MSAADA: Mke kila harusi anayoalikwa lazima avae sare

Habari wakuu,

Msaada kidogo wa mawazo, mke wangu kila harusi atakayoalikwa na kuchangia lazima atashona sare inayovaliwa katika harusi hiyo. Hata ziwe harusi 6 kwa mwezi zote atavaa sare.

Nimekuwa nikishauri na kukanya lakini wapi, amekuwa akifanya kwa siri na kuhakikisha lazima avae sare ya kila harus.

Wakuu mchango wenu wa mawazo wa kushughulika na mke wa namna hii.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app

Tatizo hapa ni kuchangia kila sherehe au kwenda kila sherehe au kushona sare kila sherehe? Kwenye hizo sherehe wewe huwa unachangia? Sioni kosa lolote mtu kuvaa sare na kupendeza labda kama kwenye hizo sare wewe ndio unagharamika!
 
Nenda naye taratibu, atachoka na ataacha mwenyewe tu. Ukimkataza unaongeza mafuta! Jaribu kuwa kama mchagga, unafiki! Msifie sana kila wakati hadi aone kero ataacha
Unampoteza mwenzio...!! Jamaa awe straight yanii
 
Niliwah pita home nikakuta maza kawaachia madogo elfu 2 waitumie kwa siku tano,yeye kaenda kwenye shuhuri na kasuka nywele za gharama nilichoka,nikawaza kuwa maza etu na umri wote huo bado anapenda kupata sifa za umependeza

Aiseeeee.........
 
Habari wakuu,

Msaada kidogo wa mawazo, mke wangu kila harusi atakayoalikwa na kuchangia lazima atashona sare inayovaliwa katika harusi hiyo. Hata ziwe harusi 6 kwa mwezi zote atavaa sare.

Nimekuwa nikishauri na kukanya lakini wapi, amekuwa akifanya kwa siri na kuhakikisha lazima avae sare ya kila harus.

Wakuu mchango wenu wa mawazo wa kushughulika na mke wa namna hii.

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Gharama za nani?
 
Pole sana mke ni Mali ya familia, jamii na aina ya ndoa mfano wachunaji, pia kuna washenga sijui umepitia ngazi zipi hadi hapo. Pole sana mwamba, pesa anatumia zako, zake, anatoa katika miradi yenu? Unahistoria yoyote ya kufumania akiomba pesa Kwa michepuko na je ana history yoyote ya kuchepuka? Ruhusa ya kuhudhuria hizo harusi unampa au anajiamulia?!
 
Anatumia zangu,Hana historia yakuchepuka na pia ruhusa Nampa mwenyewe

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Hapo huna jinsi tayari huo ushakuwa ulevi wake! Suluhu yake haitaki kukurupuka, anza na kutrack background yake ni vitu gani alivipenda maishani na akavikosa kwa wakati wake
Na pia akiwa harusini ni mwanamke wa tabia gani, ana dalili za michepuko, na je upambanaji wake kutafuta pesa unawiana na matumizi? Anapata wapi hizo pesa?
 
Back
Top Bottom