MSAADA: Mke kila harusi anayoalikwa lazima avae sare

malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
1,846
1,351
Habari wakuu,

Msaada kidogo wa mawazo, mke wangu kila harusi atakayoalikwa na kuchangia lazima atashona sare inayovaliwa katika harusi hiyo. Hata ziwe harusi 6 kwa mwezi zote atavaa sare.

Nimekuwa nikishauri na kukanya lakini wapi, amekuwa akifanya kwa siri na kuhakikisha lazima avae sare ya kila harusi.

Wakuu mchango wenu wa mawazo wa kushughulika na mke wa namna hii.
 

shantui

Member
May 18, 2022
35
61
Nilishawah kuwa na mahusiano na mwanamke wa aina hiii ambaye tulipanga kuoana yani kila shughuli lazima ahakikishe anahudhulia na sare anashono, ikaona isiwe kesi, sikutaka ushaur popote nilikaa chini nikatafakari nikaona kumuacha ni sahihi basi nikaachana nae kwa aman pasipo yeye kujua chanzo mpk leo hii na tunawasiliana vzr tu.

NB: Yule dada alikuwa anapenda sherehe na show off hakuna mfano jamn mmmmmh.
 

Mpinduameza

Member
Aug 6, 2022
50
98
Mke kavaa sare anapendeza sasa shida iko wapi au uchumi hauruhusu? Ingekuwa mimi mwanzo wa mwezi nampa pesa ya sare maana kwa kusema anashona kisirisiri sio salama kwako mwanaume lazima uhusike kwa kila kinachomhusu mkeo masela wasije chukua jimbo kimasihara uje kuru ruka hapa utuchoshe.
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,655
3,558
Kama kipato kinaruhusu muache aji enjoy lakini kama kipato hakiruhusu ongea naye. Na kama hamna mipango ya kutumia fedha kama ujenzi, uwekezaji n.k...anzisha mipango.



 

LIKE

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
4,715
9,742
Umenikumbusha. Wa kwangu alikuwa na tabia hizo...nilipiga kelele hadi nikapoa

ila nikijua nilivyosota na maisha niliamua kumbadilikia, nilianza kumtukana matusi yote nikiwa tungi.

Alikoma.

Sasa hivi anashona sare za vikoba au wanazengo tu...na Amani inatawala.
 
12 Reactions
Reply
Top Bottom