivyo
 
kwani michepuko inahusiana vipi na mtoto jaman maana me sioni relationship ya mimi kuchepuka na mtoto wang

izo pia ni iman potofu......mkuu mtoto ni wako sio wake una haki ya kumshika muda wowote na sehemu yoyote

almuhimu haumzuru mtoto au kama kazi zako ni kama fundi gereji au mzibua vyoo ni muhimu ukaoge

ama mvuvi maana wavuvi wananuka wewe yaaan karo ilooh
 
Wakuu Mke wangu ameniambia nisiwe namgusa hata kumbeba mtoto wetu Mara baada ya kutoka kazini eti mpaka nioge nimeshangazwa sana hili mi naona anataka kujifunza tabia ya Ushirikina hili amerudi nalo kutoka huko kwa mama yake alikokwenda Kujifungulia/kujisikilizia.

Nifanyeje wadau nimemuuliza sababu hajaniambia nikiwa kama Kichwa cha familia nakwazika na hili hadi nioge nibadilishe nguo hapo ndo nakua na ruhusa ya kucheza na mtoto nitakavyo weekend Hali hii inakua haipo kwa sababu nashinda nyumbani.

Msaada wenu wakuu.

Wewe ndio una mawazo ya kishirikina, mkeo yuko makini kwa afya ya mtoto.Ukitoka nje huko ni vizuri kubadiri nguo, kuoga au kujisafisha kwa ujumla usije leta maambukizi kwa mtoto wenu.
 
Back
Top Bottom